Habari leo ni gazeti la CCM?

Nyambala

JF-Expert Member
Oct 10, 2007
4,465
1,170
Napata shida kuamini kama hili ni gazeti la serikali lakini zaidi ya hayo gazeti hili sasa kuna haja ya kulishtaki maana limekuwa likifanya uchochezi na hizi unfounded allegations hasa kwa wapinzani wa CCM.

How come kodi za wananchi zinatumika kufanyia huu upuuzi.

Risasi zarindima Igunga

KAMPENI za uchaguzi wilayani hapa zimeingia sura mpya baada ya matusi majukwaani, vurugu za kumwagiana tindikali na sasa silaha za moto zimetumika.

Katika tukio la hivi karibuni, CCM inaituhumu Chadema kwa inachokieleza ni kuwafyatulia risasi wabunge wake.

Akizungumza katika ofisi za wilaya za CCM, Mbunge wa Viti Maalumu wa chama hicho, Esther Bulaya, alidai kuwa juzi usiku wa kuamkia jana, akitoka Hoteli ya Silent Inn kwenda alikofikia, alifukuzwa na gari la Chadema likiwa na kada wa Chadema, Mwikwabe Mwita ambaye alikuwa akifyatua risasi angani.
- Ghafla imegeuka siyo tena kuwafyatulia risasi wabunge ila ni kufyatua hewani?

Kwa mujibu wa madai hayo ya Ester, baada ya kuona Mwita akifyatua risasi angani, aliogopa kurudi kwenye hoteli alimofikia ya Peak Lodge na kuamua kukimbiza gari kwenda Singida.

"Baada ya kuona wanaendelea kunifukuza, nilimpigia simu Aishi (Hilary, Mbunge wa Sumbawanga Mjini), nikamwambia waje waniokoe nimetekwa naelekea upande wa Singida," alidai Bulaya.
Huyu mwanadada inabidi aone aibu yaani unafukuzwa badala ya kuita polisi unamuita Aishi???? Na huyo Aishi si alikuwa huko peak lodge ambako huyu dada aliogopa kurudi?
Aliendelea kudai kwamba wakati anafukuzwa, gari lake lilipigwa mawe na risasi na kuharibiwa.
Hapa ndiyo penyewe as this can be verified na silaha iliyotumika kujulikana.

Ushahidi wa Aishi Aishi baada ya kupata simu hiyo, wakati akikaribia kufika Hoteli ya Peack Lodge, alidai kuwa alimwambia dereva wake ageuze gari kwenda kumfuata Bulaya na njiani waliona gari aina ya Toyota Double Cabin, likiwa na bendera ya Chadema likifukuza gari la Bulaya
. Yaani hawa wabunge wa CCM bure kabisa, ina maana ukiona gari ina bendera ya Chadema ni ya Chadema, hii staili si ilishatumika 1995 tulipoonyeshwa visu vyenye bendera ya CUF?

"Tukaamua kuwafuatilia lakini baada ya kuona gari langu likiwafuatilia, walikata kona na kuingia porini na kumwacha Esther na sisi tukawafuata na wakazunguka na kutokea katika hoteli yao ambapo geti la hoteli hiyo lilikuwa wazi, lile gari (Toyota Double Cabin) likaingia ndani moja kwa moja," alidai Aishi.
Hivi huyu mbunge anaweza kusimama na Tundu Lisu kuthibitisha hili?

Wakiwa katika eneo hilo na kwa mujibu wa madai yao, walitoa taarifa Polisi, Aishi akadai kuwa
vijana wa Chadema walijitokeza na kulizingira gari lake na mmoja akalifyatulia risasi gari hilo aina ya Toyota Land Cruiser na kuvunja vioo vya nyuma
Yaani inashangaza hizi risasi badala ya kufyatuliwa watu yanfyatuliwa magari, nna wasiwasi sana na umakini wa huyu Aishi.

