Gosbert Blandes acha kutudhalilisha Karagwe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Gosbert Blandes acha kutudhalilisha Karagwe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kigoma 2015, Nov 16, 2011.

 1. K

  Kigoma 2015 JF-Expert Member

  #1
  Nov 16, 2011
  Joined: Sep 19, 2011
  Messages: 366
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Blandes MP heshima kwako,

  Mimi naishi ktk kijiji cha NYAKAKIKA, tarafa ya NYABIONZA ktk jimbo la KARAGWE.

  Naomba nisimame kwa niaba ya wananchi wa kata, tarafa pia Jimbo langu kua hayo uliyoyazungumza leo bungeni ni ya KWAKO binafsi na CCM yako.

  Ni lini ulipita jimboni kukusanya maoni juu ya rasimu ya katiba? Wacha Uongo na huo ni Unafiki kuwa eti wananchi wako wa KARAGWE wamekutuma, labda familia yako ndo imekutuma.

  Umetudhalilisha sana kuwa sisi hatuna akili kama wewe na CCM yako.

  Naomba kuwaambia wana JF kuwa sisi KARAGWE hatujamtuma kama alivyosema yeye.
   
 2. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #2
  Nov 16, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,903
  Likes Received: 5,365
  Trophy Points: 280
  Heshima mkuu, halafu huyu nasikia alichakachua kura kuliko JK.
   
 3. C

  Campana JF-Expert Member

  #3
  Nov 16, 2011
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 207
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Maswali zaidi kwa Blandes:

  Je ni lini mara ya mwisho ulijionyesha hadharani kule Karagwe mara baada ya uchakachuaji/wizi wa kura? Kule wanakuona kama bundi - ukionekana ni mkosi.

  Inasemekana ulikimbilia Dar baada ya tukio hilo - na kuwa huwa unaenda Krgw kwa siri sana - je ni kweli?

  Huo mkutano wa kupata maoni ya wananchi uliuitisha wapi (kijiji au mtaa) na lini?

  Nawasilisha
   
 4. L

  Lua JF-Expert Member

  #4
  Nov 16, 2011
  Joined: May 19, 2011
  Messages: 704
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  hawa jamaa kama vile wamelongwa!
   
 5. K

  Kigoma 2015 JF-Expert Member

  #5
  Nov 16, 2011
  Joined: Sep 19, 2011
  Messages: 366
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Yaani anadiriki kuwaaminisha watanzania eti wananchi wa Karagwe ndiyo waliomtuma wakati hajawah hata kufanya mkutano ili kuwajulisha wananchi juu ya nini kinachoendelea ktk nch yetu?.

  Ametuaibisha sana wananchi wa Karagwe na asipoangalia hili jimbo anaweza kuliona chungu zaidi ya sasa.

  Shame on you Blandes
   
 6. giraffe

  giraffe JF-Expert Member

  #6
  Nov 16, 2011
  Joined: Jun 6, 2010
  Messages: 504
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 45
  Fabian Masawe zaman dc wa karagwe na sasa ni RC wa kagera ndie alifanikisha uchakachuaji wa matokeo kwa kutumia jesh
   
 7. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #7
  Nov 16, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Hongera mkuu kwa kutujuza. Ndiyo tatizo la wabunge waliochakachua kura. Kumbe alikuwa anawasilisha mawazo kutoka kwenye masaburi yake!!!!!! Magamba bwan!!
   
 8. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #8
  Nov 16, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,782
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Mleta thread amenifanya nitafakari kwa kina zaidi,hivi hawa wabunge wanaotoa povu na mipasho bungeni tuwaulize wamefanya vikao wapi na wananchi wakajua msimamo wa wanananchi wanaowawakilisha? Mheshimiwa Kigwa najua unaingia humu ndani naomba jibu.
   
 9. bullet

  bullet JF-Expert Member

  #9
  Nov 16, 2011
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 959
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Kuna mabo mengine yanamshangaza kila mwenye kufikiri kwa kutumia kwa akili. Juzi madam speaker alisema aliwakataza wabunge kwenda kutafuta mawazo ya wananchi juu ya mswada. Kama nitakumbuka vizuri alisema "niliwazuia kwenda hata ulaya si mikoani tu". Sasa huyu the so called mbunge wa Karagwe alikusanya maoni kwa amri ya nani? Pili kama sikosei Blandes alikuwa kwenye tume ya Jairo muda wote huo. Sasa hayo maoni aliyakusanya lini na wapi? Hakuna sheria ya wapiga kura kum~vote out mbunge anayewasingizia?
   
