Nyakageni
JF-Expert Member
- Feb 1, 2011
- 15,044
- 5,114
We mzee muungawana sana. Shikamoo. Kuna mada huwa natofautiana sana na wewe. Ile nyingi sana uko sahihiKinyungu,
Sikuwa nafahamu na jamaa wamenisahihisha nami nimerekebisha.
Nakutakeni radhi.
We mzee muungawana sana. Shikamoo. Kuna mada huwa natofautiana sana na wewe. Ile nyingi sana uko sahihiKinyungu,
Sikuwa nafahamu na jamaa wamenisahihisha nami nimerekebisha.
Nakutakeni radhi.
Ikarahani,Nafuta kauli yangu kuwa wewe siyo mnyonge.
Lakini bado naamini kuwa nchi yetu Tanzania haina dini, bali wananchi wake ndiyo wenye dini. Mara kwa mara kumekuwa kukitokea changamoto zinazohusisha dini (dhehebu kwa dhehebu au dini moja dhidi ya nyingine) binafsi yangu toka moyoni sipendi dini yangu iwe kubwa kuzidi maslahi ya taifa langu hivyo mtu yoyote anayetokea kuanza kukashifu dini ya mwenzake (hata kama mtu huyo ninashiriki naye nyumba moja ya ibada) huwa ninamuangalia kwa jicho la tofauti.
Kwangu mimi naichukulia dini kama njia ya kiroho kutupeleka peponi lakini pia ndani yake imebeba mila na tamaduni za waliotuletea dini hizo mfano majina, mavazi, vyakula, ustaarabu nk. Kulitokea makosa fulani kwa watangulizi wetu (mababu) kukubali kila walichoambiwa na hao waleta dini. Walishikwa akili na kuaminishwa kuwa kila tulichonacho ni kibaya ila vyao ndiyo vizuri matokeo yake tukaacha majina yetu mazuri ya kiafrika, tukaacha na utamaduni wetu mzuri nk.
Leo hii wakitaka kutufitinisha mara nyingi hupenda kutumia misaada pamoja na dini. Binafsi namshukuru MUNGU kwa hili maana kwa Tanzania hawajafanikiwa (ninaomba wasifanikiwe), hivyo nakuomba uwe mshirika wangu kwa kupinga udini Tanzania kwa kuwakemea wanaoendekeza udini na siyo kuwapigia chapuo.
Nyakageni,We mzee muungawana sana. Shikamoo. Kuna mada huwa natofautiana sana na wewe. Ile nyingi sana uko sahihi
Ameuliza tamko hilo lingetolewa na Muislam kuzigeuza Sunday Schools zote nchini kua Madrasa ingekuaje?
Ikarahani,
Ili Tanzania iwe na serikali ambayo haina dini lazima wafuasi wa dini mbili hizi wawe na uwiano sawa au karibu na sawa katika uendeshaji wa serikali.
Hili halipo Tanzania ratio kama Waraka wa Taasisi na Jumuiya za Kiislam zinavyoonyesha ni 20:80.
Hili Waislam wamekuwa wakiitahadharisha serikali kwa miaka mingi.
Hawa wanaohodhi madaraka kwenye maamuzi ya serikali watafanya maamuzi yenye maslahi na imani zao.
Mifano ipo mingi.
Ikarahasi...Siwezi kukupinga wala kukuunga mkono kwa maana sina utafiti nilioufanya, lakini kwa nionavyo mimi baadhi yetu tunahisi kubaguliwa na hii hupelekea kuanza kujitenga na kujibagua wenyewe (hili halipo kwenye dini tu). Tangu nimepata kujitambua sijawahi kuhisi wala kusikia kuwa serikalini watu huchaguliwa/huteuliwa kwa kufuata dini, nijuavyo mimi kuna sifa mtambuka zaidi ya dini na kabila.
Kuna baadhi ya maeneo watu wa dini fulani ni wengi kuliko wa dini nyingine na hii imetokana na mapokeo (wewe unajua), pia kuna usomi wa elimu dunia. Sijawahi kusikia kwamba mtu wa taaluma fulani mwenye sifa za kitaaluma amekataliwa kuajiriwa serikalini kwa sababu ya dini yake.
Huo uwiano unaosema ni 20: 80 sidhani kuwa Serikali imekaa kimya bali kuna maelezo huwa yanatolewa sasa yawezekana baadhi yetu hatukubalinai nayo. nakumbuka enzi za Rais Mwinyi alituhimiza kusomesha watoto baada ya kuulizwa swali lililoonyesha kuna upendeleo kwa dini fulani kiserikali.
Hiyo ni kama Siasa.. CCM wangetamani wanachama wa Chadema wajiunge nao..Hali kadhalika Chadema wangependa CCM members wote wajiunge na chama Chao na hiyo sio dhambi kama Una uwezo wa kushawishi..kama sheikh anawashawishi waumini wa Sunday schools wajiunge na madrasa Kwa wingi ni Jambo la linalofanyika kila siku ila Kwa uchache Sana(watu wanabadili dini kila kukicha).Kinyungu,
Kweli hebu fikiri sheikh angesema nataka nigeuze Sunday schools zote ziwe madrasa ingekuwaje.
Ndugu yangu kakupa ushauri mzuri.