Chanzo cha ugomvi Chanzo cha ugomvi huo kwa mujibu wa Bulaya, ni mkutano wake wa kampeni za kumwombea kura mgombea wa CCM, Dk. Dalaly Kafumu katika kata ya Itumba.

Alidai akiwa njiani kwenda kwenye mkutano huo, Bulaya ambaye alikuwa na waandishi wawili wa habari katika gari lake, alidai waliona gari la Chadema likiwa limesimama katika nyumba ya mmoja wa viongozi wa CCM.

Aliendelea kudai kwamba alisimamisha gari lake na kwenda kwenye gari la Chadema na kuwakuta viongozi wa Chadema, Reuben Mtausigaye na Musa Hamis wakiwa na karatasi bandia ya kutambua wapigakura na daftari la wapigakura.
"Niliwafuata na kuhoji wametoa wapi nyaraka za Tume ya Uchaguzi (NEC), wakasema wamepewa na uongozi wa Chadema, lakini hawazitumii, niliwanyang'anya na kuzipeleka Polisi," alidai Bulaya.
Yaani hawa wabunge mpaka kichefuchefu, hvi kweli huyu dada naweza kuwanyang'anya karatasi wanaume wawili tena wenaokuwa labelled kuwa ni chama cha fujo?

Aliongeza kwamba Chadema wanatumia fomu hizo kununua shahada ili wananchi wasiende kupiga kura na kwa kuwa siri yao ilishagundulika, wakaanza kuwafuatilia.
Du! kwa hiyo ile hoja ya kufyatuliana risasi imeisha maelezo! C'moon didn't have that much popcorn.

Daftari la wapigakura
Naye Mratibu wa Kampeni za CCM, Mwigulu Nchemba, alidai Chadema wana daftari la wapigakura lenye picha za wapiga kura na wanatembea nalo vijijini, kutisha wapigakura kuwa wasipoipigia kura Chadema, kompyuta itaonesha na watashughulikiwa.
Hivi kuna watu bado wanamsikiliza huyu? Yaani mbinu za CCM leo hii zimekuwa za Chadema?

Alidai kuwa wananchi wamekuwa na woga, kwa kuwa daftari hilo lina picha zao na wanazitumia kuwatisha.

Chadema yajibu tuhuma
Baada ya maelezo ya CCM, gazeti hili lilifika Polisi kupata uthibitisho, lakini kabla ya Polisi kuzungumzia suala hilo, Mkurugenzi wa Sheria wa Chadema na Mbunge wa Iramba Mashariki, Tundu Lissu, aliingia katika kituo hicho cha Polisi na baadaye akatoka nje kuzungumza na waandishi.

Kwa mujibu wa madai ya Lissu, Chadema ndio walivamiwa na vijana wa CCM katika hoteli yao wakiongozwa na Aishi na Bulaya, lakini vijana wa Chadema wakalidhibiti gari la Mbunge huyo wa Sumbawanga.

Kutokana na kudhibitiwa kwa gari lake, Lissu alidai mbunge huyo alifyatua risasi angani, lakini
hakufanikiwa kulichukua gari hilo mpaka Polisi walipofika na kulichukua.

Lissu alisema hali hiyo imewatisha na wakichanganya na kitendo cha mbunge mwingine wa CCM, Ismail Rage wa Tabora Mjini kupanda jukwaani na bastola kiunoni, wameandika barua kwa Msimamizi wa Uchaguzi kuomba CCM na mgombea wake waondolewe katika kinyang'anyiro hicho cha uchaguzi.

Aliwalaumu polisi kwa kutowaweka ndani Aishi na Rage ambao alidai ni wahalifu, na badala yake wakawapekua Mwita na dereva wake na katika upekuzi huo hawakukutwa na kitu.

Lakini pia alikiri kwamba Chadema ina daftari la wapigakura wa nchi nzima na kuongeza kuwa vyama vyote vilipewa na NEC na wanalitumia kudhibiti wapigakura mamluki,
lakini kwa kuwa CCM ni wazee hawajui kutumia kompyuta, ndiyo maana wanalalamika.
I love this line!!!!!!!! Wazee hao lazima walifikiri daftari hilo ni nyara ya serikali.

