Josephat Gwajima ni Askofu na mwanzilishi wa kanisa la 'Glory of Christ Tanzania Church' GCTC (Ufufuo na Uzima Ministries), kadhalika ni mwanasiasa ambaye mwaka 2020 alichaguliwa kuwa
mbunge wa jimbo la Kawe kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi CCM, ambaye pia ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya chama hicho Taifa (MNEC).
Mnamo tarehe 15 Agosti, 2025 Askofu Gwajima alizungumza mbashara kupitia Mtandao wa
YouTube ambapo alitumia nafasi hiyo kutoa ushauri wake kwa Taifa la Tanzania pamoja na viongozi wake hususani kuelekea uchaguzi mkuu 2025.
Kumekuwepo na
taarifa inayosambazwa mtandaoni kuwa 'Askofu Gwajima amkosoa Polepole vikali, amuita mnafiki' huku ikitumia utambulisho wa grafiki za Millard Ayo.
Je, ni upi uhalisia wa taarifa hiyo?
Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia utafutaji wa maneno muhimu (Key Word Search) pamoja na marejeo ya video, JamiiCheck imejiridhisha kuwa taarifa hiyo si ya kweli.
Aidha grafiki iliyotumika kusambaza taarifa hiyo si ya kweli, bali ni la kughushi kwani halijachapishwa na
Millard Ayo kupitia kurasa zake rasmi za mitandao ya kijamii.
Aidha akizungumza kupitia YouTube Gwajima hakumkosoa kwa namna yoyote aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Humphrey Polepole, bali
alisema
"WanaCCM wanaolalamikia mchakato wa ndani ya Chama cha Mapinduzi wa kugombea Urais wapo na wenyewe kama milivyomsikia vile, Balozi mstaafu wa Cuba na mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi na Mbunge mstaafu ndugu yangu Humphrey Polepole.
Wanavyolalamikia, ina maana kuna wanachama wa Chama Cha Mapinduzi na wao pia ndani ya mioyo yao wana msimamo kama wa Polepole, wana msimamo kama wa Dkt. Godfrey Malisa, Hawa na wao familia hii na wao watatupa kura?"
Rejea kuanzia dakika ya 40- YouTube
View: https://www.youtube.com/live/94t64efdNxY?si=jegqkctWAt-v2ufX&t=2404