Gorofa kabla na baada kuporomoka

Gorofa kabla na baada kuporomoka

Namhurumia mwenye nalo. Sijui hapo kazika bilioni ngapi, na sijui kama huwa kuna utaratibu wa kuwa na bima kabla ya kuanza kulijenga ghorofa kama hilo. Na zaidi ya yote sijui kama mkandarasi wa hilo jengo alisaini mkataba gani na mwenye nalo? Je mkandaraasi atakuwa na uwezo wa kulipa gharama zote za hilo ghorofa?

Je ni nani aliyefanya uhuni hapa, ni mwenye ghorofa alikuwa anajaribu kubana matumizi au ni mkandarasi alikuwa anaiba cement na nondo? Kwa kweli nikiliangalia hili jambo hapa, naona lina msululu mrefu wa watu wanaotakiwa kuishi selo.
Wakati wa-Tanzania bado wapo kwenye majonzi na masikitiko kwa ajili ya roho za watu zilizopopotea, ndugu yetu huyu yeye anawaza kuhusu mabillion ya pesa yaliyopotea, pesa pesa pesa pesa. Na hii ni dalili tosha kuwa watu wenye akili ya kuendelea kujenga magorofa yanayofanana na hili bado wapo, mmojawapo akiwa huyu ndugu yangu, pesa kwanza, uhai wa wa_tanzania baadaye...., aiseee kuna watu wana ubongo aiseee!
 
Ulitaka niwahurumie waliokufa ilihali washakufa? Au ukiwahurumia wanaamuka? Acheni kudeal na impossibles bwana!
 
binafsi sidhani kama mwenye ghorofa anapaswa kushitakiwa, maana kaajiri maengenia na washauri juu, kama hiyo haitoshi kuna wakaguzi wa majengo wapo wanalipwa hela na serikali
Wenye magorofa wengine wakati wa ujenzi wakiambiwa gharama ni 6B, utawasikia mi nnazo 2B we fanya fanya mambo
 
Nibora limeanguka sasa ivi kuliko lingekamilika na kupangishwa hasara na maafa yangekua makubwa zaidi
 
Haya maafa hayataisha! Jana jioni majira ya saa 2:30 usiku, nikiwa njiani kurudi home, nimeona jamaa wakiwa na mkokoteni wanahamisha lundo la nondo nzima (siyo vipande) kutoka kwenye ghorofa moja linalojengwa along mtaa wa Swahili kwendea mataa ya faya kabla ya kuufikia mtaa wa mafia (kwenda klabu ya Yanga). Kwa kweli nimejiuliza sana, nondo kuondolewa eneo la ujenzi majira ya usiku zilikuwa zinapelekwa wapi? Je mkandarasi na mwenye mali wamehalalisha hilo? Je zilikuwa nondo za ziada! Je viwango vya ujenzi vimezingatiwa? Kazi tunayo!
 
Umenena vyema.....yawezekana mmiliki alimwambia mkandarasi atumie elimu na ujuzi wake sababu budget yake iko finyu......au mkandarasi kaiba malighafi mana tanzania magumashi mengi.......
mkandarasi alishajulikana ni diwani na inajulikana kabisa chama chake ni cha 'mlengo' gani, je inawezekana mmiliki pia ni wa mlengo huo huo? Kwamba walikutana kwenye vikao vyao na wakakubaliana bila shaka na pesa zikipatikana kwa 'mlengo' huo huo.
Kwa hiyo muhimu hapa ni kuwasikitikia wahanga lakini kwa mmiliki na mkandarasi ni ile hadithi ya "aliyeuza katoa dhahabu badia na aliyenunua katoa pesa bandia" ...wazoefu wanasema "ngoma droo".
Achana na nchi ya Tanzania. R.I.P walioaga dunia kwa rushwa hizi
 
Wenye magorofa wengine wakati wa ujenzi wakiambiwa gharama ni 6B, utawasikia mi nnazo 2B we fanya fanya mambo
tunaogopa sana gharama na kujali quantity badala ya kuangalia quality.
 
Hata mimi nimeona kama wewe, hata ukiangalia kingo za floors zake zimepishana kidoogo, haziko katika mtiririko mmoja.

Ndo urembo huo.
Chuo cha CBE Dodoma kikidondoka leo mtasema ivo ivo.
 
mkandarasi alishajulikana ni diwani na inajulikana kabisa chama chake ni cha 'mlengo' gani, je inawezekana mmiliki pia ni wa mlengo huo huo? Kwamba walikutana kwenye vikao vyao na wakakubaliana bila shaka na pesa zikipatikana kwa 'mlengo' huo huo.
Kwa hiyo muhimu hapa ni kuwasikitikia wahanga lakini kwa mmiliki na mkandarasi ni ile hadithi ya "aliyeuza katoa dhahabu badia na aliyenunua katoa pesa bandia" ...wazoefu wanasema "ngoma droo".
Achana na nchi ya Tanzania. R.I.P walioaga dunia kwa rushwa hizi
R.I.P lakini mmiliki naye awajibishwe....
 
Inapendeza kwamba na wewe shabiki namba moja wa CCM leo umeamua kuacha unafiki na kusema ukweli.

Hivi unamfahamu huyu vizuri kweli? Labda umamfananisha na avatar ya mtu mwingine.
 
Back
Top Bottom