Polisi na uchunguzi
Mkuu wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathimini wa Polisi Makao Makuu ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Isaya Mngulu, baadaye alisema wanafanya upelelezi wa suala hilo.

Alifafanua kuwa tayari watu wapatao 10, wakiwamo Bulaya, Aishi na Mwita, waliitwa na kuandikisha maelezo na pia waliokota maganda matatu ya risasi za bastola yenye mtutu wa milimita tisa.

Mngulu alisema pia wanashikilia magari ya Bulaya na Aishi na kufafanua kuwa hana hakika kama kuna lililopigwa risasi, lakini la Bulaya, aina ya Prado limetobolewa kioo cha nyuma matundu matatu kwa alichokisema ni mawe na la Aishi, huenda ndilo lilipigwa risasi kwa kuwa vioo vyake vimesambaratika kabisa.

CUF wafurahia
Wakati hali ikiendelea, gari la matangazo la CUF lilipita njiani likiwataka wananchi wa Igunga kuchagua mgombea wake, Leopold Mahona, kwa madai kuwa Chadema na CCM wameshindwa kutunza amani ya Igunga na sasa wanarushiana risasi.
 
Shocking distortion of the truth. Utterly despicable... The editor should be ashamed by letting this go to press!!
 
Shocking distortion of the truth. Utterly despicable... The editor should be ashamed by letting this go to press!!

Truly shocking and self contradicting, I wonder how the editor of this paper still maintain his job!!!!!!!!!
 
Hii ni habari ndani ya mwananchi, yaani completely different. Hawa waandishi wa habari leo ni dalili tosha kwamba jamii ikishakuwa ya kifisadi na kukosa maadili basi effect is all over.

Risasi zarindima Igunga

Wabunge wawili CCM, Waitara wahojiwa polisi

Daniel Mjema, Igunga
HALI ya usalama katika Jimbo la Igunga inazidi kuwa tete baada ya milio ya risasi kurindima usiku wa kuamkia jana katika tukio lenye utata mkubwa, huku vyama vya Chadema na CCM vikiendelea kushutumiana.Wakati CCM) ikidai risasi hizo zilifyatuliwa na Mratibu wa Kampeni wa Chadema, Mwita Waitara, Chadema wanadai risasi hizo zilifyatuliwa na Mbunge wa Sumbawanga mjini, Aishi Hilal wa CCM.

Tukio hilo lilitokea saa 8:00 usiku wa kuamkia jana nje ya nyumba ya kulala wageni ya Misana Lodge ambapo magari mawili aina ya Toyota Landruicer na Toyota Prado yalivunjwa vioo.

Gari hiyo ya Toyota Landcuiser linaelezwa kumilikiwa na Mbunge Hilal na Prado inadaiwa kuwa ni ya Mbunge wa Viti Maalumu CCM, Ester Bulaya, ambaye CCM kinadai kuwa wafuasi wa Chadema walitaka kumteka.
Eneo lilipotokea tukio hilo ndiko ambako wafuasi wa Chadema wanalala ikiwamo kulaza magari yao yakiwamo yanayotumika katika kampeni na magari ya wabunge hao yapo katika Kituo cha Polisi Igunga kwa uchunguzi.

Naibu Kamishina wa Polisi Isaya Mngulu, ambaye ndiye Msemaji wa Polisi katika Uchaguzi Mdogo Jimbo la Igunga alithibitisha jana kuwapo kwa tukio hilo na kueleza kuwa silaha iliyotumika ni bastola yenye kipenyo cha milimita tisa.
"Hatujafanikiwa kuipata bastola hiyo lakini kutokana na maganda mawili ya risasi tuliyoyaokota eneo la tukio, inawezekana silaha iliyotumika ni bastola ya milimita 9,"alisema Mngulu.

