Habari hii ni ya kweli, Tafadhali soma

Nimepokea sms kwenye simu yangu ya mkononi ikiwa na ujumbe huu na nimeona ni vizuri niwashirikishe harakati hizi zinazoendeshwa na undisclosed sources.

"Nzi na nyuki hufa kwa kulazimisha kupenya kwenye kioo angavu, na ndivyo watakavyoangamia wasomi, wafanyakazi na wakulima wanaolazimisha kutimiza ndoto zao kupitia chama cha mafisadi (ccm).
Sasa tuunge mkono kwenye kampeni maalumu dhidi ya Kikwete 2010, maana aliingia kwa mbinu atatoka kwa mbinu. Mtenda utendewa, tuwasapoti wadai haki na oparesheni SANGARA, Tanzania bila Kikwete inawezekana.
Tuma ujumbe huu kwa walio choshwa na Kikwete. Hasa Walimu, NMB, TRL, Wazee wastaafu wa EAC, Wanafunzi vyuoni, Madaktari, Polisi, Maaskofu, Mapadri, Makadhi, Mashehe, Wavuvi, Waumini wa dini zote na Wakurugenzi wa vyombo vya habari."

Nasisitiza kwamba huu ujumbe nimeupokea kwenye simu yangu na sijui ni nani kanitumia.

MF

I don't think whether this is a constructive strategy!!i've been working with nmb for more than 4 years, na sikuwahi hata mara moja kusikia watu wakimlalamikia Kikwete!!!! Walimu?! walimu gani? hawahawa ambao hata ukiwasikiliza wanapishana maoni kwenye masuala yao wenyewe au kuna wengine?! Labda TRL, lakini nahofia kama sehemu iliyo na lundo la wazee namna ile wanaweza kuwa tayari kwa mabadiliko kupita njia ya simu!!! Labda Maaskofu na mapadri, kwavile tutake tusitake, udini Tanzani upo, hususani ule wa chinichini!!! eti wakurugenzi wa vyombo vya habari!!!? lol! vyombo vipi? hivi vya TZ au vingine!!!? Mengi anayejitia kupiga vita ufisadi, magazeti yake yote nayo yanajitia kupiga vita ufisadi!!! Rostam Azizi anayeonekana papa la ufisadi, vyombo vyake vyote vina msimamo tofauti na ule wa vya IPP!! umenipata hapo mkuu?! Vyombo vya habari vyetu vinaegemea kule walikoegemea wamiliki wake!!!
 
Kama kawaida, wamekurupuka nakuuwahisha... subira kidogo hadi mwezi wa 8 au 9 mwakani na dhamira ingelileta maana!!

tehetehe, mwezi wa 8 mwakani? na hao chadema watakuwa na hali gani? maana hata sasa si kunafuka moshi huko?.
 
Tatizo ni kwamba huu ujumbe hautawafikia wale wanao piga kura ni dhahili wapo vijijini.
 
Tutawasaidiaje Chadema na operation SANGARA wakati juzi juzi wameshindwa kusimamisha wagombeaji katika uchaguzi wa serikali za mitaa huko Tegeta? Wengi tulijiandikisha kupiga kura lakini tukaambiwa hakuna haja maana CCM kapita bila kupingwa! Hata Mungu anasaidia wale wanaojisaidia kwanza
 

.....Madaktari, Polisi....

Tusimsingizie JK, simsapoti, lakini matatizo yetu hayakuanza naye.
 
Huo ujumbe ni murua kwa wakati huu ambao Jk amepwaya na CCM inanuka mipasho na ufisadi. Sambaza kwa wengine pia.
 
Angalia lugha iliyotumika mbona haina tija jamani ? halafu mbona watu wanajificha ? njoo mbele sema jina la kikundi chako pambana kwa njia ya kura uchaguliwe sio kwa njia laghai huu ni uchonganishi

Shy,

What are you talking about here? Wewe hujifichi? Hilo ndilo jina lako halisi? Hiyo ni njia sahihi kufikisha ujumbe katika jamii ambayo watu wanaishi kwa hofu ya kufuatiliwa na UWT n.k.

Tiba
 
Hizingonjera si za leo Shy, tumezisikia siku nyingi sana hadi masikio yanawasha. Tunataka mabadiliko ya kweli na haya yataletwa na wapiga kura. Full stop.
Hizi ngonjera za hao hao wezi wetu hatuzihitaji tena wala hazitusaidii tena. Tunataka kuepusha Tanzania na janga la kitaifa.

Mkuu Mchukia Fisadi,

Kutegemea kuwaondoa hawa jamaa zetu wanaofanya viiini macho badala ya kuongoza nchi kwenda katika neema kwa njia ya kupiga kura na katika mazingira yaliyopo ambayo tume ya uchaguzi inaundwa na makada wa CCM ni ndoto za mchana.

Tukitaka kweli kuwaondoa CCM madarakani kwa njia ya kura, basi tuhakikishe katiba imebadilishwa kutoka nchi kuwa ya chama kimoja kuwa ya vyama vingi na tume ya uchaguzi iundwe na independent people or otherwise iwe na wajumbe kutoka vyama vya upinzani na makundi huru ya jamii. Kama uamini ninayo yasema, kaulize yaliyotokea Busanda na Biharamulo hivi karibuni.

Tiba
 
"Nzi na nyuki hufa kwa kulazimisha kupenya kwenye kioo angavu, na ndivyo watakavyoangamia wasomi, wafanyakazi na wakulima wanaolazimisha kutimiza ndoto zao kupitia chama cha mafisadi (ccm).
Sasa tuunge mkono kwenye kampeni maalumu dhidi ya Kikwete 2010, maana aliingia kwa mbinu atatoka kwa mbinu. Mtenda utendewa, tuwasapoti wadai haki na oparesheni SANGARA, Tanzania bila Kikwete inawezekana.
Tuma ujumbe huu kwa walio choshwa na Kikwete. Hasa Walimu, NMB, TRL, Wazee wastaafu wa EAC, Wanafunzi vyuoni, Madaktari, Polisi, Maaskofu, Mapadri, Makadhi, Mashehe, Wavuvi, Waumini wa dini zote na Wakurugenzi wa vyombo vya habari."
Takataka tupu!
Venlan%20kuvat%20273.JPG

 
Back
Top Bottom