Google Adsence Special Thread: Tupeane Maoni, ushauri na Ujanja

Kasomi

JF-Expert Member
Sep 3, 2014
11,036
20,337
Hello mates kwenye jukwaa hili la Tech, Kwa wale wenye uhitaji wa kujua au kushea ideas Juu ya Google Google Adsence Tukutane hapa.

Je, unamiliki Blogu, tovuti au Channel ya YouTube ungependa kujua mengi kuhusu Google Adsence au una Google Adsence account tayari ungependa kushea ushauri au mbinu basi huu ni uzi muhimu.

Pia uzi huu utahusisha somo jinsi ya kujiunga, kulipwa, kupokea malipo na vigezo vya kulipwa na Google Adsence.

Karibu Wadau
 
Umefanya jambo jema angalau mimi nilitimiza vigezo mda kidogo na pia nalipwa kupitia Google adsense ila itakuwa vyema kwa watu hajawai pia wanatamani kujua
 
Nachojua kuna aina mbili za piblishers.

Publishers wasafi - kwa upande wa bloggers wengi bado wapo google adsense lakini wengi wao wanacheza wanapokea laki 2 jadi laki 8 kwa mwezi, hali hii imefanya wengi kuhamia youtube kwenye nafuu, kuna kipindi youtube ilimpa millard ayo mkwaja mrefu miaka ya 2013 hadi 2015 alikuwa anapiga views kijiji ila saizi ushindani ni mkubwa na pia mabando yamepanda bei ni changamoto kiasi, pia kuna adsense ya kwenye apps nayo imetulia maana ushindani ni mdogo ukilenga penye uhitaji unaogelea pesa.

Pubishers watukutu - hawa wanatengeneza blog hata haina mpangilio inakuwa na kitufe ambacho mtu akiminya pesa imeingia, wanashare lnk za blog zao kwa kutegesha picha zinazoshawishi kuminya kwenye makundi ya facebook ili wapate watembeleaji, hawa wanapiga hadi milioni 20 kwa mwezi, adsense walipowastukia mchezo wao wakahamia propeller ads, huko nako wakazinguliwa wakahamia adsterra, kwa sasa wapo huko kunaitwa gg agency, mtu analaza dola 300 kila siku utadhani mchezo.

miaka hiyo wakiwa google adsense ikifika tarehe 22 ndio ilikuwa siku ya malipo, unakuta dogo ana miaka 19 amaenda kuchukua dola milioni 4 na upuuzi kwenye lile dirisha la kupokea hela kwa western union, hapo walikuwa wanapiga milioni 4.x kwa maksudi maana ilikuwa ukizidisha hapo basi western union inakua ngumu kutoa hela, sasa hao bloggers wakaja kufanya uchunguzi wa kuruka hicho kiunzi ndio wakajua kuna njia ya bank transfer inayorusu kutoa pesa zaidi na pesa zinaingia moja kwa moja benki, hii watu walikuwa wanapiga dola milioni 20 kila mwezi, benki pendwa ilikuwa ni Equity Bank ambayo waliweza kuungansha hio njia ya bank transfer, watu wa bank walikuwa wanashangaa sana. Mpaka sasa watu wanaendelea kupiga dollar ila wamehamia gg agency huko naskia wanalipa kwa bitcoins then unaziuza na kuzibadili ziwe tshs.

Huku mtu akikusikia anaweza kuona ni rahisi ila asikwambie mtu huku mambo yanabadilka sana, njia ikianz kutumika leo kupiga dollar unakuta inakaa miezi sita tu baada ya hapo ishachuja, hizi njia wanaziita "triki", ili kupata hizo triki inabidi uwe karibu na wenye nazo na muhimu zaidi uwe na pesa ya kulipia, triki zinauzwa mpaka milioni huko, kwa mfano kupewa orodha ya groups za kuposti link yako watu walikuwa wanauziawa laki 5, kusetiwa matangazo laki 3, n.k. na ninarudia tena, hapa inabidi uwe unajuana nao au umeshikwa mkono, unaweza kwenda na pesa wakakutolea nje.

Pia kuna visasi na umafia wa hali ya juu sana, unakuta kuna wale waliokuwa wananyimwa triki, wamepambana wakapata triki zao wakaanza kupiga dollar, hizo triki huwa hawawapi waliowanyima enzi hizo, kazi inakuwa ni kuposti tu dollar wanazopiga ila hawakupi mbinu, kuna bloggers walikuwa wanalaza dolla za kutosha miaka ya 2015 lakini baada ya triki zao kuchujaleo hii wanatia huruma uchumi umeyumba, so huku hkunaga uhakika wa kesho.

Binafsi nilikuwa natamani huko sehemu ya pili ila ilishindikana maana kuna umafia wa hali ya juu sana, nilikosai laki 3 ya kusetiwa blog, wakati naitafuta nikatonywa kwamba bado watahitaji laki 3 ya groups, sikuja tena kufikiria kurudi huko, nikaona ntamezwa tu.

Kundi la kwanza uhakika na usalama ila linahitaji uvumilivu sana maana unaweza kuanza kupiga hela ya maana kidogo baada ya msoto wa miaka mitatu. kundi la pili hilo halina uhakika na ni hatari lakini pesa ipo ukijua kucheza na game, ila ndio hivyo tena, wapo watu waliotikisa miaka ya juzi tu hapo 2018 ila leo hii wameanguka vibaya mno.
 