Naibu Kamishina huyo alisema tayari watu zaidi ya 10 wamekwishahojiwa na polisi na kuandikisha maelezo yao wakiwamo Wabunge hao wawili, Waitara na walinzi watatu walioshuhudia tukio hilo lenye utata.
"Mpaka sasa hatuwezi kusema vioo vya magari yale vilivunjwa kwa kutumia risasi au mawe na hili ni moja kati ya mambo tunayoyachunguza, ikiwamo ni nani hasa aliyefyatua risasi zile," alisema Mngulu.

Katika tukio hilo, kada mmoja wa CCM aliyekuwamo katika gari la Mbunge Bulaya aliyetajwa kwa jina la Ramadhan Twaha, alidai kuwa amejeruhiwa kwa risasi katika mkono wake wa kushoto na kutibiwa kisha kuruhusiwa.
Lakini Kamishina huyo wa polisi alisema kuwa, asingependa kuingia kwa undani kuhusu tukio hilo, ila polisi wameshaanza uchunguzi.
Kwa mujibu wa Kamishina huyo, polisi walipekua chumba anachoishi Waitara pamoja na cha dereva wa moja ya magari ya Chadema, lakini hawakukuta bastola yeyote ndani ya vyumba vyao.

Eneo kulipotokea tukio hilo ni umbali wa meta 20 hivi kutoka Hoteli ya Peak ambayo wamefikia viongozi wa kitaifa wa CCM.

Maelezo ya Bulaya
Akizungumza na Waandishi wa habari jana, Mbunge wa Viti Maalumu, Esther Bulaya alidai kuwa usiku huo alikuwa ametokea Baa ya Silent Inn akiwa na wabunge wenzake wawili akiwamo Aishi.
Mbunge alidai wakati anatokea katika baa hiyo kuelekea katika Hoteli ya Peak walikofikia viongozi wa CCM, waliona gari ya Chadema ikija mbele yao katika barabara ya lami kuelekea Peak na kuwamulika kwa taa kali.

"Wakawa wanakuja kwa speed (mwendo kasi), ikabidi tuwakwepe. Wakati tunakweoa tuligonga kibao. Baada ya tukio hilo ikabidi dereva wetu ageuze gari tukaanza kukimbilia barabara ya kuelekea Singida," alidai Bulaya.
Alidai kuwa baada ya kuwakwepa, Waitara alitoa bastola na kufyatua risasi hewani kulishambulia gari lao huku vijana wengine wa Chadema waliokuwa wamepakiwa nyuma ya gari hilo, wakirusha mawe.

"Ikabidi mimi nimpigie simu Mbunge Aeshi kumweleza kuwa hawa watu wanataka kuniteka naye akawasiliana na polisi ambao walikuja kusaidia. Baada ya Waitara kuona kuna gari linawafuata wakakimbilia porini," alidai.
Kwa mujibu wa Mbunge huyo, baada ya kuona Waitara na kundi lake wanafuatwa ndipo walipogeuza gari na kurudi hoteli waliyofikia na kuingiza gari lao ndani ya geti na wakati huohuo, polisi wakafika.

Mbunge huyo alidai kuwa Mwita alianza kumwinda yeye na Aeshi muda mrefu. Wengine aliodai kuwa walikuwa wanawindwa ni Mratibu wa Kampeni wa CCM, Mwigulu Nchemba na Katibu Mkuu wa UVCCM, Martin Shigella.
Alifafanua kuwa juzi kabla ya tukio hilo, aliwakamata vijana wa Chadema wakiwa na fomu walizoziandaa kwa lengo la kuorodhesha wapiga kura na kununua shahada jimboni humo, kitendo kilichomuudhi Waitara.

Mbunge Aeshi anena
Mbunge huyo aliwaambia waandishi wa habari kuwa muda mfupi baada ya kuachana na Bulaya, alipokea simu kutoka kwake (Bulaya) akimwarifu kuwa amevamiwa na alikuwa akielekea Singida hivyo aende kumwokoa.

