Google Adsense | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Google Adsense

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Mseriandy, May 28, 2011.

 1. Mseriandy

  Mseriandy Member

  #1
  May 28, 2011
  Joined: Mar 27, 2011
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hello JF Visitors and Members.
  I wish to make money online using Google adsense.
  What is different between page views/visitors and clicks?
  I want to sell google adwords in my websites

  ===========================================

   
 2. Chamoto

  Chamoto JF-Expert Member

  #2
  May 29, 2011
  Joined: Dec 7, 2007
  Messages: 2,086
  Likes Received: 1,125
  Trophy Points: 280
  Page views is the number of times a page is loaded (like when pressing a refresh button on your browser). Clicks is when you point your cursor on hyper text link/button and hit enter.

  Having said that, you want to have a good CTR for a give number of visitors on your page. CTR (click through ratio) is a ratio of clicks to page views, expressed in percentage. The bigger the the percentage the better (more money), but that is not always true because not all ads displayed on your page are created equal. Some will make you more money than others based on what keywords you used to optimize your page.

  The trick in making money with adsense is to find expensive keywords but also relevant to your content, not only that but they must be targeted to your visitors. Wrong targeted keywords no clicks, no tons of mulla. Comprende?
   
 3. bongompya

  bongompya JF-Expert Member

  #3
  Nov 25, 2015
  Joined: May 10, 2015
  Messages: 226
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Mimi ni mtumiaji wa google adsense kwa kipindi cha miaka 4 iliyopita au zaidi, kupitia adsense nimeweza kupata kipato cha kuendesha maisha yangu kwa njia mbalimbali, kama ujenzi wa nyumba na uendeshaji wa biashara nyingine kupitia kipato hicho tu.

  Watu wengi wanapenda kujiunga na adsense na wengine walijiunga wakakata tamaa au hata wengine akaunti zao kufungiwa kutokana na kukiuka masharti kadhaa ya google adsense, mimi mwenyewe nilifungiwa mara 3 hivi na nilipoteza zaidi ya milioni 5 za kitanzania.

  Hili ni somo fupi kwa wale wanaopenda kujiunga na adsense au ambao wameshajiunga lakini wanataka kupata faida zaidi.

  Google Adsense ni nini?
  Google adsense ni mfumo wa matangazo wa Google ambao unamwezesha mtu kitangaza bidhaa zake kwa kipato alichotacho na kumwezesha mwenye tovuti au blogu kufaidika kutokana na matangazo ya adsense kuonekana kwenye blogu yake au tovuti yake .

  Kwa lugha rahisi tunaweza kuita ppc Pay Per Click, Lipa kwa Click au mguso mmoja kwenye tangazo husika , mimi mwenye blogu hela utakuja kwangu kama mtu aligusa au gonga tangazo alilioona kwenye blogu yangu na yule aliyetangaza bidhaa zake kwenye google hela ndio inakatwa kutokana na click hiyo .

  Mimi nina blogu nyingi ambazo nimejisajili na google adsense , ukiingia kwenye blogu hizo utaona matangazo yanaonekana yale matangazo sijaweka mimi na sijuani na walioweka matangazo hayo mimi yangu ni
  blogu na nafasi ya kutangaza niliyoiweka kwenye blogu .

  Unajiungaje na Adsense?
  Adsense ni mali ya Google ni lazima au vizuri uwe na barua pepe ya
  gmail ambayo ni ya google au nyingine ambayo itakuwezesha kuweza
  kusajili adsense kwa urahisi lakini ni vizuri iwe imesajiliwa google .

  Usajili unakuwaje?
  Tembelea www.google.com/adsense ukishasajili inachukuwa siku 15 kwa tovuti yako au blogu yako kuangaliwa kama inakidhi viwango vya google adsense kama lugha, picha ,maudhui ,rangi na copyrights .

