Gwajima ni 'Threat to National Security', Mamlaka husika zimdhibiti

Jack Beur

JF-Expert Member
Feb 26, 2010
222
246
Nimekuwa nikifuatilia kwa muda mrefu majibishano na mipasho ambayo anayejiita Askofu Gwajima na watu mbalimbali wanaotofautiana nae,a.k.a bifu, amekuwa akitumia mtaji wa forum ya waumini wake kuwaattack wagomvi wake non stop, ambapo hao victims bahati mbaya hawana forum ya kufight back, matokeo yake anawasababishia picha mbaya kwa jamii na hata msongo wa mawazo kwa hawa victims.

Kwa sasa Askofu huyu anajitambulisha kama ndiye mkemea maovu kwenye Nchi, matokeo yake akiachiwa aendelee hivi ataleta uvunjifu wa amani Nchini.

Ameishajua watanzania walio wengi wanapenda umbea so anawalisha kile wanachotaka kusikia achilia mbali kuwafanya watanzania hawa kama daraja la kupiga hela ,maake anajaza watu wengi kila jumapili hivyo makusanyo ya sadaka yamedouble kama siyo kutriple.

Anyway hayo ya brainwashing na kupiga hela siyo ishu kwani hao waumini wake ni watu wazima, wenye akili timamu. tatizo ninaloliona ni hii tabia ya personal attack kwa watu anaotofautiana nao, hii itahatarisha amani tuliyonayo na usalama wa Taifa kwa ujumla.

Anaposema Diamond ni member wa Freemanson, inamsaidia nini mtu akishafahamu hiyo imani ya Diamond, hii haimpi mtu ticketi ya kwenda mbinguni eti tu kwa vile umeishafahamu Diamond ni Freemanson, ticketi ya kwenda mbinguni ni kufanya yale yanayompendeza na aliyoagiza Mwenyezi Mungu kwa wanadamu, pia kwa kujua Diamond ni Freemanson haikupi wewe Kinga against matendo ya Shetani.

Mamlaka husika zimdhibiti huyu anayejiita Askofu aliyegeuka Mr Mipasho wakati waumini wake wana kiu ya neno la Mungu,wiki nzima mtu umekuwa bize na mihangaiko ya maisha, Jumapili inafka unasema uende ukamuabudu muumba wako instead unakutana na mipasho mwanzo mwisho over 5 hours, this is not fair to these poor followers.
 
Hivi Tanzania hatuna National Security Council, Matukio ya kiusalama Raisi anayopokea kutokea Kwa DG wa TISS na Minister of Home affairs, It's our time to establish National Security Council which will discuss na Report Direct to Our president Issues concern Security, TISS is Too Politics now and it's not independent Agency anymore
 
Kuhusu Diamond naona Gwajima anatwanga maji kwenye kinu kwa sababu hakuna hata kimoja atakachosema ambacho watu hawajasema:
  • Kwamba Diamond ni Freemason watu washasema sana siku za nyuma....
  • Kwamba Diamond anauza unga watu washasem sana siku za nyuma....
  • Kwamba Diamond amebambikiwa watoto; watu washasema sana siku za nyuma.....
  • Kwamba Zari yupo kwa Diamond kwa mkakati maalumu wa kumchuna pesa; watu washasema sana siku za nyuma....
  • Kwamba Tiffa ni mtoto wa Katunzi; watu washasema sana siku za nyuma
  • Kwamba kale kidume cha sasa ni mtoto wa Ivan; watu washasema siku za nyuma.....
  • Kwamba Diamond ana radhi za babake; watu washasema sana siku za nyuma....
Itoshe tu kusema kwamba safari hii Gwaajima hakuchanga karata zake sawa sawa!! Manake hata akisema Diamond alipata ZERO bado wala haiwezi kuwa story!! Inawezekana kushinda kwake madhabahuni alidhani kuna scandal ambayo inaweza kumtetemesha Diamond bila kufahamu kwamba yoooooooooooooooote yameshasemwa huko nyuma!!!

Hili la Halima Mdee binafsi ndo nikachoka kabisa!!! But trust me; Gwajima amepigwa mkwara afunge bakuli lake na ndio maana siku hizi humsikii akizungumzia suala la Makonda!! Lakini kwavile ameonja tamu ya publicity ya Instagram kupitia Daudi Bashite; anachofanya hivi sasa ni kutafuta attention kwa njia yoyote ile!!!

UPDATE:

Hii post watu wengi sana wamei-quote na karibu wooooooooooote hoja yao inashangaza sana tena kupita kiasi! Karibu wote hoja yao ni kwamba "kama huyo Diamond yote yameshaongewa dhidi yake na kwahiyo hawezi kutishika; sasa mbona alikimbilia kuomba radhi!"

Hii hoja ni ya ajabu au inawezekana inatokana na tofauti za malezi!! Kwa muungwana; kuomba radhi sio dalili ya woga wala kukubali kosa... hiyo ieleweke! Kwa muungwana, hata kama anaona hajakosea lakini kama kuna mtu amekwazika; bado ataomba radhi kwa sababu amemkwaza mtu!! Hata ukiangalia kwenye post ya Diamond, alichofanya ni kutoa ufafanuzi wa ubeti wake na wala hadhani amemdhalilishwa Gwajima lakini pamoja na yote hayo; akamtaka radhi!!!

