Joeli
JF-Expert Member
- Apr 25, 2011
- 4,941
- 3,417
Jana katika mkutano wakila mwaka na madeveloper uliopewa jina la I/O, kampuni ya Google ilitangaza toleo jipya la android lililopewa codename android m, ambayo inatarajiwa kuchukua nafasi ya android lolipop ambayo iko kwa sasa.
android m ambayo imeachiwa jana rasmi kwa ma developer, itaanza kupatikana kwa watu wote baadae mwaka huu.
kama tulivoona android lolipop ilileta muonekano mpya (material design), android m itajikita zaidi katika usability na stability ya mfumo wa android alisema msemaji wa google bwana Sundar Pichai.
kwa haraka haraka, maboresho yanayokuja kwenye android m ni pamoja na kumruhusu mtumiaji kuzuia au kukubali security permissions kama accessing camera na location access.
pia kutakuwa na maboresho kadhaa katika browser ya chrome, na pia Google wanaleta mfumo wa malipo wa Android Pay ambao utachukua nafasi ya Google wallet.
pia moja ya vitu vya kusisimua ni uwezo wa android m ku support usb type-c ambayo kama tunavyojua inachaji kwa haraka na kwa urahisi, na la kuvutia zaidi ni uwezo wa kuchaji kifaa kingine kutoka kwako.
jina halisi wala version number ya android m haijajulikana (kazi kwenu mabingwa wa kuguess)
tutaendelea kujuzana kadri mambo yanvozidi kunoga, mpaka wakati mwingine,
na sign off,
picha kwa hisani ya : TheVerge