Kwa nnavyoelewa mimi neno ''gubu'' hua linatumika kuongelea ile hali ya mtu kukumbushia makosa au kutosahau kwa maana nyingine.Wanaosemwa kwa kua na gubu mara nyingi ni wanawake.Wanaume hawachoki kabisa kuongelea ni kiasi gani hawapendelei/hawafurahishwi na hii tabia.
Binafsi sipendi hilo neno kwasababu halitendei haki watu wanaokosewa kila mara alafu akijaribu kukuonyesha kwamba hata jana ulifanya vile vile unaanza kukwambia ana gubu!!!Kama ambavyo unapomuomba mtu msamaha unategemea na unataka kusamehewa ndivyo ambavyo na wewe unatakiwa usirudie makosa.Ukikosa tena unaomba msamaha na unayemwomba ana haki ya kukuonyesha ni jinsi gani unaabuse msamaha anaokupa kila mara.
Ni kweli kwamba binadamu hatujakamilika ndo maana tunakosa na kukosa tena na tena....kwa hayo hayo mapungufu ndo inashindikana kusahau kabisa yaliyopita na kukumbushana mara kwa mara.
Naamini kwamba jana inajenga leo....ulichokosea jana unajifunza ili usirudie tena leo....ulichofanya jana kama ni kizuri kinafanikisha furaha ya leo nk.Hata swala la mafanikio....ukikumbuka kitu kilichokuangusha jana ni rahisi zaidi kukikwepa mbeleni kwahiyo watu wakubali kusemwa na kukumbushwa pale inapobidi maana safari ya mabadiliko ndivyo inavyoanza...KWA KUKUMBUKA!!!!
Ila katika kila kitu kunahitajika kiasi.Don't exaggerate things....kidogo acha kibaki kua kidogo!!!
Tatizo unaweza ukamsamehe mtu leo halafu kesho au kesho kutwa akarudi kosa hilo hilo akijua tu kwamba akija kwako akikuomba msamaha utamsamehe
Hatujakamilika ndo maana sisi ni wanadamu na sio Mungu!Tukianza kusema kila kitu kama Mungu ange...hiki au kile nadhani hamna ambae angepña huo mchanganuo!Huwezi kua mtu wa kukosea wengine kila siku alafu uchukie kuonyeshwa ulivyo!finest kama Mungu asingekuwa anakusamehe ww ungekuwa hapo ulipo?? akikukosea msamehe tu lkn usianze kukumbushia mambo ya juzi ooh ulifanya jana ukafanya leo tena umerudia!
i hate, i hate wanaume wenye gubu heri nibakie single hivi hivi!!
Sijakataa Susy Je? Leo mumeo akikuletea mwanamke ndani ya nyumba yenu utamsamehe kwa vile Mungu kasema tusamehe, tunaangalia makosa ya kusamehe sio kusamehe kwa kuwa Mungu kasema tusamehe unaweza kujikuta unasemehe mtu halafu wewe ndio unaingia kwenye matatizofinest kama Mungu asingekuwa anakusamehe ww ungekuwa hapo ulipo?? akikukosea msamehe tu lkn usianze kukumbushia mambo ya juzi ooh ulifanya jana ukafanya leo tena umerudia!!!
i hate, i hate wanaume wenye gubu heri nibakie single hivi hivi!!!!