 10. S

  SEAL Team 6 JF-Expert Member

  #10
  Nov 16, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Fanyeni jambo moja la msingi. Kama kweli ameyasema haya, mwandikieni barua ya kumuita aje jimboni kuwepo na mkutano wa hadhara kisha muulizeni ni lini alikusanya hayo maoni kwa wanakaragwe. Yawezekana alitumia wenyeviti kwa siri bila watu kujua.
   
 11. bullet

  bullet JF-Expert Member

  #11
  Nov 16, 2011
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 959
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Kama aliwatuma wenyeviti kwa siri (siri!!!) basi hayo ni maoni ya wenyeviti na ndio maana labda yakawa confidential! Otherwise, waseme waliitisha mkutano wapi na lini.
   
 12. K

  Kigoma 2015 JF-Expert Member

  #12
  Nov 16, 2011
  Joined: Sep 19, 2011
  Messages: 366
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Umesema la maana sana mkuu, ntafanya mpango wa kuwaona wazee wa Karagwe nipate busara zao halafu tuchukue hatua kama ulivyopendekeza.
  Pamoja sana
   
 13. Alexism

  Alexism JF-Expert Member

  #13
  Nov 16, 2011
  Joined: Aug 14, 2011
  Messages: 2,443
  Likes Received: 1,015
  Trophy Points: 280
  Nina siku kama nne sipati muda wakuangalia Bunge.Wanajamvi nawaombeni kunijuza mbunge Jason Rweikiza BK Vijijini amechangia nini kuhusu katiba.
   
 14. MAGEUZI KWELI

  MAGEUZI KWELI JF-Expert Member

  #14
  Nov 16, 2011
  Joined: Jul 16, 2011
  Messages: 1,943
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 145
  Pepo la wizi wa kura linamsimbua bado...
   
 15. Jeremiah

  Jeremiah JF-Expert Member

  #15
  Nov 16, 2011
  Joined: Feb 17, 2009
  Messages: 642
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Hawa wabunge wa magamba tuwakatae kwa nguvu zote mara watakaporudi majimboni. aibu yao milele
   
 16. Jeremiah

  Jeremiah JF-Expert Member

  #16
  Nov 16, 2011
  Joined: Feb 17, 2009
  Messages: 642
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  sina hakika kama mbunge wangu wa Geita amechangia chochote make naye ni kilaza
   
 17. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #17
  Nov 16, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Poleni sana wananchi wa Karagwe kwani ninafahamu 2010 mlifanya maamuzi ya busara.
  Lakini haki yenu ikaporwa na Kanali Fabian Masswe kwa kushirikiana na jeshi la polisi kuwanyang'anya
  mwakilishi wenu mliokuwa mmemchagua.

  Huyo Blandes anawakilisha maoni ya akina Fabian Masawe na NEC na sio maoni ya wananchi wa Karagwe.
  Msichoke kupigania haki kwani bila katiba mpya kama mlivyo onja wawakilishi wenu wataendelea kuteuliwa
  na DC na NEC kwa usimamizi wa jeshi la Polisi. Blandes hawezi kuthubutu kukanyaga Karagwe anajifurahisha
  tu huko Bungeni, yeye ni mbunge wa Massawe na NEC
   
 18. S

  STIDE JF-Expert Member

  #18
  Nov 16, 2011
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 999
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Mhh! Hata mimi nakuunga mkono, niko mbali na tv na naomba mwenye data atujuze.
  Ila nadhani bado anafikiria jinsi ya kurudisha pesa aliyoonga kabla na kwenye kampeini! Sidhani kama ana jipya, nae ni GHAMBA!! Hawezi dai katiba mpya!!
  Halafu, bkb 'v' tunabadirika lini? "TUNATIA AIBU"
   
 19. Biz2geza

  Biz2geza Senior Member

  #19
  Nov 16, 2011
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 117
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Waataalam wa sheria hakuna namna tunaweza piga kura ya kutokuwa na Imani na wabunge wa magamba?
   
 20. K

  Kigoma 2015 JF-Expert Member

  #20
  Nov 16, 2011
  Joined: Sep 19, 2011
  Messages: 366
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Nimetoka kupokea ujumbe huu toka kwa rafiki yangu
  "hivi nyie watu wa Karagwe ndo mumemtuma huyo Blandes wenu na yale aliyoongea leo ndiyo mawazo yenu?, kama ndiyo ntaomba unisamehe kwa niaba ya wanaKARAGWE wenzio kwa kusema MUMETUANGUSHA WATANZANIA na daima WOTE mumekosa AKILI kama mbunge wenu".
  Ujumbe huu umenichoma sana na nikampgia simu rafiki huyo na baada ya maelezo yangu akanielewa.
   
Loading...