Great thinkers mawazo yenu yanahitajika hapa.

Great thinkers mawazo yenu yanahitajika hapa.

Mtoa mada umeuliza swali zuri japo mifano yako haihusiani na jambo ulilouliza. Katika mifano yako umetaja mboni ya jicho na kutoa mate ambazo ni reflex actions. Reflex actions nyingine ni kama kupiga chafya na kujikuna unapowashwa. Hayo ni matendo ambayo mwanadamu anayafanya bila kufikiria. Na yanaongozwa na central nervous system. Sidhani kama kuna kiumbe yoyote anayeweza kufikiria kuwa sasa nipige chafya. Ila inatokea pale mfumo wa hewa unapojisafisha. Kwa maelezo hayo basi tukirudi kwenye swali lako ni kwamba matukio kama kufukuzwa kazi au tukio lolote la kuitikia kichokoo linaongozwa na ubongo. Hivyo ni kweli kabisa kama utakuwa na uelewa wa kutokukurupuka katika kufanya maamuzi basi itakuwa rahisi kwako kuweza kufanya maamuzi ya busara bila kujidhuru wala kuathiri afya yako. Binadamu tumepewa akili na utashi. Na huo ndio hutuongoza katika mambo yote yanayotumia akili. Kikubwa katika yote ni kujua jinsi ya kukontrol mapigo ya moyo wako. Hili ni somo jingine. Namalizia kwa kusema Fikiri kabla ya kutenda.

Nilipotoa mifano ya reflex action nilikuwa nina maana yangu. Maana yangu nikuwa God/nature is correct to create us with those reflex action because they are there to help us. Sasa kama hayo ni sahihi, iweje tujaribu kukinzana na ku-PANIC?
 
Umemaliza. Umenikumbusha somo ls Biology. Ningekua na like nyingine ningekupapo.
 
Nilipotoa mifano ya reflex action nilikuwa nina maana yangu. Maana yangu nikuwa God/nature is correct to create us with those reflex action because they are there to help us. Sasa kama hayo ni sahihi, iweje tujaribu kukinzana na ku-PANIC?
You can control PANIC kama ilivyo kucontrol hasira. Ufunze ubongo wako kuto react negatively kwa vitu vilivyo nje ya uwezo wako. Panic is not reflex action ni tabia ya mtu huundwa na mtu. Na ndo maana mtoto mdogo hawezi kupanic zaidi ya kushtuka ambayo ni nature. Panic ni zaidi ya mshutuko yani una utreat ubongo kufanya ilichukulie lile tukio ni kubwa sana na kuhamaki kuliko pitiliza.
 
Naona wadau wana subiri lkn ngoja mi ni-test kama sio kutoa wazo langu.
Ni kweli wkt mwingine ni vigumu kuzuia hisia kama ukiwa na mhamako (nikimaanisha kuhamaki sana) mkubwa lkn kuna mambo kadha wa kadha mtu anaweza kufanya hata kama ni kwa kujilazimisha ili mhamako huo usilete madhara yoyote. Kubwa ambalo mimi hulifanya ni kujizuia kwa nguvu zote kufanya maamuzi wakati nina hasira. Hii imenisaidia kuepuka mengi sana katika life yangu.. so kwa kujaribu wakuu just chukua hiki kiji point.. USIFANYE MAAMUZI PALE UNAPIKUWA MWENYE HASIRA

Umeshauri kile kile ambacho wengi wanashauri ila hujajibu maswali yaliyoulizwa mkuu. By the way siyo kwamba nimehamaki kwahiyo ninahitaji ushauri kwa hilo. Hapana mkuu.
 
Mkimaliza hilo mnisaidie pia kujua kwa nini mtu mwenye homa kali(hasa itokanayo na malaria) uhisi baridi kali, wakati ukipima joto lake la mwili liko 40 degree Celcius kasoro? Asanteni.
 
