Habari leo ni gazeti la CCM?

Habari leo ni gazeti la CCM?

Mkuu Nyambala, sio mara moja wala mara mbili nimewahi kucoment humu kuwa fani ya habari imevamiwa!. Ule muswada wa sheria mpya ya havari iliyotaka kuwapiga panga vilaza wote wasivamie fani ndio huo unapigwa danadana na pia umepata upinzani mkubwa toka kwa wanahabari wenyewe.

Kipengele kilichopigiwa sana kelele ni pamoja na kile cha kutaka mtu mwenye sifa kuitwa mwandishi wa habari lazima awe na shahada ya chuo kikuu. Wamiliki vya vyombo vya habari ndio waliowachagiza waandishi wagomee mswada huo ili wamiliki waendelee kuajiri vilaza kwa kuwalipa peanut na wao kumaximize profits. Waandishi nao kwa kuamini wamiliki wanawapenda wakaunga mkono hali inapekekea fani ya habari kukosa professionalism kabisa.

Mbona fani ya sheria wameweza?. Bila LL.B mtu huwi wakili!. Hila la every Tom, Dick and Harry kuwa journalist , haya sasa ndio matokeo na itatucost sana in days to come.

Vyombo vya habari navyo vimejigawa kwa makundi vyenye maslahi ya kisiasa, vinaripoti kwa lengo la kulinda maslahi ya vyama vyao ila kinachofanywa na Habari Leo ni kujikomba komba au kujipendekeza kupindukia, mbona Daily News linesimama na hali mmiliki ni mnoja?.

Kuhusu uadilifu wa baadhi ya waheshimiwa wabunge wetu, hili nalo linahitaji mjadala wa peke yake kwani mule mjengoni kuna vichwa kadhaa na madebe matupu kibao!. Wanaaongoza kwa udebe mtupu ni wabunge wa kuteuliwa japo lazima nikiri Mhe. Bulaya sio debe tupu saana kihivyo, ni mwanadada wa shoka, role model wake ni Mdee na naamini 2015 atatinga jimboni huko kwao Musoma!.

Mkuu Pasco maneno mazito haya, yaani waandishi wetu kwa kweli wanatia shaka mno, habari badala ijitosheleze kwa facts inaongezewa chumvi mpaka inakuwa tena si habari maana contradictions za kumwaga....... Yaani tukio hata kama hukuwepo, hujalisikia kokote ukalisoma kwenye habari hii utajikuta unadata kwa chumvi na Vikolombwezo.

Kuhusu udebe tupu wa Bulaya kweli ni debetable lakini hasa hasa nnachokiongelea hapa mimi ni umakini. And she should be careful maana taifa zima linashuhudia haya. A smart move would be for her kuweka kwa maandishi habari nzima kuisaini na kuwapa waandishi wa habari. Probably that is late now but not no too late.
 
Back
Top Bottom