Govt slams UN report on Arms Trafficking; demands apology

Kuwa mzalendo si kutetea uovu. Hata kama serikali haikuhusika moja kwa moja, kuna watu waliokuwa/wenye ngazi za juu serikalini waliohusika. Membe angesema tu kuwa haikuwa sera ya serikali kuwapa silaha wapinzani na kwamba itapeleleza shutuma hizo angekuwa more diplomatic. Lakini kwa kukanusha kwa lugha kali ni kama amemwaga mafuta kwenye moto.
 
Kuwa mzalendo si kutetea uovu. Hata kama serikali haikuhusika moja kwa moja, kuna watu waliokuwa/wenye ngazi za juu serikalini waliohusika. Membe angesema tu kuwa haikuwa sera ya serikali kuwapa silaha wapinzani na kwamba itapeleleza shutuma hizo angekuwa more diplomatic. Lakini kwa kukanusha kwa lugha kali ni kama amemwaga mafuta kwenye moto.

Jasusi,

Shakespeare katika Hamlet kwa kupitia Malkia Getrude alituhusia kwamba mtu akikanusha kwa nguvu kubwa kuliko zinazotakiwa ujue allegations zimegusa mfupa.

Queen

The lady doth protest too much, methinks.

Hamlet Act 3, scene 2, 222–230

I say Membe doth protest too much, therefore, there must be a grain of truth in the allegations.

At least this is what dumb dumb makes it appear to be.
 
duh!

Nakumbuka issue ya dili ya vitambulisho Membe alikuja juu na ikabidi ASSA MWAMBENE aje humu kumtetea

na wakawa wanapokezana na BALILE sasa sijui wamepotelea wapi...
 
its a big issue here, i wondre if thid report is true or not but what i think, is not true these reporters do not know very well about tanzanian, our country is THE ISLAND OF PEACE we cannot do that.
Mawazo Mgando kama haya ndio yanawafanya Mafisadi wazidi kuimaliza Tanzania huku wananchi wenyewe wakiwa wanakenua midomo na kuwapigia makofi. Yaani inatia aibu kuona baadhi yetu wana ukomo wa akili na fikra mithili ya udogo wa sisimizi. Jamani hebu tokeni kwenye usingizi mzito mithili ya Pono ndani ya bahari, kuizuia akili yako kuwa na akili kuna madhara makubwa kuliko hata upungufu wa chembechembe za kinga mwilini kwa mgonjwa mahututi wa ukimwi.
 
Mmarekani ndo anaeongoza kutibua Africa, hususan DRC. na USA ni rafiki mkubwa wa Tanzania kwa sasa, siajabu anapitisha silaha zake kupitia Tanzania. Kama USA kasema ni ngum sana ku resist hata kiongozi wa nchi angekua nani. Tatizo ni njaa tunashindwa kuwagomea kupitisha silaha zao, tukiogopa kunyimwa misaasa. kiukweli hamna nchi za Africa apart from Libya, Tunisia na Morrocco zinazoweza kukataa maombi ya USA.

naweza kusema WW2 imeweka hiyo hali, ya USA kuwa kiranja wadunia, hata akiwa kiongozi gani TZ, Obama akimwambia wanataka kupitisha silaha TZ kwenda kongo, hamna Rais wa TZ atakaekataa.
 
Urging Member States, particularly those in the Great Lakes region, to submit implementation reports in
connection with paragraph 7 of resolution 1857 (2008). The Group notes in this regard that at the time of
writing, only 15 Member States had submitted such reports.


Just a glimpse of the report bwana membe needs to answer constructively na sio kukurupuka tu inatilisha aibu kwa Tanzania
 
Mjadala huu umekosa uzalendo kwa kiasi kikubwa na wengi wenu mko tayari kuamini wachonganisha wa kimataifa na kuliacha Taifa lenu kwenye matatizo makubwa...this is nonsense na kila mwenye harufu ya uzalendo lazima ajitahidi kuipinga .