"Kwa hiyo nilimwambia dereva ageuze gari tukaanza kuwafuata nyuma kuelekea Singida na nilipowakaribia nikampigia Esther nikamwambia niko nyuma yake na nimeshalifahamu hilo gari linalomfukuza," alisema.
Alisema baada ya kulibana sana gari hilo liliingia porini naye akalifuata huko na ndipo likageuza kurudi mjini na yeye akaendelea kulifukuza na kwamba, akiwa njiani alikutana na polisi wa doria akawaarifu.

"Polisi nao wakatufuata hadi pale wanapokaa, lakini wanaonekana ni wajanja sana maana tulikuta gati (lango) likiwa wazi gari lao likaingia moja kwa moja hadi ndani na wakati huo polisi wakafika," alidai.
Alidai kuwa wakiwa katika taharuki hiyo, ghafla gari yake ilipigwa kwa risasi kioo cha pembeni ambayo ilipita na kuvunja pia kioo cha upande wa pili na kwamba, tukio hilo lilishuhudiwa na polisi waliokuwa eneo hilo.

Tundu Lissu awageuzia kibao CCM
Mkurugenzi wa Sheria na Katiba wa Chadema, Tundu Lissu, alisema jana kuwa vijana wao ndio waliovamiwa na kundi la Vijana wa CCM wakiongozwa na Mbunge wa Jimbo la Sumbawanga mjini, Aeshi.

"Lengo lao lilikuwa ni kuchoma magari yetu moto, baada ya kugundulika kuwa wameingia katika eneo la hoteli tulipokaa, vijana wetu walianza kupiga kelele na kuizunguka ile gari ya Mbunge wa Aeshi," alisema.

Lissu aliongeza kuwa baada ya mbunge huyo kuona amezungukwa alichomoa bastola na kufyatua risasi hewani watu wakalala chini akatoroka, lakini ile gari yake ilidhibitiwa hadi polisi walipokuja.

Alifafanua kuwa polisi walilichukua gari lile na kumtafuta Mbunge huyo na kumpeleka kituoni.
Lisu alisema anashangaa badala ya polisi kumkamata mbunge huyo kwa matumizi mabaya ya silaha, walimwachia huru. "Badala ya kumweka ndani kama walivyowaweka ndani Wabunge wetu waliotuhumiwa kumvua yule Mkuu wa Wilaya kilemba cha kichwani wakawaachilia na badala yake wanakuja kumpekua Waitara," alisema.

Alidai kuwa mtu aliyetoa taarifa polisi kuwa Waitara ana silaha ni Mbunge Esther Bulaya aliyekuwepo pia kwenye tukio hilo la saa 8:00 usiku na kumtuhumu kwa kuwatukana polisi alipofika kituo cha polisi Igunga."Yule mbunge aliyefyatua risasi yupo huru bunduki yake anayo… na Rage (Ismail) aliyekuwa na bunduki juzi kwenye mkutano wa hadhara yupo huru licha ya makatazo ya tume ya uchaguzi…,"alilalamika.

Alisema jeshi la polisi linatumika kama chombo cha mabavu badala ya kutumika kama chombo cha kulinda amani na kwamba, wakiambiwa wakamate watu wa Chadema wanawakamata bila kuuliza.

Waitara azungumza

Kwa upande wake, Mwita Waitara alisema anashangazwa na hatua ya Mbunge Bulaya kumsingizia tukio kubwa kama hilo.Aliwaambia Waandishi wa habari kuwa wakati wa tafrani hiyo yeye alikuwa amelala chumbani kwake na alishtuka usingizini kutokana na kelele alizozisikia nje.Waitara alisema pamoja na yeye kutokuwapo kwenye gari usiku huo, anashanagzwa na hatua ya polisi kumkamata na kumshikilia kwa saa kadhaa.