Ufunze ubongo wako kuto react negatively kwa vitu vilivyo nje ya uwezo wako.
-Bila kuwa'mzuka' hii kitu ngumu!!
===
Najaribu kuona uko mtoni unaogelea mara unamuona pande la mamba linakunyemelea...unakimbia kuelekea nchi kavu unaona simba wawili wamelalia nguo zako na chui wanne...wote wanasogelea pale unapotaka kutokea majini...!! (yaani nawaza tu namana ya kutokureact negatively)
 
Kuna maoni yanayochukua kukubalika kwa sana sasa katika nyanja za saikolojia kwamba, ni vizuri watu kuachia hisia zao.

Kwa mfano, habari za kwamba wanaume ni shupavu na hawatakiwi kulia, angalau hadharani, zinapingwa, na wanasaikolojia wanasemakwamba mtu akijisikia kulia, halafu akajizuia kulia, hilo linamfanya akosekutoa hisia zake na atazikusanya zikae ndanikwa namna ambayo inaweza kumletea madhara baadaye.Kuna ushahidi wa kisayansi ya kikemikali unaoonesha kwamba matendo kama kulia huwa yanaendana na kuachilia kemikali fulani ubongoni, mwilini, na hivyo, kama mtu anajisikia kulia na asipolia, anawezakuwa anazifungia kemikalihizi asizitoe.

Mimi binafsi hupenda kuangaliamambo kimantiki, na kwenye vitu kama misiba, nakuwa mgumu kulia. Kwa kitambo sasa, nimejifunza kutohuzunika sana mambo yanavyokwenda kinyume na ninavyotaka, na pia kutofurahia sana mambo yanavyokwenda vizuri sana, nafikiri falsafa za ki Buddha nilizosoma, zinazoelezea umuhimu wa kuwa na equanimity (kuchukulia mambo yote kwa usawa wa mawazobila kuhamanika au kufurahi sana) zimenisaidia sana kuwa hivyo.

Pia, mimihujiona kamamtu wa kusaidia, kwa mfano, sehemu kama msibani, mimi hujiona kama askari ambaye atadaka wale wanaolia na kuanguka, sasa askari mimi tena nikilia, watu wakilia na kuanguka nani atawadaka? Muda wote nakuwa busy kuangalia logistics,kuna chakula? kuna vinywaji? Kuna viti? Nini kinahitajikakufanyika? Mipango inaendaje? Nani anahitaji msaada? Watu muhimu wana habari? Wazee wanaohitaji kusaidiwa wamesaidiwa? Watoto wataendanaje na mazingira haya? Habari za usafiri zimetengemaa? Kuna hatari ya mifarakano? Kama zipo, usuluhishi na uzuizi unaweza kugfanyaje? Kuna wanaotaka kupiga picha? Hilohalitaleta mtafaruku? Kuna mgongano wa kitamaduni?Pombe itanyweka? Walokole watasemaje? Waislamu watakula chakula kilicho halal? Maji yakosalama?

Yani kwenye msiba akili inaenda spidi ya mwanga hivyo, hata kulia nasahau.

Nitakuja kulia peke yangu wiki mojabaadaye, mwaka mmoja baadaye, au hata miaka ishirini baadaye.

Nikimkumbuka mtu peke yangu.
Vipi kuhusu hayo maswali matatu yaliyoulizwa kwenye original post?
 
-Bila kuwa'mzuka' hii kitu ngumu!!
===
Najaribu kuona uko mtoni unaogelea mara unamuona pande la mamba linakunyemelea...unakimbia kuelekea nchi kavu unaona simba wawili wamelalia nguo zako na chui wanne...wote wanasogelea pale unapotaka kutokea majini...!! (yaani nawaza tu namana ya kutokureact negatively)
Umefikiria mbali hahahaaaa hapo mwili utafanya kazi wenyewe kwa kupitia tezi yake ya Adrenaline ambayo hutumika kwenye kipindi cha hatari kama hicho inatoa vichocheo either nguvu zitaongezeka na ubongo utafnya maamuzi either ukimbie au la. Kutokua negatively labda inasound vibaya ila uufanye ubongo usikate tamaa
 
