Gwajima: Sina ugomvi na Jeshi la Polisi wala Serikali

Gwajima: Sina ugomvi na Jeshi la Polisi wala Serikali

Fandre

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2013
Posts
320
Reaction score
225
Askofu Gwajima ametumia muda wa ibada leo hii katika kanisa la Ufufuo na Uzima-Kawe kuweka wazi baadhi ya mambo ya msingi yaliyozua maswali katika jamii, Askofu Mkuu wa kanisa la Ufufuo na Uzima duniani ameweka bayana ya kuwa yeye binafsi pamoja na Kanisa lake hawana ugomvi wala mgogoro na Jeshi la Polisi nchini.

Katika kuthibitisha ukweli huo, Askofu Gwajima amesema ya kuwa yeye binafsi pamoja na Kanisa lake walijitolea kudhamini mafunzo ya Polisi Jamii kwa muda wa miezi Mitatu. Katika kuelezea ukweli wa jambo hilo, Kamanda Sillo wa Jeshi la Polisi ndiye aliyezindua na kuyafunga mafunzo hayo yaliyodumu kwa muda tajwa hapo juu.

Katika hatua nyingine Askofu Gwajima amesema ya kuwa, tayari alikwisha waandikia barua Jeshi la Polisi ili kutoa elimu ya kijamii kuhusiana na masuala ya mauaji ya Albino ambayo kimsingi yamekithiri sana nchini. Na Jeshi la Polisi lilikwisha jibu barua hiyo kupitia Kamishina wake wa Mafunzo na Elimu kwa Jamii kuwa amepata ruhusa ya kutoa mfunzo hayo na kuwagaharamia Polisi wote watakao kuwa pamoja naye katika kutoa elimu hiyo ya kijamii kuhusiana na kadhia hii ya mauaji ya albino nchini.

Lakini zaidi, Askofu Gwajima ameweka bayana ya kuwa hakuna mtu atakayeweza kumchagulia rafiki kwani marafiki alionao ambao ni Dr. Slaa (KATIBU MKUU WA CHADEMA) alkdhalika Mh. Edward Lowasa (Mbunge) ametoka nao mbali na wameishi kwa pamoja kwa muda mrefu kwahiyo mtu yeyote yule anayeona yeye kuwa na watu hao ni kosa au inamuumiza kwa njia moja au nyingine basi asahau kuharibu urafiki wao uliojengwa kwa muda mrefu.

Kwa upande mwingine ameweka wazi ya kuwa alikataa kutibiwa katika hopsitali ya Jeshi la Polisi kule Kurasini kwa sababu matatizo aliyoyapata hata kuzimia aliyapata akiwa polisi kwahiyo hakuona umuhimu wa kuendelea kuwa chii ya hospitali ya Jeshi la Polisi ambalo hali aliyonayo sasa aliipata akiwa mikononi mwa Jeshi la Polisi ndipo alipoomba kupelekwa kwenye hospitali nyingine mbali na hapo..

Katika kuonyesha kuwa jambo hili lilikuwa wazi kabisa kwa kila mwenye akili kuhoji ni pale alipoweka bayana ya kuwa alipokuwa Polisi aliwauliza kosa alililoitiwa ndipo wakamwambia ni kwa sababu amemtukana Pengo, lakini katika mahojiano hakukuwa na swali hata moja lililohusiana na suala la Pengo wala maneno yake kwa Pengo.

Kitu kingine kilichozua maswali kwake ni pale ambapo Polisi walinuia kwenda kukagua na kupekua nyumbani kwake na kuuliza, Je..."NI MANENO TU ALIYOMWAMBIA KARDINALI PENGO AU KUNA JAMBO JINGINE LA ZIADA NYUMA YAKE?"

Katika kuonyesha ya kuwa amekua kiongozi mwenye USHIRIKIANO MZURI NA SERIKALI AMEWEKA BAYANA YA KUWA YEYE PEKE YAKE HAPA NCHINI AMEKUA KIONGOZI ANAYEKEMEA MAOVU KWA UJASIRI HADHARANI PASIPO KUFICHA AKITOLEA MFANO WA TUKIO LA KIGAIDI LILILOTOKEA MKOANI TANGA AMBALO NI YEYE PEKE YAKE KWA UJASIRI ALILIKEMEA MBELE YA MADHABAHU YA KANISA LAKE NA KULIOMBE TAIFA.

Lakini pia Askofu Gwajima ameweka wazi ya kuwa hataacha kuwakemea watu wote watakafanya makosa katika jamii pasipo kuogopa wala kuficha jambo lolote. Kadharika amekazia ya kuwa Askofu yeyote atakayekwenda kinyume na maamuzi ya pamoja ya maaskofu wote pamoja na baraza la maaskofu hataacha kumkemea kwani nia ya maaskofu wote ni kuhakikisha amani ya nchi hii inadumu daima na hivyo yeyote atakayesababisha au kwenda kinyume na jambo hili ni lazima atamkemea hadharani bila hofu.
 