Chadema wataka mgombea CCM aenguliwe
Lissu alisema tayari Chadema kimemwandikia barua Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya Uchaguzi kulalamikia kitendo cha Mbunge wa Tabora mjini, Ismail Aden Rage, kutembea na bastola waziwazi hadharani.Kutokana na kitendo hicho, Chadema kimemwomba mwenyekiti wa kamati hiyo ya maadili kukiomba mgombea wa CCM, Dalaly Kafumu, aondolewe kwenye kampeni kutokana na ukiukwaji huo wa maadili.

Lissu alisema Ibara ya 2(2) ya Maadili ya Uchaguzi ya mwaka 2010 ilivyofanyiwa marekebisho Septemba 20, mwaka huu inakataza kubeba silaha yoyote inayoweza kudhuru mtu yeyote katika mikutano ya kampeni.Alilitaka Jeshi la polisi kumkamata Rage na wabunge waliofyatua risasi na kuwaweka rumande akisema kama hilo litafanyika ataamini jeshi hilo linatenda haki kwa usawa na bila upendeleo.

Polisi kumhoji Rage
Naibu Kamishina wa polisi, Mngulu alisema polisi watamhoji Mbunge wa Tabora Mjini Aden Rage kwa kitendo chake cha kutembea na bastola hadharani."Tutaanza kwa kumhoji Mheshimiwa Rage kwa nini alitembeza na bastola na uchunguzi utakapokamilika tutatuma kwa wataalamu wa sheria ili wafanye ufafanuzi kwamba katika hali ile inakuwaje," alisema.

CCM nao watoa tamko

Katibu wa NEC Fedha na Uchumi, Mwigulu Nchemba alisema jaribio la kutaka kutekwa kwa wabunge wao wawili usiku wa kuamkia jana ni mwendelezo wa matukio ya vurugu dhidi ya wana-CCM na viongozi wake.Nchemba alisema yeye na wabunge hao wamekuwa wakiwindwa kwa muda mrefu na Chadema baada ya wao kubadilisha upepo na kuwafanya vijana wabadilike na kuamua kukiunga mkono CCM.

Katibu huyo ambaye pia ni mratibu wa kampeni za CCM jimbo la Igunga amelaani tukio hilo na matukio mengine, akiwataka polisi kuwakamata wote waliotajwa kuhusika kuwashambulia wabunge hao.

Zitto Kabwe atua Igunga
Katika hatua nyingine Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe, jana aliingia katika Jimbo la Igunga kuongeza nguvu ya kampeni kwa chama chake cha Chadema na kupata mapokezi makubwa kutoka kwa wanachama na wapenzi wa chama hicho.
 
Sasa ulitaka isiripoti kinachoelezwa kutokea? Mlaumu Esther Bulaya aliyehojiwa. Mbona ripoti ya Zitto kulakiwa na maelfu huizungumizii?
 
Mfa maji haachi kutapatapa. Ccm wanahangaika hawaoni pakutokea.
 
Sasa ulitaka isiripoti kinachoelezwa kutokea? Mlaumu Esther Bulaya aliyehojiwa. Mbona ripoti ya Zitto kulakiwa na maelfu huizungumizii?

Your opinion is always predicted!!!!! Tatizo huwa unaongozwa zaidi na ideology kuliko facts. Rudia kuisoma hiyo habari objectively na u will see what I am talking about!!!!!!! By the way how come your guys wanasema wanaitambua NTC kule Libya? Inakuwaje mnakumbuka shuka kumekucha, always leading from behind ahahaha ahahaha ahahaha! sorry kwa kutoka nje ya topic! Couldn't wait anywayz nilivyoona tu jina lako......
 
