Gwajima aishauri Serikali kumkamata Ahmed Msangi

Saraalee!! Aibu kubwa kwa jeshi la polisi na serikali ya Magamba. Nimependa sana ITV walivyoripoti kwa kuweka kipande cha povu alilolitoa Kova. These are signs of the falling empire.
 
Kova umejitia aibu, ebu achia hicho cheo hakikufai,. Unataka uchafue ukristu ushindwe katika jana la mwenyezi
 
Nimemwona Gwajima "akimvua nguo" Kova. Sijui Kova ataweka wapi uso wake! Uzuri wa mijitu hii, haina aibu.
 
Mchungaji Gwajima ameliumbua jeshi la polisi kwa kukanusha maelezo ya Kamanda Kova kuhusu mkenya aliyekamatwa kwa utekaji na kuumizwa kwa Dr. Ulimboka.

Mchungaji Gwajima amesema si kweli kuwa huyo mkenya alienda kutubu kuhusu ushiriki wake katika utekaji wa Dr. Ulimboka na kufafanua kuwa hata kama huyo mtu angekuwa ameenda kutubu kweli basi kanisa lisingeweza kusema ametubu kuhusu nini maana ni kinyume na taratibu za kanisa.

Gwajima amelishauri jeshi la polisi kutoshiriki katika uchunguzi wa tukio la utekaji wa Dr. Ulimboka na kuacha kusingizia watu.

Source - Taarifa ya habari ITV

Kova na jeshi zima wameumbuka sana. Inabidi wajipange upya.
 
Hakika leo ITV imenifurahisha jinsi ilivyoonyesha Mch Gwajima akiongea kwa kujiamini na kuivua nguo Serikali jinsi ilivyodanganya kuhusu mtuhumiwa wa utekaji wa Dr Ulimboka kuwa alikamatwa baada ya kwenda kutubu wakati sio kweli!
Gwajima amesisitiza Serikali iunde tume huru kwa sababu hao polisi nao ni watuhumiwa!!
 
Hata mimi nimeona!!Duh watu wazima wameumbuka sana!!!Sijui kina Kova watakuja na single gani tena!!!
 
ITV wamemalizia kwa kuweka video ya Kova akiongelea khs huyo mkenya
kweli hii kuna mambo
 
Waheshimiwa, nchi hii haina usalama wa raia wala usalama wa Taifa. ni matatizo tu. that is why unaona maovu yakitokea hivyo vyombo ndio vinakuwa msitari wa mbele kutetea hayo maovu, jambo linaloonyesha wazi kuwa wanajua kilichotokea.mimi nadhani ni vyema huyo mwehu wao wamtunze, then dr. ulimboka akirudi amtambue, ndipo utakapochoka na kuamini kuwa nchi hii inaendeshwa kimkanda mkanda tu !Huyo Mwehu amepandikizwa wakiwa wanaamini kuwa wananchi hawana uelewa so watasikiliza na kuamini kuwa huyo mwehu wao alimteka Ulimboka. Sasa kanisa limekataa, watasema nini tena ?
 
Gwajima kasema govt inahusika,tume huru iundwe!yule mtu kapandikizwa sio muumini wala hajaungama mbele ya kanisa!
 
jamani, angalieni video ya Dr Ulimboka kwenye you tube,hawa watu Ahmeid na Rama mbona hawakamatwi?

hapa tujiandae,watatafuta tukio moja kubwa ambalo watalitumia kufukia hiki kisanga cha Dr Ulimboka

kuna kila dalili ya GVT kuhusika katika hili jambo.:wacko::wacko:
 
Back
Top Bottom