Daaaaa.....aisee mch.gwajima Mungu akubariki sn kwa namna hyo...wananchi pia tupo macho tunalifuatilia sakata lako kwa karibu sana.....mtumishi sawasawa.........mtumishi
 
aiseee wangemuua tu kumbe bado ajaacha jeuri na kidomo domo alafu mbona hakusema nini kilimfanya akazima?!

#Zitto
 
Yaani ww kweli huna maana unafurahia mwenzio kufaAchilia mbali mambo yote lkn huwezi kumtamania mwenzio kifo kaka@mzaramo
 
Alafu kuwapata watu majasiri kama Gwajima kwa sasa ngumu....mjombaaaa..jamaa yule anakuchana live haogopi....na yy mwenyewe nasikia amesema hafi leo wala kesho....kwikwikwikwi.......
 
mtu anazimia halafu anachagua hospitali ya kwenda?
Mjomba nnasikia alizinduka akiwa hosp ya polisi alafu wanataka kumuwekea drip aliposhituka akakataa ndio wachungaji wake wasaidiz ndio wakampeleka TMJ...
 
kumbe alikua anaigiza ili apate umaarufu ili ajiongezee kondoo watiifu..unazimiaje then unachagua hospital na kuagiza bastola yako kwa ajili ya kujilinda ukiwa kitandani...tafakari chukua hatua...
 
nipp hapa kanisani kwa gwajima baada ya kuongea yote ya moyoni mwake naona maspika yamepunguzwa suti kabisa
 
Kama atashikilia msimamo wake wa kuwaumbua watu WANAFIKI kama pengo atakuwa ananifurahisha sana maana viongozi wengi wanapenda sana kusifiwa sifiwa tu
 
hakika huyo ni mwana wa aliyefufuka leo. barikiwa sana mchungaji gwajima na hata wakikuua kanisa la Tanzania halitakusahu milele na shawabu ya kazi yako nzuri hapa duniani utaikua mbinguni.
 
Kama atashikilia msimamo wake wa kuwaumbua watu WANAFIKI kama pengo atakuwa ananifurahisha sana maana viongozi wengi wanapenda sana kusifiwa sifiwa tu

leo naona gwajima kawa na busara hakukuwa na matusi zaidi ya ngonjeraa
 
Viongozi wa madhehebu michepuo pamoja na wana Sihasa lao moja tu, wote wapigaji.
 
aiseee wangemuua tu kumbe bado ajaacha jeuri na kidomo domo alafu mbona hakusema nini kilimfanya akazima?!

[URL=https://www.jamiiforums.com/usertag.php?do

Mzaramo hakika akili yako inaonyesha ni div 5 😳😁
 
kumbe alikua anaigiza ili apate umaarufu ili ajiongezee kondoo watiifu..unazimiaje then unachagua hospital na kuagiza bastola yako kwa ajili ya kujilinda ukiwa kitandani...tafakari chukua hatua...


Mbona una hoja ya dhaifu aisee?:shocked:
Gwajima hakuwa peke yake Polisi na hakuwa peke yake alipokuwa Polisi wala alipokua akipelekwa katika hospitali ya Jeshi la Polisi na kama shida au tatizo lilimpata akiwa Polisi yawezekanaje tena akatibiwe katika hospitali ya polisi? yani ni suala dogo kuelewa kuwa kesi ya nyani umpelekee ngedere!

Alikua sahihi kabisa kwa sababu hakujua kilichomfanya azimie
 
kumbe ni mgonjwa !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! aaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
hapo nimekuelewa mchungajii..hoja nyengine hujajibu;kama alikuwa kazuunguukwa na wachungaji bastola ambayo alikiri kuiagiza ilikuwa ya nini...majibu yako yatanisaidia ama kujenga hoja au kufya mkia
 
Nadhani itakua vyema polisi wakaenda kupekua nyumbani kwa Gwajima huenda wakapata kitu kinachoweza kumsafisha au kumtia hatiani.

Mana watumishi.wengine tunasikia wakisadikiwa kuwa wanafuga mpaka majoka ndani huku wakijifanya kumtumikia Mungu.
Ningependa apekuliwe ili aonekane ni msafi kabisa.
 
kumbe alikua anaigiza ili apate umaarufu ili ajiongezee kondoo watiifu..unazimiaje then unachagua hospital na kuagiza bastola yako kwa ajili ya kujilinda ukiwa kitandani...tafakari chukua hatua...


Mbona una hoja ya dhaifu aisee?:shocked:
Gwajima hakuwa peke yake Polisi na hakuwa peke yake alipokuwa Polisi wala alipokua akipelekwa katika hospitali ya Jeshi la Polisi na kama shida au tatizo lilimpata akiwa Polisi yawezekanaje tena akatibiwe katika hospitali ya polisi? yani ni suala dogo kuelewa kuwa kesi ya nyani umpelekee ngedere!

Alikua sahihi kabisa kwa sababu hakujua kilichomfanya azimie sasa ataendeleaje kutibiwa na wale ambao amezimia akiwa chini yao?
 
Back
Top Bottom