Kwanza hebu tuone mistari iliyomzungumzia Gwajima! Hii hapa:

Mama ananiambia Nasibu we ni mtu mzima nakutegemea,
Yanayotokea jaribu kupiga kimya usidiriki hata kuongea,
Mara nasikia vya aibu, Gwajima Konda eti ugomvi umekolea,
Kuchunguza karibu, ni binti mmoja kwa mitandao anachochea,

Sasa tuanze na wale wanaokomaa kwamba eti Gwajima "amechokozwa!" Hivi hapo alichochokozwa hasa ni kipi hadi muone Gwajima alistahili kuapiza kwamba ataigeuza almasi kuwa maji?! Btw, hivi huyu Mheshimiwa si Askofu kwa maana ya kwamba ni kiongozi wa kiroho?!

Hivi ikiwa mistari kama hiyo tu ilimfanya aapize kulipa kisasi na kweli akafanya hivyo; what kama yale maneno ambayo yeye alimuongelea Askofu Pengo ingekuwa ndo ameambiwa yeye si angekodisha Al Shabaab kabisa?!

Hivi hamuoni hapo ndo mnampa credit Diamond aliposema "kuchunguza karibu ni binti mmoja kwa mitandao anachochea!" Hivi kwa mistari kama hiyo watu kukomaa kwamba Gwajima amechokozwa si ndo kuchochea kwenyewe huko?!

Naongea hili kutoka ndani kabisa ya moyo wangu!! Kama kuna wafuasi wa Gwajima wanaoshabikia mambo ya kwamba "...si amechokozwa..." Trust me, mnampa picha mbaya sana kiongozi wenu ingawaje ni picha aliyoijenga mwenyewe!! Kwa sababu; mosi wala sioni hicho alichochokozwa hapo ni kipi! Lakini hata kama kweli amechokozwa; hizo sio sifa za kumpa kiongozi wa kiroho... kwamba "...ana haki ya kujibu mashambulizi kwa sababu amechokozwa!"

Na kama mtu anafikiri sawasawa, hatua ya Diamond kuomba radhi ingawaje sioni kosa lenyewe lakini bado Gwajima akaendelea na visasi ni hatua inayozidi kumchora picha mbaya Gwajima kwamba pamoja na Kiongozi wa Kiroho kuombwa msamaha lakini bado akaendelea na jicho kwa jicho; jino kwa jino "...kwa sababu alichokozwa!"

Wafuasi wa kweli wa Gwajima nilitarajia wangeonea aibu suala hili lakini kwa bahati mbaya nao wapo walioingia kwenye mtego wa wafuasi wa Mange na Ali Kiba ambao ima fahima lazima washabikie kusikia Gwajima ameapa "kumchana chana Diamond!"

Mimi sio mfuasi wa Gwajima na wala sio Mkristo!! Lakini kwa kufahamu nafasi ya Gwajima kwa jamii na kwa kufahamu uendawazimu wa mashabiki wa Diamond, juzi niliandika posts 3 kwenye wall ya Gwajima na nikamweleza wazi kwamba sifa zako zinatokana na "kumchana chana" Askofu Pengo, Dr. Slaa na Makonda!

Nikamwambia wazi kwamba hao watu kutokana na nafasi zao kwa jamii wasingeweza kujibizana na wewe matokeo yake umeingia kiburi kwamba wewe huchokozwi na mtu akikuchokoza atakiona cha moto kwa sababu tu wale waliokiona cha moto waliamua kukaa kimya!!

Nikaendelea kuandika lakini huyu wa sasa hata kama mweyewe hatakujibu lakini ana wafuasi ambao wengi wao hawana adabu hata kidogo!! Wafuasi wake hawa hata mama Mzazi wa Diamond mwenyewe anawaogopa! Nikatoa ushauri kwamba aachane na hayo mambo manake yeye kama kiongozi wa dini haitapendeza hata kidogo atakapoanza kuporomoshewa matusi mitandaoni! Nikamwambia wazi "usipofuata ushauri huu; hesabu kesho akaunti yako utaiweka private bila kutaka!!!!

Kama mnavyomsifia kwamba the guy is unbeatable hakufuata ushauri! Akapuuza hata ushauri wa Mkude Simba ambae alitangaza hadharani kwamba ni rafiki yake!!!

Na ambacho nilikisema juzi ni kweli jana kilitokea hadi akalazimika kuiweka akaunti yake private kwa saa kadhaa baada ya kushindwa kuhimili mvua ya matusi na kashifa!

Gwajima.png

Sasa endeleeni kumjaza kwamba "alichokozwa" lakini mjue huko Instagram anakohamishia vita zake kuna watu wamepinda mara elfu moja ya Gwajima!!! Na mbaya zaidi ni watoto wadogo!!!


Na kama wewe ni mfuasi wa Gwajima halafu bado unashabikia jambo kama hili basi utakuwa inashangaza kuona watu wa madhabahuni wanashabikia visasi!!!!

Mkuu Christine ibrahimu nadhani hapa nawe nimeshakujibu kwamba "..mbona aliomba radhi!" Hata hivyo, kuna mahali ni kama hukunisoma vizuri!!! Hakuna niliposema Gwajima amewataja wanafamilia ya Diamond; HAKUNA!

Nilichosema ni kwamba hakuna ambacho Gwajima angesema ambacho huko nyuma hakijasemwa! Hata kwamba watoto wa Diamond wote sio wake nayo yashasemwa sana na kuandikwa kwenye magazeti ya udaku!! Kwamba Zari yupo pale kwa mission maalumu nayo yashasemwa sana!!!! Kwamba Diamond ana radhi ya babake nayo yashasemwa kwahiyo hapawezi kuwa na jipya!!
 
Back
Top Bottom