Said Cosmetics
JF-Expert Member
- Sep 4, 2017
- 2,007
- 1,600
BAADA ya miaka minne ya kuajiriwa bila hata kuongezwa mshahara au hata marupurupu, *Bwana Juma Hassani* aliamua kwenda kwa bosi wake kulalamika. Jibu alilolipata kwa bosi wake ni kwamba, hakupewa nyongeza wala marupurupu kwa sababu *HAKUSTAHILI*
Akauliza kwa nini?
Akaambiwa katika miaka minne uliyofanya hapa, hujafikisha hata mwaka mmoja. Akasimama na kuanza kufoka, akaambiwa kaa chini, na majibizano yakawa hivi;
*Bosi:* Mwaka una siku ngapi?
*Juma:* 365 au 366.
*Bosi:* Huwa unakuja kazini wikiendi?
*Juma:* Hapana
*Bosi:* Hebu piga hesabu mwaka una jumamosi na jumapili ngapi kisha zitoe katika 366.
*Juma:* Jumamosi 52 na Jumapili 52 jumla unapata siku 104. Ukitoa katika siku 366 unabaki na siku 262.
*Bosi:* Siku ina masaa 24, wewe umafanya kazi masaa mangapi?
*Juma:* Masaa nane kwa siku
*Bosi:* Sasa nipigie hesabu masaa nane katika masaa 24. Nane kwa 24 inaingia mara ngapi?
*Juma:* Inaingia mara tatu mkuu
*Bosi:* Sasa ukizigawa zile siku 262 kwa masaa uliyofanya kazi yaani uigawe kwa tatu kulingana na masaa uliyofanya kazi unapata siku ngapi zilizokamilika?
*Juma:* 87
*Bosi;* Kwa mujibu wa saa ulizofanya kazi kwangu, ni sawa na siku 87, tuendelee na mahesabu?
*Juma:* Tuendelee.
*Bosi:* Unakumbuka uliumwa wiki mbili nikakupa likizo? Na ulishachukua likizo yako ya kawaida siku 28 na ukaenda msibani wiki moja hebu piga hesabu vizuri.
*Juma:* 14 + 28 + 7 = 49.
*Bosi;* Toa katika siku 87
*Juma:* 42
*Bosi;* Toa sikukuu za Idd, Maulid, Uhuru, Mapinduzi, Pasaka, Krismas, Nyerere Day, Mwaka mpya, Mei Mosi, Sabasaba, Nanenane na ile wiki iliyonyesha mvua kuuubwa nikawaruhusu mpumzike.
*Juma:* Bosi naomba nikaendelee na kazi.
*Bosi:* Malalamiko vipi?
*Juma:* *HAPA KAZI TU*.
[emoji1][emoji1]