Serikali imuunge mkono Askofu Dr. Gwajima katika mpango wa kununua Treni ya Mwendo kasi

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,895
Serikali imuunge Mkono Gwajima katika mpango wake wa kununua Treni

Heshima kwenu wakuu,

Baba Askofu Dr. Gwajima, ameanza mchakato wa kunua Treni ya mwendo kasi ambayo itakua inatoka Dar hadi Morogoro. Katika usajili bado anawekewa Zengwe, ila nia yake ni nzuri kabisa.

Katika Tanzania ya Viwanda, hatuwezi kufanikiwa Tanzania ya viwanda kama hatuna Usafiri wa Uhakika wa kutoka sehemu moja hadi nyingine.

Tayari kashafanikisha Mpango wa kujenga chuo cha Urubani, anasubiri ruksa ya Rais Magufuli. Dr Gwajima alishampeleka Mkufunzi wa mambo ya ndege kusomea kufundisha mambo ya ndege. Kwa Tanzania watu wengi wanapenda Urubani lakini garama za masomo ni kubwa. Hivyo kampeleka Kaka John kusomea Ualimu wa ndege. Nadhani wote mnamjua John wa Ufufuo na uzima. Ni kijana mwenye akili sana.

Hadi sasa Dr Gwajima kushirikiana na Msukuma(Mbunge) wameshaanza mchakato wa kumuona Rais ili awape sehemu ya kujenga chuo cha Urubani.

Vilevile ameshaagiza Chopa tatu kwaajili ya wanafunzi.

Wito wangu
Naomba Serikali isilete siasa katika hili Swala kwani lina manufaa kwa Watanzania. Tutawanyanyasa wawekezaji lakini Kenya ikiwachukua tunaanza kulalamika.

Askofu Dr Gwajima kwa wasiomjua, ni Askofu wa Makanisa ya Ufufuo na Uzima ambayo ni Zaidi ya Makanisa mia nne(400) Dunia. Vilevile ana makampuni mengi kama makanisa mengine yalivyo na mabank mfano Mkombozi, Efatha Bank nk.

Dr Gwajima ni Mwalimu ambaye Hulipwa zaidi ya dola 1,000/= kwa saa. Anafundisha Mambo ya Kiroho Duniani na huwa anaalikwa kufundisha hata kwa miezi mitatu.

Kwa sasa anamiliki ndege ambayo humuwezesha kuhudumia Ibada katika Makanisa Matatu Tofauti mikoa tofauti kwa siku.

Watanzania tuache wivu na kijicho cha roho mbaya, bali tuwaunge mkono Watanzania wenzetu ambao Mungu Kawainua.

Daniel 3:16-30

16 Ndipo Shadraka, na Meshaki, na Abednego, wakajibu, wakamwambia mfalme, Ee Nebukadreza, hamna haja kukujibu katika neno hili.

17 Kama ni hivyo, Mungu wetu tunayemtumikia aweza kutuokoa na tanuru ile iwakayo moto; naye atatuokoa na mkono wako, Ee mfalme.

18 Bali kama si hivyo, ujue, Ee mfalme, ya kuwa sisi hatukubali kuitumikia miungu yako, wala kuisujudia hiyo sanamu ya dhahabu uliyoisimamisha.Tanuri Liwakalo

19 Ndipo Nebukadreza akajaa ghadhabu, na sura ya uso wake ikabadilika juu ya Shadraka, na Meshaki, na Abednego, basi akatoa amri watie moto ile tanuru mara saba kuliko desturi yake ya kutiwa moto.

20 Kisha akawaamuru baadhi ya watu mashujaa wa jeshi lake kuwafunga Shadraka, na Meshaki, na Abednego, na kuwatupa katika ile tanuru iliyokuwa ikiwaka moto.

21 Basi watu hao wakafungwa, hali wamevaa suruali zao, na kanzu zao, na joho zao, na mavazi yao mengine, wakatupwa katikati ya ile tanuru iliyokuwa ikiwaka moto.

22 Basi kwa sababu amri ya mfalme ilikuwa ni kali, na ile tanuru ilikuwa ina moto sana, mwako wa ule moto ukawaua wale watu waliowashika Shadraka, na Meshaki, na Abednego......

====

Askofu Gwajima kununua Treni, ni kielelezo cha siasa safi?
 
Naomba mdau atuletee mahubiri mubashara ya Dkt Gwajima kutoka kanisani kwake!
Sidhani kama nitaudhuria pale!
 
Wakati alipotuhumiwa aliongelea kwamba kuna kampuni kutoka nje ya nchi inampa ufadhili.
Kwa hiyo inawezekana hiyo pesa anapewa kutoka huko lakini tujiulize anapewa kwa masharti gani maana wazungu ni wajanja Sana wanakuja kwa via ya umisionary kume wameona fursa ya rasilimali.
 
Hzo Hela Amepata Wapi?Wakati Baba Jesca Kila Siku Anahaha?Ujenzi Unaogarimu Zaidi Ya Trilion 2?Labda Hyo Chuo Cha Urubani Anaweza
 
CHARITY START AT HOME(hapa na maanisha kanisa lake lina hali gani????..)......hivi porojo zote ulizo leta hapa hauoni hata aibu...

Hilo kanisa la ufufuo na UZIMA ameshindwa hata kulijenga na kuliweka katika condition nzuri......HATAWEZA VIPI KUSIMAMIA HAYO MANENO YAKE ya kuwa na chuo cha URUBANI na kujenga treni ya mwendo kasi ili hali NYUMBA YAKE TU YA IBADA majanga........
Mimi kwa upande wangu sijawai mwamini GWAJIMA kuhusiana na UTAJIRI WAKE....unatia mashaka sana sana

Na tutakuwa na SERIKALI YA KIPUUZI kumpa mtu KIBALI kufanya haya yote anayotaka bila ya KUWA NA UHAKIKA NA VYANZO HALALI YA PESA ZAKE.........
 
Back
Top Bottom