Fanya hivyo na rejea hapa utupe fikra zako.
Mohamed Said, Yaani nikiangalia clip alipokuwa akiponda ubunge kwa dharau zote waumini wanashangilia kwa mbwbwe zote na miluzi halafu clip ya juzi akitangaza kutia nia na kupamba uamuzi wake wa kigeugeu bado waumini wanashangilia pia kwa miluzi, nimeona aibu sana kwa niaba ya waumini hao.
Yani kiongozi wa dini anaweza kuchezea akili za watu apendavyo kwa kigezo cha imani tu jamani!!!!. Imani ya hivi ni kuuza utu na ufahamu wako ambao ni zawadi binafsi kutoka kwa Mungu!!!!
Kama dhana ya dhambi ni halisi, tendo hili ni dhambi pia!!!!
Weeeee! Mtu alisema Yesu sio Mungu alifungwa huko Moro bila waislam kuingilia kati ilikuwa nitoleee
[/QUOTE
Alisema akiwa wapi na mkutadha geni
Samahani ya nini Sasa na wewe? UMENENA. OverHuyu mtu na nabii tito utofaut ni kidogo tu, Gwajima ana miujiza ya mazingaombwe ila nabii tito hana ila matendo wote sawa tu.
Hamna alicho ongea kikatimia kila kitu lazima kiende kombo, 2015 team lowassa, 2020 team magufuri, 2025 team makonda
Samahani waumini wa Gwajima
Hivi huyo Bw Gwaji ana wafuasi wangapi?, kwa nini unataka ionekane kana kwamba anayofanya au kusema huyo Bwana anawakilisha jamii nzima ya Ukristu?.
Hivi ni mangapi tunakutana nayo mitaani na tunayapuuza...kuna wakati unapita unakuta Mtu kakusanya Watu anaongea mambo yake tena kavaa kanzu na baragashia lakini Mtu unapita na zako unaachana nao...tukianza kushabikia kila kitu kinachofanywa na kila Mtu sidhani kama tutapata muda wa kufanya mambo mengine ya muhimu.
Kama hayo Magazeti yamempuuza kwa nini na wewe unashindwa kumpuuza?, ni wapi umeona Nabii Tito akipewa kipaumbele kwenye vyombo rasmi vya habari zaidi ya mitandaoni?...Kwa nini wewe unatamani wawe wanatoa uzito kwa mambo yasiyo na afya kwa jamii kama hayo?.
Sasa hao ndio Watu wanaopaswa kupuuzwa na Wajumbe, wasiangalie rushwa tu za kuneemesha matumbo yao wakatuwekea Mtu asiye na faida kwenye Jamii kubwa...huyo anapaswa kubaki huko kwenye kundi lake.Wajumbe wameshafanya yao! Lets move on.
Kukosekana ulinganifu baina ya watu wa mzee Saidi hakutoi uhalali kwa watu wengine kutoa matamko yenye kuleta hisia hasi kwa watu hao.May Day, kuna hoja ambayo sijui kama wengi wanaielewa! huenda wanaielewa lakini hawataki kukabiliana nayo. Hilo ni tatizo kubwa kwa Watanzania.
Wazungu wanasema 'ukitaka kupata suluhu ya tatizo lazima kwanza ulitambue tatizo''
Hapa kuna sehemu mbili za kuongelea
Mohamed Said anauliza, je ingalitokea maneno hayo kayasema Sheikh, je, magazeti unayosema yangepuuza?
Je, vyombo rasmi unavyosema vingepuuza kama vinavyompuuza Nabii tito?
Je, wangeacha kutoa uzito kwa mambo yasiyo na afya kwa jamii?
Kwahiyo unatakiwa kumjibu Mohamed Said hoja yake kwa mtazamo wa Askofu Gwajima vs Sheikh X
Wakati ukitafakari kumjibu Mohamed, nikukumbushe kuwa kuna kauli kama ''siasa kali, fundamentalist'' , kwamba kauli hizi zinatoka wapi kama tuna uwezo wa kupuuza kila kitu kutoka kwa hawa viongozi wa dini?
Kwa upande wa pili, kuna tatizo kwa Mohamed Said kugoma ku appreciate'' uwepo wa tatizo kwa watu wake
Mathalan, Juzi katiwa ndani Sheikh Ponda . Siku iliyofuata Sheikh Kundecha kakanusha waraka.
Siku iliyofuata shura inakubali waraka huo ni wao.
Katika mazingira haya unawezaje kusema '' waislam wapo kimya' na si kuwa wamepagawa?
Huwezi kuangalia waraka wa Ponda kwa jicho la waraka wa Maaskofu.
Ukifanya hivyo bila kuangalia tatizo la msingi ni kukwepa ukweli.
Kabla ya ulinganifu unatakiwa ujiulize kwanza, je, kuna ulinganifu miongoni mwa watu wako?
Na wala huwezi kuangalia waraka wa Ponda kwa jicho la serikali bila kujiuliza serikali hiyo ipoje madarakani?
Utaratibu wa nchi, serikali inatokana na chama, na chama tawala ni CCM
Nitaendelea nikipata nafasi, nalala niwahi shambani kesho.
Magimbi hapa Magila na Kicheba tumejaaliwa mwaka huu