GSM waliishusha Majimaji FC daraja 2017

nzagambadume

JF-Expert Member
Apr 9, 2018
2,430
5,769
Matapeli ya GSM baada ya kuitaka simba 2015 yakashindwana yalihamia Majimaji yalikuwa yakihaha kufunika uozo wao wa home shopping centre maana baada ya kudhamini kipindi cha ze comedy TBC waliona haitoshi soka ndipo kwa kuoshea jina

Sasa leo lopolopo kijana la mzee tozi linatupigia kelele kwamba tajiri wa GSM ndiye mtu wa maana kwenye mpira. Pumbavu wewe mtoto m little, Yaani mo ambaye uncle wake Mo Dewji kaifikisha simba fainali simba ya afrika 1993 utalinganisha na hao wapiga deal? Si bora ningesikia mtoto wa Abass Gulamaili yuko hapo utopoloni?

Mo aliyeitoa Zamalek 2003 akaipokea kwa bashasha na kuvua hadi shati leo akivua shati unalinganisha na wajinga walioshusha majimaji daraja?Wachumia tumbo wanaingia kwenye mpira ku cover their tracks?

Mo Dewji is real anaipenda simba anaupenda mpira haswaaa we lopolopo kijana wa mzee tozi kilichobaki kamtafute boss wa assas upige naye picha na kuturingia kwamba niko na boss asiyevua shati, unataka wavue shati ili iweje ndiyo unakuwa aroused au? Dunderhead msukule wa ajabu kabisa

=============

GSM YABORESHA MASLAHI YA WACHEZAJI MAJI MAJI ISISHUKE DARAJA


Na Princess Asia, DAR ES SALAAM

KAMPUNI ya GSM imesema kwamba imeboresha maslahi ya wachezaji wa Maji Maji FC ya Songea mkoani Ruvuma ili kuwahamasisha washinde mechi zote zilizosalia za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na kuepuka kushuka Daraja.

Akizungumza na Bin Zubeiry Sports – Online jana mjini Dar es Salaam, Mkuu wa Uwekezaji wa GSM, ambao ni wafadhili wa Maji Maji, Hersi Said (pichani juu) amesema kwamba watahakikisha wanaibakiza Ligi Kuu timu hiyo.

“Tumekwishafanya mazungumzo na Mkuu wa Mkoa, Chama cha Soka na wadau wakubwa wa Songea na wote wanataka Maji Maji inaki Ligi Kuu. Kwa hivyo tumeweka mkakati mzuri kuhakikisha tunashinda mechi zote timu ibaki Ligi Kuu,”alisema Hersi Said.

Katika kuhakikisha mpango unafanikiwa, uongozi wa Maji Maji umeanza kuwashughulikia wachezaji wativu wa nidhamu baada ya kuwasimamisha wanne, George Mpole, Peter Joseph, Yussuf Mfanyaje na Ibrahim Tende mapema wiki hii.

Mwenyekiti wa Wana Lizombe hao, Humphrey Milanzi alisema kwamba wachezaji hao wamefanya utovu wa nidhamu ambao klabu haiwezi kuuvumilia na ili liwe fundisho kwa wachezaji wengine, uongozi umeamua kuwasimamisha.

Aidha, Milanzi alisema kwamba kwa sasa uongozi unajikita katika jitihada za kuhakikisha unainusuru timu kushuka Daraja kwa kuhakikisha timu inashinda mechi zake zote saba zilizosalia za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

Maji Maji kwa sasa inashika nafasi ya pili kutoka mwisho katika msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na pointi 22 baada ya kucheza mechi 24, juu ya JKT Ruvu inayoshika mkia kwa pointi zake 20 za mechi 24 pia.
 
Utateseka sana mwaka huu! Tapeli wenu Mo mpaka anaondoka makolokolo wote mtakuwa mmeshachanganyikiwa.
 
Basi na Yanga wanashuka daraja msimu huu
Kwani wewe unasemaje ndugu mwandishi?
 
Hahaha tumekwisha sahau habari ya Mo kuikacha Afrika Lyoni kipind iko daraja la pili. Si afadhali GSM aliweza kuihudumia timu ya ligi kuu .

Mo timu ya daraja la pili ilimshinda ndio maana akaamua kuja simba ili abandike matangazo ya sabuni kwenye jezi za simba.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom