Gwajima: Mama katili anaetesa watoto wa kufikia amekamatwa

Mjanja M1

JF-Expert Member
Oct 7, 2018
3,660
12,306
Dr. Dorothy Onesphoro Gwajima, Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Wanawake na Makundi Maalum, ametoa taarifa juu ya kushikiliwa kwa muhusika aliewanyanyasa watoto wake wa kufikia.

Waziri Gwajima ameandika kwenye ukurasa wake wa "X",

"Video fupi inayozunguka mitandaoni na yenye kipande chenye mwonekano kama kwenye picha hiyo, wakiwemo pia watoto wenye alama za makovu kwa madai ya kuteswa na mzazi wa kufikia (mama); wamepatikana kwa ushirikiano na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga na Wataalamu wake wa Ustawi wa Jamii. Aliyewakatili naye amepatikana na hatua za kisheria zinaendelea dhidi ya katili huyo".

Screenshot_20240126-174101.jpg


Written by Mjanja M1

 
Nahitaji namba za kuwasiliana na wadau ambao wana deal na masuala ya unyanyasaji wa watoto.
Najirani yangu anafanya kama walivyofanyiwa hao watoto.
 
Back
Top Bottom