  Unaposajili unapewa CODE maalumu ambazo unaweza kuweka kwenye kurasa za tovuti au blogu yako kwa ajili ya kuanza kuonyesha matangazo mbalimbali .

  Nikisema lugha nina maanisha utumie lugha zinazokubalika na adsense kama kiingereza , kifaransa na nyingine za kimataifa Kiswahili
  hakitakiwi labda uchanganye ,kama blogu au tovuti yako ina picha chafu haitakiwi , rangi zake ziwe nzuri zisiingilie maslahi ya matangazo ya adsense na angalia milki ya vile unavyoweka .

  Baada ya siku 15 inakuwaje?
  Baada ya siku 15 utapata email kama umekubaliwa au umekataliwa kama imekataliwa unaweza kuangalia ulichokosea na kubalisha kwa kukata rufaa unatakiwa ujaze appeal form ambayo nayo itaangaliwa kwa siku 15 .

  Kama umekubaliwa basi unatakiwa kuingiza dola 100 au euro 70 , hela hizi zinapatikana kutokana na matangazo yanayoonekana kwenye blogu au tovuti yako , ukiwa na kipato hicho utatumiwa kadi yenye namba ya siri ambayo utaingiza kwenye akaunti yako ili uweze kukamilisha usajili wako wa adsense , mlolongo huu unaweza kuchukuwa miezi 2 hivi .

  Unalipwaje?
  Inategemea umechagua mfumo gani wa kulipwa, kuna mifumo 3 hivi inayojulikana zaidi.

  • Cheki - Njia hii ilikuwa inatumika zaidi zamani hata sasa hivi kwa baadhi ya nchi na wale wanaopenda , kwa wale wa afrika inachukuwa siku 7 kupata cheki yako hapo utakatwa euro 17 kwa ajili ya kusafirisha cheki hiyo ,halafu unatakiwa kuingiza cheki kwenye akaunti yako ya benki ambapo inachukuwa siku 21 kulipwa au zaidi ya hapo ? benki nyingine hazikubali cheki hizi kwahiyo wanaweza kukataa, kama ikikubali benki itakata hela ya kuprocess cheki.
  • Uhamisho wa Benki - Njia hii pia ni nzuri lakini kuna hela Fulani unakatwa kwa ajili ya kuhamisha hela kutoka nchi moja kwenda nyingine kwa njia ya benki na sio benki zote zenye huduma hii na inategemeana na kiwango cha hela inayotumwa kama ni ndogo sana inaweza kuwa tabu kidogo.
  • Western union - Hii ndio bora na ya haraka zaidi mara nyingi inalipwa kila mwisho wa mwezi unaofuatia kama ulipata dola 600 mwezi wa 3 utalipwa mwezi wa 4 mwishoni baada ya mahesabu kukamilika na baada ya kukatwa kodi na masuala mengine muhimu .
  NINI KISICHOTAKIWA?

  1. Huduma nyingine za Matangazo , Kwa sababu adsense ni Pay Per Click ni bora usiweke matangazo mengine ya PPC kwa sababu yataingiliana na maslahi ya adsense unaweza kufungiwa au kuweka huduma nyingine za matangazo ambazo zinaweza kuzorotesha huduma za matangazo ya adsense.
  2. Kulazimisha watu kugonga au click au wewe mwenyewe kufanya hivyo, hutakiwi kulazimisha watu kugonga matangazo ili ujiongezee kipato, waache waangalie na kuamua wenyewe, kazi yako iwe ni kuweka taarifa za kutosha kwenye blogu au tovuti yako zinazovutia watu kutembelea na kuvutia watu wa masoko kupitisha matangazo yao kwenye kurasa zako. Hiyo namba moja ndio ya kwanza na muhimu zaidi nyingine ni Lugha, haki miliki, picha chafu na rangi nzuri kwenye kurasa zako ambazo zitafanya matangazo kuonekana vizuri.

