figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,492
- 54,895
Mkurugenzi wa Meatu mkoani Simiyu amechomewa nyumba yake usiku wa kuamkia leo.
Nyumba yote imechomwa na vitu vyote vilivyomo ndani.
RPC wa Simiyu, ACP Richard Abwao amesema kwenye nyumba alikuwepo mdogo wake na Mkurugenzi Fabian Manonza ndiye aliona moshi ndani na kibaya zaidi gesi nayo ikalipuka.
Mdogo wake na Mkurugenzi ndiye alitoa taarifa kwa askari Polisi waliokuwa kwa Mkuu wa Wilaya.
Kulikuwa na gari karibu na ukuta ambao ulikuwa unawaka moto, Polisi walichukua maamuzi ya kuvunja kioo ili kuondoa handbrake ya gari ,bahati nzuri ufunguo ukapatikana na kuiokoa gari.
Nyumba yote imeteketea na moto. Timu ya Polisi na jeshi la Zimamoto na uokoaji na TANESCO wanaendelea na uchunguzi ili kujua chanzo cha moto huo.
RPC amesema ni mapema kulihusisha tukio hilo na mambo mengine.
Mkurugenzi Fabian Manonza amenukuliwa akisema kuna hujuma sababu inaonekana petrol ilimwagwa kabla ya nyumba kuchomwa. Yeye hakuwepo muda huo nyumba inachomwa.
MY TAKE:
Polisi ifanye jitihaza za kuleta Utulivu Nchini sababu nchi yetu ni kisiwa cha Amani. Iwachukulie hatua wote waliohusika.