Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 6,132
- 10,514
Mahakama moja nchini Guinea ya Ikweta imemhukumu kifungo cha miaka 8 gerezani aliyekuwa afisa mwandamizi wa serikali ya nchi hiyo Baltasar Ebang Engonga kwa makosa ya ubadhirifu wa fedha za umma.
Bwana Engonga aliutikisa mtandao wa intaneti mwaka jana kwa sifa chafu baada ya kuvuja kwa mamia ya video za ngono zilizopatikana kwenye vifaa vyake vya kielektroniki vilivyokamatwa wakati wa uchunguzi wa makosa ya matumizi mabaya ya fedha za umma. Baadhi ya waliokuwamo kwenye video hizo walikuwa wake wa maafisa wengine wa serikali. Mbali ya kifungo cha miaka 8, Baltasar ametakiwa pia kulipa faini ya dola 220,000.