Gunia la mahindi linauzwa lakimoja au kuna njaa?

eddy

JF-Expert Member
Dec 26, 2007
15,108
10,080
Leo nimestuka kusikia maeneo ya kanda ya ziwa kunia la mahindi linauzwa hadi lakimoja, sasa kuna njaa au ndo mambo ya kuwakirimu jirani zetu na wale wenye matatizo na mabeberu?
 
Kama ni Shinyanga kawaida tu sababu huko wanalima sana Mpunga halafu kuna tabianchi ya nusu jangwa
 
mbona mwaka huu ukame ulitawala sana,Morogoro,mfuko wa sembe kg 25,unauzwa hadi sh.27,000|=Debbie1 moja linauzwa 13,000=zidisha ×6
 
Mwaka jana tulilalamika kwa nn bei ndogo, mwaka huu tunalalamika kwa nn bei kubwa! Magu kazi anayo

Mwaka jana tulilalamika kwa nn bei ndogo, mwaka huu tunalalamika kwa nn bei kubwa! Magu kazi anayo

Watu hawaeleweki, hamtaki mkulima aneemeke.... lifike japo laki mbili.

Takwimu zinaonesha tuna ziada ya chakula, na tutaziuzia nchi jirani.... endeleeni kulialia.
 
Mwaka jana tulilalamika kwa nn bei ndogo, mwaka huu tunalalamika kwa nn bei kubwa! Magu kazi anayo

Mimi sishangai sana bei kushuka na kupanda najua hizo ni kanunj za soko...law of demand and supply.....Mimi nachojialamu kwanini tunashindwa kutumia hizi boom and basts kujitajirisha?....ndani ya miezi nane iliyopita tu gunia lilikuwa elfu 20 leo ni laki,ni ongezeko la zaidi ya % 300 ya bei ya mwanzo....kwanini tunashindwa kutumia this opportunities to gain financial success?
 
Kama ikiwa ni bei inayotoka kwa mkulima moja kwa moja basi itakuwa ni jambo jema angalau wakulima nao waneememke. Lakini ikiwa ni bei ya wanyanyabiashara wao wamenunua kutoka kwa wakulima kwa bei ya kutupwa basi hii itakuwa sio habari njema kwa walaji na wakulima.
 
Hali halisi kwa mwaka huu maeneo meng yamekumbwa na ukame kama meoneo kanda ya kat, hivyo kuna uhaba wa chakula hali iliyopelekea bei ya mahind kupanda,kwa ufupi kuna njaaa.
 
Kama ikiwa ni bei inayotoka kwa mkulima moja kwa moja basi itakuwa ni jambo jema angalau wakulima nao waneememke. Lakini ikiwa ni bei ya wanyanyabiashara wao wamenunua kutoka kwa wakulima kwa bei ya kutupwa basi hii itakuwa sio habari njema kwa walaji na wakulima.
Sio kila mtu anaweza kujadili kuhusu biashara.

Hilo gunia linasafirishwa bure toka Sumbawanga, Katavi kwenda kanda ya ziwa?

Gharama za kupakia, kushusha, ulinzi, na chakula na malazi ya mnunuzi akiwa huko ugenini kukusanya mahindi umehesabia?

Ushuru wa mazao kama mzigo umezidi tani 1 usisahau pia.
 
Kama hujawahi kulima hata pilipili hoho hautaelewa nilichokiandika.
 
Ndo hulka yetu binaadmu llikuzwa laki tayari maneno likipungua bei kuuzwa elfu 20 watakuja wengine kusema....
 
wacha yapande ili wakulima na wao wawe na uhakika wa kushinda kesi mahakamani kama wafugaji wanavyojidai.
kikawaida kwa shule zetu kilo moja ya sembe huliwa na watu wanne kwaama kilo kitoweo cha nusu kilo.
hivyo kwa hesabu hizo ilitakiwa unga ukiwa kilo 1000 basi nyama kilo 2000
 
Mwaka jana tulilalamika kwa nn bei ndogo, mwaka huu tunalalamika kwa nn bei kubwa! Magu kazi anayo

Hatuna jema
 
Back
Top Bottom