Uchaguzi 2020 Gwajima adai Mdee alimuwekea vizuizi Magufuli kupeleka maendeleo Kawe. Je, inawezekana kweli?

Ndio mana Mimi huwa siendi makanisani, maana ni kwenda kubeba dhambi za waovu kama kina gwajiboy,ni bora ushinde bar utaiingizia nchi mapato kuliko huko kwa wanaojiita watumishi
 
Kwani pale JPm anapotaka bajeti yake ipitishwe bungeni ili ikafanye kazi majimboni alafu Mdee anakataa kuipitisha huoni hapo ni kizuizi?

Halima aliwahi kuzuia barabara isijengwe jimboni kwake?? Alifanya matendo gani kuizuia serikali isitekeleze majukumu gani??

Hujasikia JPM akisema huko kwingine kwa wapinzani hakuwapa maendeleo kwa sababu hawakumchagua??? Nilitarajia uniambie kwa kuwa wapinzani walipinga bajeti, JPM alipeleka maendeleo Chemba, Mvumi, Meatu na kadhalika!!
 
Katika mkutano wa kampeni unaoendelea hapo Kawe, mgombea wa Ubunge wa Kawe kupitia CCM, Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Josephat Gwajima amesema jambo fulani la kushangaza...
Umesahau mdee aligomea bajeti zote tano au wewe kipofu
 
Kwani pale JPm anapotaka bajeti yake ipitishwe bungeni ili ikafanye kazi majimboni alafu Mdee anakataa kuipitisha huoni hapo ni kizuizi?
wajinga kumbe wapo wengi
kumbe Bunge ni rubber stamp, halina meno sasa wameenda kufanya nini huko km miradi inaamuliwa Ikulu, wakati wanaposema maendeleo hayana vyama,
mnaunga mikono ya ndiooooo mtu anapoamua kujenga uwanja wa ndege na cha mpira wakati wapiga kura wanashabikia upinzani, mbunge wao anapigwa kisa tu Mdee kagoma kuipitisha
Tuwekane sawa tu Bunge bila upinzani halina meno pesa zote sasa hazitapita kwao, Zitto alisema wakamuona juha
 
Yaani Mbunge amuwekee vishawishi Rais wa nchi?!

Hii ni akili ya Gwajima na wajinga wenzake wa CCM.
Na Kama kweli Mbunge kamvimbia Rais na Rais kashindwa kufanya Maendeleo Lisa Mbunge, basi Rais huyo Hafai mana ni Rais dhaifu.
 
Wapigakura wengi wako mtaani hawamo humu kwenye mitandao!

Gwajima hazuiliki!
Mwanzoni nilikua nashangaa kwanini baadhi ya watu humu hushangilia misiba au matatizo ya maccm au kundi flani la watu, nikaja gundua kuwa uonevu huzaa chuki na visasi kwenye mioyo ya watu. Unamcheka anayepigwa na polisi leo, kesho usitegemee akaja kulia kwenye msiba wako.

FUNZO: Ukiwa mnufaika (beneficiary) wa mfumo wowote ule usitumie vibaya hiyo privilege kuwatukana/gandamiza/dharau/piga/onea wengine, Hakuna hali inayodumu milele.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
..Ndio anazidi kujiharibia.

..Anajiita Askofu halafu anasema uongo wa waziwazi.
Mkuu JOKAKUU HESHIMA YAKO.

Alafu ndo mtu pekee ambaye CHADEMA walimtegemea katika USHENGA uleee ha ha ha ha TANZANIA UBARIKIWE NA USIVURUGWE.
 
Huyo Gwajiboy ni tapeli na muhuni tu ambaye yuko tayari kusema uongo wa kila aina ili kutafuta kura. Hebu atwambie ni mambo gani ambayo Mdee au Mbunge yeyote wa Chadema aliyafanya ili kuizuia Serikali kupeleka maendeleo katika majimbo yenye Wabunge wa Chadema. Je, Serikali baada ya kuzuiliwa na Mdee kupeleka maendeleo Chadema au katika jimbo lolote la Wabunge wa Chadema ilichukua hatua gani katika kuwataarifu Wananchi wa Kawe au jimbo husika kwamba tulitaka kuwaletea maendeleo ya hiki au kile lakini Mbunge wenu KATUZUIA?
Katika mkutano wa kampeni unaoendelea hapo Kawe, mgombea wa Ubunge wa Kawe kupitia CCM, Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Josephat Gwajima amesema jambo fulani la kushangaza.

Namnukuu “Rais Magufuli umenishangaza kwenye mambo uliyofanya Kawe hali ukijua ilikuwa ni jimbo la chama cha upinzani.

Pamoja na kwamba ilikuwa ngumu kuwaletea maendeleo watu wa Kawe kutokana na vizuizi ulivyowekewa na Mbunge aliyekuwepo, ulitafuta njia mbadala ya kuwafikishia maendeleo


Hivi hilo linawezekana? Yaani Serikali iamue kufanya jambo fulani halafu Mbunge aweke kizuizi?
 
Ndio mana Mimi huwa siendi makanisani, maana ni kwenda kubeba dhambi za waovu kama kina gwajiboy,ni bora ushinde bar utaiingizia nchi mapato kuliko huko kwa wanaojiita watumishi
Gwajima hana kosa wajameni hata rais mwenyewe kasema Halima alimzuia kutoa sehemu ya ardhi kwaajili ya wananchi wa Kawe hata kushindwa kutoa mikopo kwa kina mama, vile vile mafuriko ya jana Kawe yalitokana na Halima kutowajibika kama mbunge.
Sasa hapo unategemea Gwajiboy ataongea kitu gani?
 
Nadhani Gwaji naye ni Majnun/Saa Mbovu (in Majuto's Voice)! Ujenzi gani wa hoja huo? Ataweza kujenga hoja Bungen kweli Kwa ushawish wa kitoto kama huu??
Hukumbuki tamko la Ndugai kuhusu uwezo wa mbunge anaeitajika na ccm?
 
Kabadili gia angani, ameona mavuno kwa waumini wake hayamtoshi!

Screenshot_20200927-131729_1602708012471.jpg
 
Kwani pale JPm anapotaka bajeti yake ipitishwe bungeni ili ikafanye kazi majimboni alafu Mdee anakataa kuipitisha huoni hapo ni kizuizi?
Na wewe unaamini kabisa kwa dhati kuwa mbunge mmoja wa upinzani alizikosesha bajeti kupita?
 
Back
Top Bottom