Mama wakambo ageuka mwiba kwa watoto

mwehu ndama

JF-Expert Member
Nov 12, 2019
543
1,875
Wasalaam wakuu!

kama nilivyowahi kubainisha katika moja ya nyuzi zangu kuwa kila nitakapokuwa napata fursa ya kuandika hapa jukwaani, basi nitakuwa naruka na masingo maza mpaka wateme mabungo,

Well katika kipande hiki cha video, watoto wadogo wanaokadiliwa kuwa na umri wa miaka 4 na 5, wanaonekana wakiwa katika hali mbaya kiafya na makovu ya majeraha yatakonayo na mateso wanayoyapitia kutoka kwa mama yao wakambo, ambapo katika kipande hichi cha video mtoto wa mama Huyo wa kambo ni Huyo binti mwenye kinguo chekundu akiwa na afya tele

NB: habari kutoka chanzo cha uhakika zinadai mama Huyo wakambo ni single maza anayeishi kinyumba na baba wa watoto hao, yaani jamaa ilibidi amuweke ndani single maza mkombozi wa ukoo akiwa na imani kwamba atakuwa mama bora kwa wanae pia, hasa kwa kuzingatia kwamba Kausha Damu Huyo na yeye pia anamtoto. Huenda kama baba wa watoto hao angelikuwa ni mwana Jf haya yasingemkuta maana tumekuwa tukiwaasa sana masela juu ya hatari ya kuparamia masingle maza åka makausha Damu.
Yaani katika zama hizi wanawake kibao lakini mtu bado unaamua kwenda kuanza mechi ukiwa umetanguliwa goli la ugenini, hii ni hatari sana.

Baada yakuwataarifu juu ya hili, naruka nakupepesuka kimadoido, huku nikiachia kipaza cha jukwaa kimanjonjo kabisa

Adios amigo!!!!!
 
Hata asingekua single mother angewatesa tu. Chagueni kwa umakini wanawake wa kuzaa nao ili masuala ya kutesa watoto yasitokee,watoto walelewe na mama yao mzazi
 
Hawa masingo maza ni makonkodi ya maisha. Hayana huruma na watoto wa wenzao. Huyo jamaa aliyemuoa naye hazimtoshi. Hao watoto wake angewaacha kwingine mradi tu awe anawapelekea mahitaji kuliko kuungaunga familia mbili huku akijua watoto wake wataishia kunyanyaswa. Bibi/babu na ndugu wengine wapo wa kusaidia kulea watoto wa mke wa kwanza, kama vipi watoto wabaki na mama yao huko aliko kama mmeachana kuliko mwanaume kung'ang'ania watoto na kwenda kuishi nao kwa mwanamke mwingine asiyethamini watoto wasio wake
 
Back
Top Bottom