Truly shocking and self contradicting, I wonder how the editor of this paper still maintain his job!!!!!!!!!

msameheni bure Kingoba Mgaya(mhariri), niliwahi kuongea naye, utashangaa ilikuaje akawa mhariri, mweupe kichwani

mtoto wa uswazi,kada wa ccm, kapigika sana anajua wakimtimua anarudi msoto, hamna professional hapo
 
e''Nilikuwa natoka Silent Inn, nikaona gari inanifuatilia kabla sijaingia njia ya kwenda Peak nilikofikia, nikapitiliza kama naenda Singida, bado wakawa wananifuata huku wakipiga gari langu kwa mawe na risasi. Nilipompigia mwenzangu Aeshi akanambia anakuja kunisaidia na amewapigia simu polisi kuomba msaada zaidi, ndipo wale watu wakakimbia porini. Aliyerusha risasi ni Waitara. Nimemwona.'' alisema Esther Bulaya

''Vijana waliokuwa na wabunge wa CCM walivamia hoteli tunayoishi viongozi wa Chadema na kutaka kuchoma moto magari mawili ya matangazo yanayotumiwa kwa kampeni. Nilikuwa ndani wakati sakata hilo linaanza, lakini baada ya kutoka nje nilikuta tafrani huku gari la Aeshi likiwa chini ya ulinzi wa vijana wa Chadema. Baada ya polisi kufika, mimi na vijana wengine wa Chadema tuliongozana nao hadi kituo cha polisi kutoa taarifa ya uvamizi. Esther alikuja kituoni huku akiwatukana polisi na kuwaambia eti mimi ndiye niliyekuwa na bastola, nao wakaamua kunishikilia kwa muda.'' alisema Mwikabe Waitara

N.B: Maelezo ya Esther yanatia shaka, kama waliokuwa wakimshambulia walikimbia baada ya kufika kwa polisi na Aeshi Hillary ilikuwaje gari la Aeshi liwe miongoni mwa mali zilizoharibiwa
 
N.B: Maelezo ya Esther yanatia shaka, kama waliokuwa wakimshambulia walikimbia baada ya kufika kwa polisi na Aeshi Hillary ilikuwaje gari la Aeshi liwe miongoni mwa mali zilizoharibiwa

Mkuu napata shida sana kuamini eti hao Bulaya na Aeshi ni wabunge, wanaonekana si watu makini hata kidogo!!!!!!!!! Halafu utetezi wao wameamua ku-compromise hata na maadili ya kiuongozi ili mradi tu waiingize CHADEMA. Nahisi hizo kampeni za Igunga sasa hivi ni kupigania kuimpress viongozi wa juu wa CCM na si sera.
 
Sasa ulitaka isiripoti kinachoelezwa kutokea? Mlaumu Esther Bulaya aliyehojiwa. Mbona ripoti ya Zitto kulakiwa na maelfu huizungumizii?

Mkubwa... hivi kweli umesoma hiyo habari???!!!.... Halafu kazi ya wanahabari si kuripoti kila kinachosemwa na kila mtu!!!! La sivyo hakuna haja ya kuwa na muhariri!!!!!...
 
Ndiyo maana mie nawachukia CCM!
Huwezim kuwa mtawala then ukawa mlalamishi kwa kuonewa, eti wanataka tuwaonee huruma! hawapati kura yangu 2015, na CCM sasa wanazidi kujienezea sifa mbaya na kila mtu sasa anona jinsi CCM ilivyochoka na kukosa mwelekeo kabisa, yaani CCM ni -0%
 
msameheni bure Kingoba Mgaya(mhariri), niliwahi kuongea naye, utashangaa ilikuaje akawa mhariri, mweupe kichwani

mtoto wa uswazi,kada wa ccm, kapigika sana anajua wakimtimua anarudi msoto, hamna professional hapo

Problem ni kwamba anatumia kodi zetu kuendekeza na kuendeleza huu upupu!!!! Yaani utashangaa magazeti mawili daily news na habari leo kutoka chumba cha habari kimoja, wanaripoti habari hiyo hiyo tofauti kabisa!!!!!!!
 
Ni kweli maelezo ya Esther yanaonekana kuwa real fabricated. tungekuwa na polisi wanaotumia uweledi wa kazi zao haswaa! uongo wake ungebainika dhahiri. hata msisitizo wake kuwa aliyekuwa anafyatua risasi alimwona ni Mwita usiku huo wa manane na ktk hali ya magari kufukuzana ni tata kidogo.
 