  FAIDA KWA MWENYE BLOGU TOVUTI
  Kutegemeana na aina ya blogu yako na maudhui lakini blogu au tovuti ili iweze kupata zaidi ya dola 15 kwa siku inatakiwa angalau kuwa na watembeleaji wa siku moja zaidi ya alfu 3000 , wanaotembelea toka nchi zinazoendelea na kuclick toka nchi za ulaya ndio wenye fedha na kuwezesha kulipwa vizuri zaidi kuliko nchi za afrika .

  Kwa Tanzania blogu ya kawaida yenye watembeleaji kati ya 2000 au 4000
  kwa Tanzania inatakiwa iwe na shilingi laki 9 kwa mwezi mmoja au zaidi
  kama kipato chake

  FAIDA KWA WATANGAZAJI /WAFANYABIASHARA
  Utangazaji kwa kupitia adsense ni rahisi na fedha yako inaenda kihalali na ni rahisi kutokana na bajeti yako kama umepanga kutangaza kwa laki 1 kwa mwezi na unataka tangazo lako lionekane Tanzania pekee basi kwa kupitia adsense hiyo inawezekana kama unataka lionekana kwa lugha ya kiingereza pekee na lionekane Kapan au Korea hilo linawezekana ni wewe kuamua na kufanikisha hilo kupitia adsense.

  Kama wewe ni mfanyabiashara huhitaji kuhangaika kutafuta blogu au tovuti kubwa kutangaza bidhaa zako ambako inaweza kuwa gharama zaidi na kupata nafasi ni finyu, fikiria adsense ifanyie kazi.

  ADSENSE INAWEZA KUWA AJIRA TOSHA?
  Inategemea na mipango yako lakini adsense sio ya kuitegemea sana kama usipofuata taratibu unaweza kufungiwa lakini kama ukifuata masharti na kukaa nayo vizuri inaweza kuwa ajira yako inayokulipa vizuri na kufanya maisha yako kwenda vizuri .

  ADSENSE SIKU ZIJAZO
  Sasa hivi watu wanatumia simu za mikononi na vifaa vingine kwa ajili ya kutembelea tovuti na blogu sio komputa kama zamani , kama ni mtumiaji wa adsense jiandae kwa hilo hakikisha matangazo yako ni mepesi na yanaweza kuonekana au kusomeka na watu wanaotuvmia vifaa hivi na kukulipa vizuri bila usumbufu mwingine. Tuwasiliane kupitia 0687-535650
   
 4. HUGO CHAVES

  HUGO CHAVES JF-Expert Member

  #4
  Nov 26, 2015
  Joined: Mar 25, 2011
  Messages: 1,852
  Likes Received: 235
  Trophy Points: 160
  mkuu nimeisoma na nimefungua link bado sijaielewa vizuri
   
 5. Asante Mambosasa

  Asante Mambosasa Verified User

  #5
  Nov 29, 2015
  Joined: May 10, 2012
  Messages: 234
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 60
  asee mkuu nina account yangu adsense lkini sasa ni mwaka wa tatu huu sijaona mafanikio yake nimeamua kuachana na biashara ya blogg kabisa naona sina bahati kama wenzangu cuz mpka leo naambiwa nna $0.99
  na blogg yangu walikuwa wanaitembelea wengi tytu kwa siku ilikuwa 150 na sikuwahi kufungiwa na matangazo yao niliwawekea sijui kwakweli
   
 6. Karimu123

  Karimu123 JF-Expert Member

  #6
  Nov 29, 2015
  Joined: Aug 3, 2015
  Messages: 213
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 45
  duuuh wew jamaa usiseme kwa nguv watu wakisokia ni aibu mkuu
   
 7. Karimu123

  Karimu123 JF-Expert Member

  #7
  Nov 29, 2015
  Joined: Aug 3, 2015
  Messages: 213
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 45
  aisee 4yrs uko vzr....sas nilulize tu unatumia lugha gan kwenyee blog
   
