'Green Guards' kutovaa sare!

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,007
Inapendekezwa kuwa wale 'Vijana Wakakamavu Wajasiriamali wa CCM' almaarufu kama Green Guards wasivae tena sare zao zinazofanana na zile za Jeshi la Polisi. Mapendekezo hayo yanatoka katika Kitengo cha Propaganda cha CCM Ofisi Ndogo za Lumumba,Dar es Salaam.

Mapendekezo hayo yanafuatia kikao cha kitengo hicho kilichofanyika jioni ya leo. Pia,inapendekezwa kuwa Green Guards wasiwe wanapiga 'salute' kama ile ya majeshi kuanzia sasa badala yake aina mpya ya salamu itatumika.Lakini,bado aina hiyo mpya ya salamu haijaainishwa.

Lengo hasa la mapendekezo hayo ni kuuaminisha umma kuwa CCM haina na haijawahi kuwa na kikundi/kikosi cha ulinzi wa chama na hivyo kuchagiza mapambano dhidi ya CHADEMA waliodhamiria kuimarisha Red Brigade. Mapendekezo hayo yatapelekwa katika ngazi za juu ili kuweza kuamuliwa zaidi na kufanyiwa kazi pale ambapo yatapitishwa. JF itajua juu ya hilo pia.

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
 
Tulianza na mungu
Tutamaliza na mungu 2015.

Watanzania wa sasa wanajua kila kitu, acha waangaike tu, mwisho wao ni 2015 kwani "mchawi wa yote ni serikari by dr slaa jana nkuruma"
 
saa nyingine utaamini MACCM ni matahira kwani hao magreen guard wanaishi mbinguni si wanaishi pamoja na wananchi na wanafahamu kila kitu wanachokifanya ,CCM ya KIkwete haishi vituko
 
CCM wanadhani maovu yao hayaonekani na watu hawajui!
 


:A S-key: mzee tupa tupa wananchi tayari wliishaanza kuchukua ufunguo wao wa ikulu kama vile!
:A S-fire1: hii kitu itawawakia tu hata waje na mbinu gani kwani hao wanaoitwa wananchi hawana macho na walikuwa hawaoni?
 
Kwa kweli duniani kuna mengi, ila 80% ya matukio vya ajabu vinapatikana tanzania kwetu tu
 
Tulianza na mungu
Tutamaliza na mungu 2015.

Watanzania wa sasa wanajua kila kitu, acha waangaike tu, mwisho wao ni 2015 kwani "mchawi wa yote ni serikari by dr slaa jana nkuruma"

ulianza na mke wa mtu uta......
 
Je hivi vitu watafuta au kuchoma moto? Maana issue si mavazi na staili ya kusalimia...ni contents...it is the content that counts.

Wameweka hadi kwenye sera za msingi za chama chao! Watamdanganya nani? Fooling themselves around, ndiyo uwezo wao ulipofikia.
 
Nyie ccm endeleeni kukaza buti kunawatu lazima wafe kwa presha mwaka huu,mfano slaa kaisha sana kabakiza makovu tu ndiyo masalia yetu.
 
ubaya wa watendaji wa CCM huwa waapanga jambo bila kufikiria mengineyo.
Alichosema Makene kinanipa wasiwasi na upeo wa hao watu wa CCM
mkipanga plan A je mnaangalia na plan B?
kwa upungufu huo chadema njia nyeupeee kisiasa.
 
Waambie ni kheri wangeendelea kuwafundisha ukakamavu kwakuwa red brigade inakuja kwa nguvu zote na hakutakuwa swalia mtume tutawashughulikia kisawasawa pale tu watakapothubutu kuingilia shughuli zetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…