Kama uzalendo wenyewe ndio huu wa kutetea madudu yaliyo wazi then sijui tunajenga taifa la aina gani. Nenda katafute article ya Allafrica.com At the other end of the pipe wametoa background nzuri ya biashara ya "samaki" na jinsi silaha zilivyokuwa zinapitishwa Mwanza.
 
Uzalendo utakuja akina chenge wakitueleza utajiri wao wameupata wapi? Uzalendo utakuja ikiwa akina diria watatueleza wamepata wapi utajiri wao. na wengineo wengi usitake kutuletea unafikia wa kutupaka mafuta wakati chini unatuungaza na moto. Ukweli ni kwamba dili kama hizi ziliachwa na baba wa taifa wakachukua wajanja wakiwa pamoja na wahindi fulani wajitajirishe kwa utajiri wa haraka huku tukidanganywa kama majinga??? Hakuna uzalendo karne hii kama hamna haki kaka!!!
 
Baba wa taifa alifanya kwa uzalendo wa kuikomboa Afrika dhidi ya ukoloni. Sasa akina akina Crown Jewelery wanamkomboa akina nani??? msituchafue kichwa hapa
 
hakuna cha apology wala nini; tulishaandika haya miaka imepita. kama wanataka apology watuambie kwamba Meremeta ni aje?
Mzee Mwanakijiji; with due respect, I beg to differ.

Siyo kila mTanzania anpofanya bishara ya contraband maanake serikali imerithia, na makosa ya watu mmojammoja isiwe sababu ya kutufanya wote tutukanwe mbele ya jumuia ya kimataifa.

Ungejua unyama wanoufanya hao FDLR mashariki ya Congo usingeshabikia Tanzania kuhusishawa na uppuzi kama huu. Au tuseme Ghailani alipowasaidia akina Osama kupiga ubalozi pale Dar ni serikali ya Tanzania iliyotuhumiwa?

Jamani hata kama ni upinzani, tafuteni issues za kuibana serikali, hamuisaidii Tanzania kuungana na watu wa nje kushabikia fedheha kama hii.
 
Sasa hivi Balozi Mahiga alikuwa anazungumza na BBC. Anaeleza bado kuna majadiliano juu ya hiyo ripoti na kikao rasmi ktk UN kuijadili ripoti itakuwa ni tarehe 16 Dec.

Itakuwaje kama itakuwa imethibitishwa kwamba yote ni kweli? hawa wenye papala ya kukataa ktk hii inayoitwa serikali yetu, watasemaje?

Itachukuwa muda mrefu sana kupata watu wenye akili timamu ktk siasa zetu.
 
Wahesimiwa nimeiona ile barua majira ya asubuhi ila saa hizi siioni imekuwaje tena wadungu wapenzi. Aidha barua hiyo ilikuwa peke yake bila makandokando (appendices) yake. Mzee Mwanakijiji alitupatiaa riporti hiyo basi muung'wana wingine atupatie makandokando hayo
 
Out of point, meremata inahusikaje hapa..watu mliokosa uzalendo kama nyinyi hamna maana kabisa shame on
Uzalendo utoke wapi hivi hii serikali tuliyo nayo inashindwa nini kufanya kwenye michezo michafu kama hata jeshi linauziwa helicopter, silaha, malori mabovu? Na tunajuaje kama hiyo miradi wanayoiita ya Jeshi kama Meremeta ilijumuisha silaha pia?

Jamani tuamkeni! UN wametoa vidhibitisho juu ya ripoti yao ikiwa kudakwa kwa mazungumzo kati ya waasi na wakubwa jeshini! Nyie kalaghabao endeleeni kulala wakina Vithalini wanauza mpk silaha kupitia hiyo bandari yenu ya salama! Amkeni na muache ushabiki usio na mipaka kwa kisingizio cha uzalendo huo ni upuuzi sasa!
 
Back
Top Bottom