Habari Mbaya: Mkurugenzi wa Meatu achomewa nyumba yake, yote yateketea

Hao labla ni ccm tu sasa wanataka Chadema wakamatwe. Walichoma ofisi za Chadema Arusha na Mbeya lkn polisi bado waliwakamata wafuasi wa Chadema.

Polisi wa nchi hii hawana weledi wa kufanya kazi za kipolisi wao ni wanasiasa wanaovaa sare za kipolisi.

That's the way I can describe this discredited and disgraced public service personnel.
 
Mkurugenzi wa Meatu mkoani Simiyu amechomewa nyumba yake usiku wa kuamkia leo...

Sijakuelewa. Nchi ni kisiwa cha amani, polisi walete utulivu kwenye nchi ya amani? Kila tukio lina sababu yake. Wakulaumiwa ni waliotufikisha hapa ambapo amani uisemayo ni nadharia. Watawala wa leo ni sawa na yule mwanamke mpumbavu anaetajwa kwenye biblia, mvunja nyumba yake kwa mikono yake mwenyewe.
 
Hizi ndio mambo CHADEMA wanafurahia, wakisikia vurugu roho wao kwatu, wakisikia kuna watanzania wamepata matatizo Mtwara huko kwa kuuliwa wao roho kwatu, wakisikia MKIRU wenyekiti wa vijiji wameuliwa wao roho kwatu, huu upambuvu ni kuendelea kuushughulikia bila huruma, Tz inahitaji vyama mbadala ila sio wapinga maendeleo.
Hebu tuangalie kwa makini hilo kama hivi;

Jirani yako anamega aridhi yako kila wakati, unapompeleka kwa wazee wa baraza na hakimu wanawaketisha na kusawazisha jirani anasema atarudisha sehemu aliyochukua na mkirudi mtaani jamaa anakomaa harudishi na anakwambia kwa kejeri za kutosha.

Inapita muda jirani anamega tena aridhi na kupanda migomba, wkt anapanda unamfuata unapiga picha na kumwambia analofanya siyo sawa huku ukiwaita viongozi washuhudie, wanapofika wanakuta amemaliza kupanda na kaondoka huku akikuachia ujumbe usemao, "Ole wako ung'oe migomba yangu, utanijua vizuri".

Umekwenda kwa mara nyingine ngazi zinazotakiwa na kupata usuruhushi unaoleta majibu same like earlier, baada ya hapo, asubuhi unasikia nyumba ya jirani yako imeanguka au wezi wameingia na kuiba kila kitu!.

👉 Ni nini moyo wako utamwadhimisha Bwana au kuzungumza na mkeo au rafikiyo kutokana na tukio hilo?
 
Nimeshuhudia Kijiji kimoja mkoani Rukwa watu wamegawana soko dogo pale Kijijini. Kulia wànauza na kununua CCM peke yao, Kushoto CHADEMA na ACT.

Naungana na wewe kuwaomba Polisi kwa kutumia falsafa yao ya polisi jamii warejeshe umoja na utangamano miongoni mwa Watanzania maana wengine wanajali madaraka tu.
Hao hao ndiyo wamesababisha na kusherekea aya alafu hao hao ndiyo watatue ili tatizo? Siamini kabisa
 
Lissu akiongelea maridhiano, kuna watu wanambeza, wacha tufike wanakotaka tufike.
Punguani, maridhiano kwa lipi?. Hakuna cha kubembelezana hapa, na wahalifu wote watashughulikiwa ipasavyo. Ongezeni ujinga vichwani mwenu.
 
Mkurugenzi wa Meatu mkoani Simiyu amechomewa nyumba yake usiku wa kuamkia leo...

Polisi hawana la kufanya bali rais wa nchi anajua kwanini haya matukio yataendelea kutokea
Nilishangaaa sana kusikia kijana anahojiwa anasema anatamani hata bunge liungue moto, tumefikia hapo

leo hii madiwani; wabunge; wenyeviti wa mtaaa; DED etc wanaishi kama digi digi, wengi kwenye maeneo hatari hawalalali kwenye nyumba zao

Je, hii ndio Tanzania tunayoitaka?
 
Kwa jinsi mambo yalivyoenda awamu hii, sirikali itapata shida sana kutambua wanaofanya uhalifu huu ni wajumbe au wapinzani
 
Ha ha ha haa.

Hakuna CHATU kadhaa wakutumwa pale mjengoni Dom baadhi ya wahuni wamezwe kabisa??
 
Back
Top Bottom