Ni kweli maelezo ya Esther yanaonekana kuwa real fabricated. tungekuwa na polisi wanaotumia uweledi wa kazi zao haswaa! uongo wake ungebainika dhahiri. hata msisitizo wake kuwa aliyekuwa anafyatua risasi alimwona ni Mwita usiku huo wa manane na ktk hali ya magari kufukuzana ni tata kidogo.

Wasichokifahamu hawa wanaCCM ni kwamba hizi fabrication ndiyo zinazidi kuijenga CHADEMA maana hata wanaCCM makini wanaona ni namna gani chama chao kinapoteza mwelekeo!!!!!!!
 
Kama kumbukumbu zangu nzuri, kuna mwandishi wa mara alifungiwa kipindi cha uchaguzi mdogo wa kujaza jimbo la marehemu wangwe kwa kufabricate habari, vipi haiwezekani na hawa kupelekwa baraza la habari?
 
Kama kumbukumbu zangu nzuri, kuna mwandishi wa mara alifungiwa kipindi cha uchaguzi mdogo wa kujaza jimbo la marehemu wangwe kwa kufabricate habari, vipi haiwezekani na hawa kupelekwa baraza la habari?

Ofcourse hiyo ingetokea chap chap kama mwandishi huyo angekuwa amefabricate habari ya kuinang'a CCM. What a shame?
 
Mkuu napata shida sana kuamini eti hao Bulaya na Aeshi ni wabunge, wanaonekana si watu makini hata kidogo!!!!!!!!! Halafu utetezi wao wameamua ku-compromise hata na maadili ya kiuongozi ili mradi tu waiingize CHADEMA. Nahisi hizo kampeni za Igunga sasa hivi ni kupigania kuimpress viongozi wa juu wa CCM na si sera.
Mkuu Nyambala, sio mara moja wala mara mbili nimewahi kucoment humu kuwa fani ya habari imevamiwa!. Ule muswada wa sheria mpya ya havari iliyotaka kuwapiga panga vilaza wote wasivamie fani ndio huo unapigwa danadana na pia umepata upinzani mkubwa toka kwa wanahabari wenyewe.

Kipengele kilichopigiwa sana kelele ni pamoja na kile cha kutaka mtu mwenye sifa kuitwa mwandishi wa habari lazima awe na shahada ya chuo kikuu. Wamiliki vya vyombo vya habari ndio waliowachagiza waandishi wagomee mswada huo ili wamiliki waendelee kuajiri vilaza kwa kuwalipa peanut na wao kumaximize profits. Waandishi nao kwa kuamini wamiliki wanawapenda wakaunga mkono hali inapekekea fani ya habari kukosa professionalism kabisa.

Mbona fani ya sheria wameweza?. Bila LL.B mtu huwi wakili!. Hila la every Tom, Dick and Harry kuwa journalist , haya sasa ndio matokeo na itatucost sana in days to come.

Vyombo vya habari navyo vimejigawa kwa makundi vyenye maslahi ya kisiasa, vinaripoti kwa lengo la kulinda maslahi ya vyama vyao ila kinachofanywa na Habari Leo ni kujikomba komba au kujipendekeza kupindukia, mbona Daily News linesimama na hali mmiliki ni mnoja?.

Kuhusu uadilifu wa baadhi ya waheshimiwa wabunge wetu, hili nalo linahitaji mjadala wa peke yake kwani mule mjengoni kuna vichwa kadhaa na madebe matupu kibao!. Wanaaongoza kwa udebe mtupu ni wabunge wa kuteuliwa japo lazima nikiri Mhe. Bulaya sio debe tupu saana kihivyo, ni mwanadada wa shoka, role model wake ni Mdee na naamini 2015 atatinga jimboni huko kwao Musoma!.
 
wabunge wa chupi always mawazo yao huyatoa as if hawajavaa chupi...
 
Back
Top Bottom