May Day
JF-Expert Member
- May 18, 2018
- 6,367
- 9,112
Nguruvi3,
Umedadavua vizuri sana Mkuu..ila kwa mimi sioni ushahidi wa moja kwa moja kama Mamlaka zingemzingatia Sheikh yeyote(asiye rasmi) ambaye angetamka kama alivyotamka Bw Gwajima (kwamba angetamani Makanisa kuwa misikiti n.k).
Maana pia haya hutegemea sana mazingira... na kwa bahati mbaya au nzuri mazingira ya imani hizi mbili yanatofautiana kwa namna moja au nyingine...kwa mfano kwenye ukristo kuna utitiri wa "mabanda" mitaani yanayojitambulisha kama nao ni nyumba za ibada, tofauti na ninavyoona kwa Uislam(labda kama sifahamu zaidi)... hivyo basi anachoongea Kiongozi wa banda fulani sidhani kama italinganishwa na atakachoongea Sheikh iwapo ataongelea kwenye nyumba rasmi ya ibada(Msikiti).
Hivi maneno kama hayo yatamkwe na Askofu wa Katoliki, Anglican au Lutheran unadhani Mamlaka zitakaa kimya? na sidhani kama zitaachiwa mamlaka pekee bali ni jamii yote itaguna.
Kwa hiyo nasisitiza kuwa Mzee Said hana sababu ya kulinganisha mambo yasiyowiana kwenye mizani, Gwajima ni Kiongozi wa kikundi chake tu hapo Dar.