Gorofa kabla na baada kuporomoka

Gorofa kabla na baada kuporomoka

Namhurumia mwenye nalo. Sijui hapo kazika bilioni ngapi, na sijui kama huwa kuna utaratibu wa kuwa na bima kabla ya kuanza kulijenga ghorofa kama hilo. Na zaidi ya yote sijui kama mkandarasi wa hilo jengo alisaini mkataba gani na mwenye nalo? Je mkandaraasi atakuwa na uwezo wa kulipa gharama zote za hilo ghorofa?

Je ni nani aliyefanya uhuni hapa, ni mwenye ghorofa alikuwa anajaribu kubana matumizi au ni mkandarasi alikuwa anaiba cement na nondo? Kwa kweli nikiliangalia hili jambo hapa, naona lina msululu mrefu wa watu wanaotakiwa kuishi selo.

Shortcut zimeanza kuwazingua wala hizo shortcut...hata hivyo pamoja na kujenga substandard building, maana kuongezea floor nyingine bila engineering considerations was illegal, alikuwa anategema nani atakayepanga kwenye jengo hilo mtaa wa Kisutu?
Kaazi kweli kweli
 
Umenena vyema.....yawezekana mmiliki alimwambia mkandarasi atumie elimu na ujuzi wake sababu budget yake iko finyu......au mkandarasi kaiba malighafi mana tanzania magumashi mengi.......[/QUOTE sister kweli mkandarasi anaweza kushauriwa na mwenye jengo kupunguzakubadilisha vipimo vya matilio...!?
yawezekana sana .....moja ya changamoto ambayo wakandarasi wanakautana nazo ni hizo.....mmiliki anataka kitu kizuri na kikubwa lakini budget finyu ila anataka wewe utumie ujuzi wako apate anachotaka.....
 
Lakini kwa mkandarasi anaefata taaluma yake kuna kiwango ikifikia inabidi uikatae kazi..
 
Nimesoma makala ktk gazeti la Jamhuri leo.. Naunga mkono Pinda nae akamatwe ahojiwe

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
binafsi sidhani kama mwenye ghorofa anapaswa kushitakiwa, maana kaajiri maengenia na washauri juu, kama hiyo haitoshi kuna wakaguzi wa majengo wapo wanalipwa hela na serikali
anapaswa sana mana tanzania magumashi mengi.......document zote ziangaliwe vizuri.....kama yeye analipa pesa alipaswa afwatilie kwa karibu kupitia consultancy wake kama mkandarasi anaweka malighafi zinazohitajika......
 
Hili jengo mbona hata kwa kuliangalia tu kwa macho kama limelalia upande vile
Kabla ya kuchukuliwa hatua mkandalasi kwanza vyeti vyake vichuguzwe
itakuwa ndo walewale ambao siku za paper hawapo darasani,alafu matokeo
yakitoka ana AAAAAAAAAAAAAAA COZ ZOTE

Hata mimi nimeona kama wewe, hata ukiangalia kingo za floors zake zimepishana kidoogo, haziko katika mtiririko mmoja.
 
Lakini kwa mkandarasi anaefata taaluma yake kuna kiwango ikifikia inabidi uikatae kazi..
ni wachache wenye huo ujasiri......wengi wanafanya ili apate pesa na kumridhisha mmiliki na kuipanua CV yake kuwa ameshawahi kujenga jengo fulani.....yawezekana pia engineer estimation ilikuwa ndogo compare to actual cost na mmiliki alikuwa amejiandaa kwa kupitia engineer estimation tu na akutaka kusitisha project yake.
 
Sasa hapo ndo serikali ichague moja kati ya haya
1. Kununua vifaa vya uokoaji maana majanga kama haya yako sanaa tu
Au
2. kuhakikisha ujenzi holela kama huu unadhibitiwa kikamilifu na sio kimchezo mchezo kama ilivyo sasa

Mungu aziweke roho za marehemu mahali pema peponi, amen
 
anapaswa sana mana tanzania magumashi mengi.......document zote ziangaliwe vizuri.....kama yeye analipa pesa alipaswa afwatilie kwa karibu kupitia consultancy wake kama mkandarasi anaweka malighafi zinazohitajika......
Ndicho ninachokifikiria pia. Inafaa asaidie polisi. Angalau na yeye atuambie ni nini kilichopelekea huko tulikofikia. Hadi kupoteza uhai wa watanzania zaidi ya 30 wasio na hatia na pia disturbance aliyoisababisha pale mahali. Though katika hali ya kawaida si ajabu huyo mwenye ghorofa, yupo hospitali hadi hivi sasa. Maana haya mambo sometimes ni mazuri kuyasikia kwa wenzako tu, yasikupate mwenyewe.
 
Mungu mkubwa, lingekuwa limekamilika na kuanza kutumika. Sijui hali ing'ekuwa vipi.
View attachment 88906
Hakika sisi Watanzania ufisadi utatuangamiza. Tumezowea kushuhudia wa asasi kubwa kubwa lakini huu wa kukabidhiwa simenti ya kuchanganyia zege kisha ukaiuza na kukoroga zege la tope Na kupanda juu yake na kuporomoka nalo ndiyo kiboko zaidi.
 
.....Hebu angalia madirisha mbona kama nyumba za uswahilini?
 
Namhurumia mwenye nalo. Sijui hapo kazika bilioni ngapi, na sijui kama huwa kuna utaratibu wa kuwa na bima kabla ya kuanza kulijenga ghorofa kama hilo. Na zaidi ya yote sijui kama mkandarasi wa hilo jengo alisaini mkataba gani na mwenye nalo? Je mkandaraasi atakuwa na uwezo wa kulipa gharama zote za hilo ghorofa?

