Gwajima ni 'Threat to National Security', Mamlaka husika zimdhibiti

Hv mtu unashahidi gan kuwa fulan n freemasonry au.mchawi? Je una vdeo akiwa anabudu ndan ya jengo? Kama unazo vdeo za masonic temple yeye akiwa ana budu bac ww n kiongoz wao maana hakuna anayeingia mule ambaye sio muhusika...pili uksema tu kwa manenp fulan n mchawi au masonic haitosh maana ww sio mungu..gwajima anajitia yeye mungu mtu lakin atakuja kuwa na mwisho mbaya zaidi ya kakobe
Tulia wewe, haumuoni diamond mwenyewe kimya, ukweli hauchanganyiki na giza
 
Kuna watu nawaheshimu sana humu JF kutokana ndio walikuwa think tankers wa JF ikiwemo hii ID ya Waberoya lakini kwa sasa nimeshtuka,

Defenetely hii ID ni taasisi haikuwa individual ID, na for sure ID hii ilikuwa na mahusiano ya moja kwa moja na Ayatollah kama ilivyokuwaga ile ID maarufu hapa JF ya TUNTEMEKE nayo ilikuwa ni taasisi.

Wasiwasi genuine user wa ID ya Waberoya na currently user ni vitu viwili tofauti, hii ni deeply vetting ninayokupa ingia kwenye profile chunguza previous thread and post utagunduwa currently ID user ni mweupe kichwani ID imempwaja.

Defenetly sasa bila shaka na kwa uhakika kabisa nakuthibitishia hii ID ilikuwa ni taasisi na Ayatollah ameitumia sana kabla ya kuiabandon.
Matoka
Hata mimi niliina hii change nikashindwa kuelewa ni njaa, frustrations, au nini. Asante kwa kunipa mwanga.
 
Huyu mwehu akiachwa kuna jambo baya sana anakwenda kufanya, kashaaona kuwa anaweza kufanya chochote na asiguswe ila natoa Rai huu ni muda wa kumuonyesha kua Serikali ipo, haiwezekani kutumia kichaka cha kanisa kutukana kila anaekugusa na sasa anaweza kufanya lolote akijua hawez kuguswa
Ila kama una kumbukumbu njema walioanza shida ni wawakilishi wa serikali sasa sijui nani alipaswa kudhibitiwa Gwaji au Bashi?
 
Yaan diamond kusemwa taifa litapoteza aman dah unatafuta kiki.mbona umefanya kumsema vp unataka kupoteza aman think big kabla hamjaleta mada ni nan diamond asemwe aman ya nchi ipotee shame of u
 
Martin Luther King Jr hakuwa mwanasiasa bali Mchungaji na alileta mabadiliko ya kihistoria Marekani. Yeye pia alionekana National Security Threat kwa serikali ya kibaguzi ya wakati huo leo ni shujaa mpaka ana siku yake maalum.
 
Kuhusu Diamond naona Gwajima anatwanga maji kwenye kinu kwa sababu hakuna hata kimoja atakachosema ambacho watu hawajasema:
  • Kwamba Diamond ni Freemason watu washasema sana siku za nyuma....
  • Kwamba Diamond anauza unga watu washasem sana siku za nyuma....
  • Kwamba Diamond amebambikiwa watoto; watu washasema sana siku za nyuma.....
  • Kwamba Zari yupo kwa Diamond kwa mkakati maalumu wa kumchuna pesa; watu washasema sana siku za nyuma....
  • Kwamba Tiffa ni mtoto wa Katunzi; watu washasema sana siku za nyuma
  • Kwamba kale kidume cha sasa ni mtoto wa Ivan; watu washasema siku za nyuma.....
  • Kwamba Diamond ana radhi za babake; watu washasema sana siku za nyuma....
Itoshe tu kusema kwamba safari hii Gwaajima hakuchanga karata zake sawa sawa!! Manake hata akisema Diamond alipata ZERO bado wala haiwezi kuwa story!! Inawezekana kushinda kwake madhabahuni alidhani kuna scandal ambayo inaweza kumtetemesha Diamond bila kufahamu kwamba yoooooooooooooooote yameshasemwa huko nyuma!!!