You can control PANIC kama ilivyo kucontrol hasira. Ufunze ubongo wako kuto react negatively kwa vitu vilivyo nje ya uwezo wako. Panic is not reflex action ni tabia ya mtu huundwa na mtu. Na ndo maana mtoto mdogo hawezi kupanic zaidi ya kushtuka ambayo ni nature. Panic ni zaidi ya mshutuko yani una utreat ubongo kufanya ilichukulie lile tukio ni kubwa sana na kuhamaki kuliko pitiliza.
Let's say kuwa uko sahihi kuwa mtoto ha-panic bali anashituka.
Now, naamini kuwa utakubaliana na mimi kuwa mtoto atashituka kutokana na kitu kuwa a bit intense beyond normal na hivyo nature iko sahihi kufanya mtoto ashituke. Sawa swali linarudi pale pale, kwanini huko kwenye reflex action na kwa mtoto kushituka nature iwe correct lakini kwenye ku-panic tuone si sawa na kujaribu kukinzana na paic kwa ku-calm down? Kwanini tusiache panic iendelee mpaka itakapoisha yenyewe?
 
Mkimaliza hilo mnisaidie pia kujua kwa nini mtu mwenye homa kali(hasa itokanayo na malaria) uhisi baridi kali, wakati ukipima joto lake la mwili liko 40 degree Celcius kasoro? Asanteni.

Mgonjwa atasikia baridi kwa kuwa mazingira yanayomzunguka ni ya baridi kuliko mwili wake.
 
-Bila kuwa'mzuka' hii kitu ngumu!!
===
Najaribu kuona uko mtoni unaogelea mara unamuona pande la mamba linakunyemelea...unakimbia kuelekea nchi kavu unaona simba wawili wamelalia nguo zako na chui wanne...wote wanasogelea pale unapotaka kutokea majini...!! (yaani nawaza tu namana ya kutokureact negatively)
Scenario nzuri sana hii. Na hii inaweza kutuonesha kuwa the nature might be right to make us PANIC.
 
Hata msibani mtu anapokuwa analia sana inashauliwa aachwe asibembelezwe,
Kwani hiyo ni njia ambayo mwili una response kupunguza maumivu moyoni
 
Umefikiria mbali hahahaaaa hapo mwili utafanya kazi wenyewe kwa kupitia tezi yake ya Adrenaline ambayo hutumika kwenye kipindi cha hatari kama hicho inatoa vichocheo either nguvu zitaongezeka na ubongo utafnya maamuzi either ukimbie au la. Kutokua negatively labda inasound vibaya ila uufanye ubongo usikate tamaa
So the nature is right in this case.
 
Unapomwambia mtu calm down,easy,chukulia poa n.k unamtoa mtu kwenye hatari ya kuudhuru mwili wake,binadamu anapokuwa kwenye state ya uchungu kwa muda mrefu organs za mwili wake zinadhurika,mf.Moyo,Figo,Maini n.k.kwani unapokuwa kwenye hizo hali vitu hivyo hufanya kazi ya ziada,na hiyo kazi ya ziada inapodumu muda mrefu vinaanza kuumia,ni taratibu lakini hatimaye utaishia kuumwa na hatimaye kufa.Kwa sisi wakristo kwenye Biblia Mithali 4:23 inasema,Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo,maana ndiko zitokako chemichemi za uzima.Kwahiyo pamoja na kwamba tunakutana na mambo yanayoumiza hatutakiwi kuyaacha yaendelee kutuumiza kwakuwa tu mwili umeumbwa ili upambane navyo,kinachotakiwa hizo hali zikishatokea tufarijiane na sisi wenyewe tujitahidi tuwezavyo kujisahaulisha ili maisha yaendelee...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kila gari ina shock absorbers au shock ups mzigo ukiwa mzito kuzidi shock ups ni hatari huvunjilka Na kuleta madhara makubwa kwa gari.Binadamu pia ana shock ups shock ikiwa kubwa kuliko shock ups aweza kufa kwa pressure au kapata maradhi ya kupasuka mishipa ya fahamu akapooza .Hivyo watu wakiona kama kazidiwa ndio humsihi a cool down asije pata matatizo yeye binafsi akaleta shida kwa watu wengine kama waliokuwa wakimtegemea au akaleta shida kwa wengine watakaohangaika kumuuguza badala ya kuendelea Na shughuli zao zingine za kiuchumi.Mwenye uwezo mkubwa wa shock absorbers huwezi ona watu wanamsihi kuwa calm down.
 
Back
Top Bottom