 8. Asante Mambosasa

  Asante Mambosasa Verified User

  #8
  Nov 30, 2015
  Joined: May 10, 2012
  Messages: 234
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 60
  swahili na engl au kuna vitu nakosea basi nicheki on asantemambosasa@gmail.com tusaidiane mkuuu huenda nikaipenda tena adsense
   
 9. Asante Mambosasa

  Asante Mambosasa Verified User

  #9
  Nov 30, 2015
  Joined: May 10, 2012
  Messages: 234
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 60
 10. J

  JJ Traders Member

  #10
  Dec 6, 2015
  Joined: Dec 3, 2015
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Mambo Vip Wakuu

  Jamani Hili tatizo la Facebook mnalipata kama mimi au ni mimi tu??Mimi ni Mtumiaje wa Adsense natumia social network kushare habari kama za kina diamond lakin sasa ukipost hata group tano tu nafungiwa akaunti mapato yameshuka sana kuna njia tunaweza kushariana kukabili changamoto hii
   
 11. ymollel

  ymollel JF-Expert Member

  #11
  Dec 6, 2015
  Joined: Aug 23, 2012
  Messages: 2,217
  Likes Received: 509
  Trophy Points: 180
  Duh! Sio wewe tu kaka' hilo ni janga kwa wengi
   
 12. Tony guy

  Tony guy Senior Member

  #12
  Dec 7, 2015
  Joined: Sep 29, 2015
  Messages: 107
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 45
  hat mm pia ila nimejua sir 0743497079
   
 13. Mathias Byabato

  Mathias Byabato Verified User

  #13
  Dec 7, 2015
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 908
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 45
  Sheria nyingi za fb zinabadilishwa bila kusema wakati mwingine.Kwa sasa suala la kupost tena kwa kutumia hizi app za multposter hiyo biashara nadhani sasa inakufa rasmi.

  Nafikiri tatizo ni kupost content juu ya nyingine kwa muda mfupi na/au kutumia account mpya.

  lakini wajuzi watatuelewesha vema.

  pole sana.
   
 14. J

  JJ Traders Member

  #14
  Dec 7, 2015
  Joined: Dec 3, 2015
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  vipi mkuu kama umejua siri na sisi wengine tunaomba utujuze tufanyeje maana wengine ndiyo tunategemea adsense kama ajira kwa hiyo tukifungiwa account fb ni majanga.kama mimi jana nilipost habari kwenye groop moja tu ile najaribu kupost groop linginje wamenifungia tayari siku kumi nimeshangaa sana nashindwa kuelewa nifanyeje.au nitumie njia gani mkuu
   
 15. cc12

  cc12 JF-Expert Member

  #15
  Dec 8, 2015
  Joined: Jan 26, 2013
  Messages: 970
  Likes Received: 206
  Trophy Points: 60
  Are You Great Thinker kweli mim ninavyojua mtu akiwa anajua kitu anatuambia hatoi namba sasa wew umetoa namba maana yake nin mkuu
   
 16. LILONGO

  LILONGO JF-Expert Member

  #16
  Dec 8, 2015
  Joined: Jan 22, 2012
  Messages: 373
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Mkuu, tupe ujuzi hapa.Hiyo namba nimeipiga haipatikani
   
 17. Potax

  Potax Member

  #17
  Dec 14, 2015
  Joined: Jan 10, 2015
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Eti ni kweli kuwa siku hizi AdSense wamesitisha kupokea new publishers
   
 18. mishe bwoy

  mishe bwoy Senior Member

  #18
  Dec 19, 2015
  Joined: Oct 26, 2014
  Messages: 118
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Mwongo huyo tena ndio wamefungua madirirsha
   
 19. Rider

  Rider Content Manager Staff Member

  #19
  Dec 19, 2015
  Joined: Apr 18, 2010
  Messages: 62
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
 20. Rider

  Rider Content Manager Staff Member

  #20
  Dec 19, 2015
  Joined: Apr 18, 2010
  Messages: 62
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
Loading...