Hili la Halima Mdee binafsi ndo nikachoka kabisa!!! But trust me; Gwajima amepigwa mkwara afunge bakuli lake na ndio maana siku hizi humsikii akizungumzia suala la Makonda!! Lakini kwavile ameonja tamu ya publicity ya Instagram kupitia Daudi Bashite; anachofanya hivi sasa ni kutafuta attention kwa njia yoyote ile!!!
Watu walisema diamond ni freemason ila zilikuwa ni tetesi sasa gwajima amesema kama dogo ataendelea na ujinga wake yeye atathibitisha zile tuhuma za kuwa ni freemason...UPO?
 
Martin Luther King Jr hakuwa mwanasiasa bali Mchungaji na alileta mabadiliko ya kihistoria Marekani. Yeye pia alionekana National Security Threat kwa serikali ya kibaguzi ya wakati huo leo ni shujaa mpaka ana siku yake maalum.

Ha haaa unamfananiza G na Martin Luther King!
Hapo ni north na south.
 
Nimekuwa nikifuatilia kwa muda mrefu majibishano na mipasho ambayo anayejiita Askofu Gwajima na watu mbalimbali wanaotofautiana nae,a.k.a bifu, amekuwa akitumia mtaji wa forum ya waumini wake kuwaattack wagomvi wake non stop, ambapo hao victims bahati mbaya hawana forum ya kufight back, matokeo yake anawasababishia picha mbaya kwa jamii na hata msongo wa mawazo kwa hawa victims.

Kwa sasa Askofu huyu anajitambulisha kama ndiye mkemea maovu kwenye Nchi, matokeo yake akiachiwa aendelee hivi ataleta uvunjifu wa amani Nchini.

Ameishajua watanzania walio wengi wanapenda umbea so anawalisha kile wanachotaka kusikia achilia mbali kuwafanya watanzania hawa kama daraja la kupiga hela ,maake anajaza watu wengi kila jumapili hivyo makusanyo ya sadaka yamedouble kama siyo kutriple.

Anyway hayo ya brainwashing na kupiga hela siyo ishu kwani hao waumini wake ni watu wazima, wenye akili timamu. tatizo ninaloliona ni hii tabia ya personal attack kwa watu anaotofautiana nao, hii itahatarisha amani tuliyonayo na usalama wa Taifa kwa ujumla.

Anaposema Diamond ni member wa Freemanson, inamsaidia nini mtu akishafahamu hiyo imani ya Diamond, hii haimpi mtu ticketi ya kwenda mbinguni eti tu kwa vile umeishafahamu Diamond ni Freemanson, ticketi ya kwenda mbinguni ni kufanya yale yanayompendeza na aliyoagiza Mwenyezi Mungu kwa wanadamu, pia kwa kujua Diamond ni Freemanson haikupi wewe Kinga against matendo ya Shetani.

Mamlaka husika zimdhibiti huyu anayejiita Askofu aliyegeuka Mr Mipasho wakati waumini wake wana kiu ya neno la Mungu,wiki nzima mtu umekuwa bize na mihangaiko ya maisha, Jumapili inafka unasema uende ukamuabudu muumba wako instead unakutana na mipasho mwanzo mwisho over 5 hours, this is not fair to these poor followers.
Mbona husemi kuhusu yeye kuchafuliwa na ishu ya madawa ya kulevya na huyo mungu wa DSM , na kuhusu diamond una uhakika gan kuwa sio Freemason tupe ushahid maana gwajima kasema anao afu kumbuka diamond ndiyo kamchokoza gwajima kwenye wimbo wake kwahiyo acha wapuuze wasemwee tu

Na ndiyo maana hata ishu ya halima mdee kamchana live ujinga wa kutukana ovyo bungeni

Binafsi Nina imani sana na vyombo vyetu vya usalama wapo makin kuliko unavyonia wewe . wacha waendelee kufanya kazi yao na mungu azidi kuwalinda hawa watu muhimu sana japo kuna wapuuz wachache mnajifanya kuwadharau
 
Hivi Tanzania hatuna National Security Council, Matukio ya kiusalama Raisi anayopokea kutokea Kwa DG wa TISS na Minister of Home affairs, It's our time to establish National Security Council which will discuss na Report Direct to Our president Issues concern Security, TISS is Too Politics now and it's not independent Agency anymore
Bonge la point umeongea
 
Watu walisema diamond ni freemason ila zilikuwa ni tetesi sasa gwajima amesema kama dogo ataendelea na ujinga wake yeye atathibitisha zile tuhuma za kuwa ni freemason...UPO?
Ukisikia maajabu ndo haya sasa! Eti atathibitisha... Narudia tena na tena... hakuna cha maana atakachoongea ambacho hakijasemwa! Ikiwa ameshindwa kuthibitisha jambo dogo tu la Division Zero ya Bashite ambalo vyeti huwa vinapatikana bila kificho ndo ataweza kuthibitisha suala la Freemason ambao wanaendesha mambo yao kwa usiri?! Ingawaje na mimi nimemkomalia Bashite lakini nitakuwa mtu wa ajabu kama nitaamini the so called cheti ambacho alikionesha Gwajima!!!

