Gwajima: Sina ugomvi na Jeshi la Polisi wala Serikali

Gwajima: Sina ugomvi na Jeshi la Polisi wala Serikali

mbona kwa uelewa wangu hyo story kma inamsafisha hivi gwajima...wht z da fact?? maviongozii ya dini mnatuchanganya tuuu
 
hongera sana baba askofu gwajima kwa afya yako kendelea kuimarika
 
kumbe alikua anaigiza ili apate umaarufu ili ajiongezee kondoo watiifu..unazimiaje then unachagua hospital na kuagiza bastola yako kwa ajili ya kujilinda ukiwa kitandani...tafakari chukua hatua...
Mkuu umewaza vzr lkn au umenena tu
 
Askofu Gwajima ametumia muda wa ibada leo hii katika kanisa la Ufufuo na Uzima-Kawe kuweka wazi baadhi ya mambo ya msingi yaliyozua maswali katika jamii, Askofu Mkuu wa kanisa la Ufufuo na Uzima duniani ameweka bayana ya kuwa yeye binafsi pamoja na Kanisa lake hawana ugomvi wala mgogoro na Jeshi la Polisi nchini.

Katika kuthibitisha ukweli huo, Askofu Gwajima amesema ya kuwa yeye binafsi pamoja na Kanisa lake walijitolea kudhamini mafunzo ya Polisi Jamii kwa muda wa miezi Mitatu. Katika kuelezea ukweli wa jambo hilo, Kamanda Sillo wa Jeshi la Polisi ndiye aliyezindua na kuyafunga mafunzo hayo yaliyodumu kwa muda tajwa hapo juu.

Katika hatua nyingine Askofu Gwajima amesema ya kuwa, tayari alikwisha waandikia barua Jeshi la Polisi ili kutoa elimu ya kijamii kuhusiana na masuala ya mauaji ya Albino ambayo kimsingi yamekithiri sana nchini. Na Jeshi la Polisi lilikwisha jibu barua hiyo kupitia Kamishina wake wa Mafunzo na Elimu kwa Jamii kuwa amepata ruhusa ya kutoa mfunzo hayo na kuwagaharamia Polisi wote watakao kuwa pamoja naye katika kutoa elimu hiyo ya kijamii kuhusiana na kadhia hii ya mauaji ya albino nchini.

Lakini zaidi, Askofu Gwajima ameweka bayana ya kuwa hakuna mtu atakayeweza kumchagulia rafiki kwani marafiki alionao ambao ni Dr. Slaa (KATIBU MKUU WA CHADEMA) alkdhalika Mh. Edward Lowasa (Mbunge) ametoka nao mbali na wameishi kwa pamoja kwa muda mrefu kwahiyo mtu yeyote yule anayeona yeye kuwa na watu hao ni kosa au inamuumiza kwa njia moja au nyingine basi asahau kuharibu urafiki wao uliojengwa kwa muda mrefu.

Kwa upande mwingine ameweka wazi ya kuwa alikataa kutibiwa katika hopsitali ya Jeshi la Polisi kule Kurasini kwa sababu matatizo aliyoyapata hata kuzimia aliyapata akiwa polisi kwahiyo hakuona umuhimu wa kuendelea kuwa chii ya hospitali ya Jeshi la Polisi ambalo hali aliyonayo sasa aliipata akiwa mikononi mwa Jeshi la Polisi ndipo alipoomba kupelekwa kwenye hospitali nyingine mbali na hapo..

Katika kuonyesha kuwa jambo hili lilikuwa wazi kabisa kwa kila mwenye akili kuhoji ni pale alipoweka bayana ya kuwa alipokuwa Polisi aliwauliza kosa alililoitiwa ndipo wakamwambia ni kwa sababu amemtukana Pengo, lakini katika mahojiano hakukuwa na swali hata moja lililohusiana na suala la Pengo wala maneno yake kwa Pengo.

Kitu kingine kilichozua maswali kwake ni pale ambapo Polisi walinuia kwenda kukagua na kupekua nyumbani kwake na kuuliza, Je..."NI MANENO TU ALIYOMWAMBIA KARDINALI PENGO AU KUNA JAMBO JINGINE LA ZIADA NYUMA YAKE?"

Katika kuonyesha ya kuwa amekua kiongozi mwenye USHIRIKIANO MZURI NA SERIKALI AMEWEKA BAYANA YA KUWA YEYE PEKE YAKE HAPA NCHINI AMEKUA KIONGOZI ANAYEKEMEA MAOVU KWA UJASIRI HADHARANI PASIPO KUFICHA AKITOLEA MFANO WA TUKIO LA KIGAIDI LILILOTOKEA MKOANI TANGA AMBALO NI YEYE PEKE YAKE KWA UJASIRI ALILIKEMEA MBELE YA MADHABAHU YA KANISA LAKE NA KULIOMBE TAIFA.

Lakini pia Askofu Gwajima ameweka wazi ya kuwa hataacha kuwakemea watu wote watakafanya makosa katika jamii pasipo kuogopa wala kuficha jambo lolote. Kadharika amekazia ya kuwa Askofu yeyote atakayekwenda kinyume na maamuzi ya pamoja ya maaskofu wote pamoja na baraza la maaskofu hataacha kumkemea kwani nia ya maaskofu wote ni kuhakikisha amani ya nchi hii inadumu daima na hivyo yeyote atakayesababisha au kwenda kinyume na jambo hili ni lazima atamkemea hadharani bila hofu.
Cha msingi asirudie tena kulaani watumishi wa Mungu,atarudi tena ICU
 
hakika askofu kasema kweli yake na serikali wamwache ahubili injili.
 
Gwajima ni miongono mwa watumishi wa Mungu wachache sana katika nchi hii wenye ujasiri wa kutoa matamko! Wengine walishawekwa mifukoni!
 
hii muvi hata siielewi, ngoja nikae kimya tu
 
Kama atashikilia msimamo wake wa kuwaumbua watu WANAFIKI kama pengo atakuwa ananifurahisha sana maana viongozi wengi wanapenda sana kusifiwa sifiwa tu
Pengo hana muda wa kupoteza na watu wa aina ya Gwajima, ndio maana hajamshtaki na hata yeye Gwajima anakiri kuwa hakuulizwa swali lolote kuhusu Pengo. Cha ajabu Gwajima anaendelea na msimamo wa kumchukia Pengo wakati wanaomuhoji hadi sasa ni polisi, tena kuhusu mambo mengine kabisa kuhusu mali zake zenye utata
 
Back
Top Bottom