Je ni nani aliyefanya uhuni hapa, ni mwenye ghorofa alikuwa anajaribu kubana matumizi au ni mkandarasi alikuwa anaiba cement na nondo? Kwa kweli nikiliangalia hili jambo hapa, naona lina msululu mrefu wa watu wanaotakiwa kuishi selo.

Mkuu bima ipo tena inajulikana kabisa.Inaitwa ENGINEERING INSURANCE
 
Inapendeza kwamba na wewe shabiki namba moja wa CCM leo umeamua kuacha unafiki na kusema ukweli. Ni nini tatizo sasa? Angalia vitu feki vingi vilivyowahi kukamatwa au dhuluma kubwa zilizowahi kufanywa nchini uone kama hutakuta wahusika wake wakubwa ni CCM. Hizi feki nyingi zinaendeshwa na CCM kwa kuwa hawawezi kukamatwa wala kushitakiwa kutokana na uenzetu plus michango yao kwa chama. Hapa ndipo ambapo CCM imetufikisha kwa sasa. Tuna wakati mgumu sana kusema ukweli, hadi CCM ije itoke madarakani tutakuwa tushapoteza uhai wa watanzania wengi sana.

Samahani mkuu nadhani umenifananisha.
Sijawahi hata siku moja kuwa shabiki wa ccm, una uhuru wa kucheki posts zangu kadhaa humu jamvini.
Ninakusamehe ingawa kauli yako kwangu mimi ni sawa na tusi la nguoni!
 
Nakuomba radhi kwa kuchanganya majina. Lakini ninakushukuru pia kwamba umeshanisamehe.
 
Mara nyingi sana nimekuwa nikiona kwenye blogi mbalimbali kama Michuzi, magazetini na kwenye matangazo na picha binafsi zinazoonyeshwa kwenye mitandao ya kijamii. Kwa sifa nyingi sana watu wamekuwa wakinadi 'vikwangua anga' vinavyochipuka kila kona ya jiji la Dar na miji mingine ya Tanzania. Baada ya kuangalia picha ya lile jengo lililobomoka juzi na kuangalia jinsi kile kifusi kilivyokuwa, ninaogopa hata kufikiria kuhusu ubora wa hivyo 'vikwangua anga' vinavyosifiwa sana kila kukicha. Ukweli ni kwamba suala zima la viwango nchini kwetu halipo. Madawa feki yamezagaa, hospitali ziko chini ya viwango, shule ziko chini ya viwango, barabara chini ya viwango n.k. Hivi vyote ni viashiria dhahiri vya mahali ambapo ccm ambayo imekuwa madarakani tangu ilipoanzishwa 1977 na kupokea kijiti kama kwenye mbio za vijiti kutoka TANU ambayo ilikuwa madarakani tangu 1961. Ninachojaribu kusema ni kwamba, tumepotea njia. Sasa hatuna budi kukaa chini na kufikiri ili tubadilishe kabisa mwelekeo. Tufanye maamuzi magumu leo ili kesho tuweze kuipata dira yetu ambayo itatuonyesha njia ya kuelekea huko tunakokutaka.

Mwalimu alituasa, maendeleo siyo vitu, maendeleo ni lazima yawe ya watu. Tulipoanza kushabikia vikwangua anga wakati hatuna udhibiti juu ya wajenzi, makandarasi, vifaa vya ujenzi vya uhakika ikiwemo sementi, vibali vya ujenzi vinavyotolewa kwa misingi ya rushwa na udanganyifu tulishafikiria ya kuwa vikwangua anga ndiyo maendeleo. Tujiandae kwa matukio mengi tu kama haya.

Mungu Ibariki Tanzania!

MICHUZI: vikwangua anga vyaendelea kula mbavu za mbwa jijini Dar
 
Hakuna la zaidi,zaidi ya kuwaombea wote waliotangulia kutokana na janga hili,Mungu awalaze pema peponi ameen.
 
Namhurumia mwenye nalo. Sijui hapo kazika bilioni ngapi, na sijui kama huwa kuna utaratibu wa kuwa na bima kabla ya kuanza kulijenga ghorofa kama hilo. Na zaidi ya yote sijui kama mkandarasi wa hilo jengo alisaini mkataba gani na mwenye nalo? Je mkandaraasi atakuwa na uwezo wa kulipa gharama zote za hilo ghorofa?

Je ni nani aliyefanya uhuni hapa, ni mwenye ghorofa alikuwa anajaribu kubana matumizi au ni mkandarasi alikuwa anaiba cement na nondo? Kwa kweli nikiliangalia hili jambo hapa, naona lina msululu mrefu wa watu wanaotakiwa kuishi selo.

Mkuu Lukolo nikumbushe kesho nikupe ka LIKE, umeongea vizuri
 
Last edited by a moderator:
Umenena vyema.....yawezekana mmiliki alimwambia mkandarasi atumie elimu na ujuzi wake sababu budget yake iko finyu......au mkandarasi kaiba malighafi mana tanzania magumashi mengi.......

kweli, inasikitisha sana... hapo sasa jengo la ghorofa 16 linajengwa kwa kufanya maarifa zaidi kuliko nondo na sementi,
 
Hili jengo mbona hata kwa kuliangalia tu kwa macho kama limelalia upande vile
Kabla ya kuchukuliwa hatua mkandalasi kwanza vyeti vyake vichuguzwe
itakuwa ndo walewale ambao siku za paper hawapo darasani,alafu matokeo
yakitoka ana AAAAAAAAAAAAAAA COZ ZOTE

dah limejipiga mtama pwa kwa sasa tanzania hakuna tunaloliweza.
 
Back
Top Bottom