Btw, hata kwenye suala la Bashite; si alikuwa anasema anampa nafasi JPM kumchukulia hatua Bashite! Hadi sasa JPM kakaza; huyo Gwajima amefanya nini?! Au ndo kutoa kile "cheti?"
 
kila mtu akitumia jukwaa lake na kila pastor na misikiti ifanye hivyo nchi itakalika kweli? akina msambichaka ninaowafahamu ni wasomi na maprofesa, wewe utakuwa adopted au mtoto wa nje..kamuulize mama yako vizuri
Soma ili uelewe content.

Kama ni halali kwa wengine kutumia majukwaa yao kwa nini iwe haramu kwa mwingine? Kama hatukuwalaani wengine wanaotumia majukwaa yao vibaya, kuna uhalali gani kuwalaumu wengine? Mbona mzee wa Upako anatumia jukwaa lake hatulalamiki? Tuache unafiki wa kujifanya wenye hekima kwa vile tumesemwa vibaya badala ya kusifiwa. Kama unafurahia kusifiwa madhabahuni, ukubali pia kulaaniwa madhabahuni.

Mengine uliyoyaeleza, sina haja ya kuyajibu, maana akili ya mtu hutambuliwa na kitokacho kwenye kinywa chake.
 
Mamlaka husika zimdhibiti huyu anayejiita Askofu aliyegeuka Mr Mipasho wakati waumini wake wana kiu ya neno la Mungu,wiki nzima mtu umekuwa bize na mihangaiko ya maisha, Jumapili inafka unasema uende ukamuabudu muumba wako instead unakutana na mipasho mwanzo mwisho over 5 hours, this is not fair to these poor followers.

Umeniwahi vizuri sana; miye hofu yangu ni kuwa huyu jamaa ni kama anaweza kuwashika watu sehemu zisizostahili na akawafanya wamuombe msamaha mapema tu... Ni zaidi ya tishio kwa usalama wa taifa bali ni tishio kwa usalama wa maisha ya watu wengi. Anaanza kukusanya nguvu ambazo hapaswi kuwa nazo.. na watu wanamkubalia. Ni kama watu wanaomuhofia yule dada mwingine... kiasi kwamba wakisikia ana details zako inabidi uombe radhi mapema.
 
Gwajima hakuacha ile stori!! Kwavile watu walikuwa wanamjaza; akajaa kwa kile anachoamini anaaogopwa kwa kibri kwamba "atakayemchokoza" lazima akione cha mtema kuni!!!

Lakini kama nilivyosema hakuna cha maana ambacho Gwajima angesema ambacho hakijasemwa huko nyuma!! Alichofanya ni kusema kwamba Diamond ni Freemason... stori ambazo zimeshakuwa obsolete hivi sasa!!! Watu wakamshukia sawa sawa hadi akaunti yake akaikimbizia private!!!
Punguza mahaba yako kwa huyo mpuuzi Nassib, unajichoresha tu na kujidharaulisha.
 
Umeniwahi vizuri sana; miye hofu yangu ni kuwa huyu jamaa ni kama anaweza kuwashika watu sehemu zisizostahili na akawafanya wamuombe msamaha mapema tu... Ni zaidi ya tishio kwa usalama wa taifa bali ni tishio kwa usalama wa maisha ya watu wengi. Anaanza kukusanya nguvu ambazo hapaswi kuwa nazo.. na watu wanamkubalia. Ni kama watu wanaomuhofia yule dada mwingine... kiasi kwamba wakisikia ana details zako inabidi uombe radhi mapema.
Ukitaka kumjuwa vizuri Gwajima muuliza swahiba wako Dr Mihogo a.k.a Slaa. Atakueleza vizuri kuhusu hiyo mashine.
 
Back
Top Bottom