Nachojua kuna aina mbili za piblishers.

Publishers wasafi - kwa upande wa bloggers wengi bado wapo google adsense lakini wengi wao wanacheza kwenye dola 100 hadi 400 kwa mwezi. kwa upande wa youtube huku Kuna kipindi millard ayo miaka ya 2013 hadi 2015 alikuwa anapiga views kijiji ila saizi ushindani ni mkubwa na pia mabando yamepanda bei ni shida sana kwa youtuber mpya labda kwa hawa comedians, kuna adsense ya kwenye apps nayo imetulia maana ushindani ni mdogo ukilenga penye uhitaji.

Pubishers watukutu - hawa wanatengeneza blog hata haina mpangilio inakuwa na kitufe ambacho mtu akiminya pesa imeingia, wanashare picha zinazoshawishi kuminya kwenye makundi ya facebook ili wapate watembeleaji, hawa wanapiga hadi dola elf 8 kwa mwezi, adsenae walipowazingua wakahamia propeller ads wakahamia adsterra na sasa wapo huko kunaitwa gg agency, mtu analaza dola 300 kila siku utadhani mchezo.

miaka hiyo wakiwa google adsense ikifika tarehe 22 ambayo ni siku ya malipo, unakuta dogo ana miaka 19 amaenda kuchukua dola elf 2 kwa western union (kama una mtu anaefanyia benki zenye hio huduma mwambie akupe stori za ziada), hapo walikuwa wanapiga dola elf 2 maksudi maana ilikuwa ukizidisha sana western union inakua ngumu kutoa hela, sasa wakaja kufanya uchunguzi wakajua kuna njia ya bank transfer inayorusu kutoa pesa zaidi, hii watu walikuwa wanapiga dola elf 10 kila mwezi pesa zinaingia kwenye account ya benki moja kwa moja, benki pendwa ilikuwa ni Equity Bank, watu wa bank walikuwa wanashangaa sana.

Mpaka sasa watu wanagonga pesa za maana ila upande huo mambo hayatulii, yanabadilika kila muda hivyo inabidi uwe mhunifu, uwe na connections, n.k. kitu kidogo tu kikibadilika, njia ya kukitatua inaweza kuuzwa hata laki 3 kawaida kabisa, kwa mfano miaka hio ya zamani mtu alikuwa anauziwa groups za facebook kwa laki 5, huko ndio anaenda kushea link zake ili apate wambeleaji.

Binafsi nilikuwa natamani huko sehemu ya pili ila ilishindikana maana kuna umafia wa hali ya juu sana, niliambiwa ili kisetiwa tu blog ni laki 3, sikuja tena kufikiria kurudi huko, nikaona ntamezwa tu.

Anyway, bora ufanye kitu chenye uhakika kuliko kitu cha ujanja ujanja, hivyo vya ujanja ujanja hakikisha na wewe ni mjanja ama umezungukwa na wajanja lasivyo ujipange kisaikolojia.
Mkuuu ebu zungumza hii gg man naisikia san
 
Umefanya jambo jema angalau mimi nilitimiza vigezo mda kidogo na pia nalipwa kupitia Google adsense ila itakuwa vyema kwa watu hajawai pia wanatamani kujua
Mkuu jaribu kushea uzoefu wako je, ni njia gani Google AdSense hulipa/ wewe unalipwa kwa njia gani.

Na hatua gani ulifuata ili kulipwa baada ya kukamiliza vigezo. Na pin ulipokeaje kutoka Google na zilichukua Muda gani.
 
Kimasiara nimefungua kiblog nimeunaga na adsterra hii ni siku ya 3 ngoja nione maendeleo

Ahsante kwa maelezo mazuri, kweli nimekuwa motivated sana.
 
Bloga wengi wa bongo ni hao wa type namba mbili. Na huwez kupewa technique mpaka uwe unajuana nao. Mwaka 2019 nilimfata bloga mmoja mpaka mbeya lakn nikaishia kuchoma pesa yangu kama laki 6 hv.

Sent from my TECNO LC6a using JamiiForums mobile app
 
Mkuu jaribu kushea uzoefu wako je, ni njia gani Google AdSense hulipa/ wewe unalipwa kwa njia gani.

Na hatua gani ulifuata ili kulipwa baada ya kukamiliza vigezo. Na pin ulipokeaje kutoka Google na zilichukua Muda gani.
Kama utafikisha vigezo vya kulipwa na Google adsense kuna njia 3 za kupokea pesa zako uliofanikiwa kutengeneza.

Njia ya kwanza kupitia western union

Njia ya pili ni bank wire transfer ambayo mimi huwa na itumia kwa sababu inanipa taharifa kupitia simu yangu ya mkononi kwamba kuna pesa imeingia kwenye account yangu ya bank, njia hii unachotakiwa kufanya unaenda kwenye bank yako usika au utawapigia simu ila uzuri uwende ukaombe SWIFT codes Ambazo utazijaza kwenye Google adsense yako na account number ya Bank.

Njia ya tatu ni PayPal account njia hii kwetu ni ngumu kupokea pesa kwa sababu serikali yetu hajakubaliana kupokea pesa kupitia mfumo huu.

Kupata PIN kutoka Google adsense inachukua siku 14 tu ila kwangu ilichukua siku 7 nilikuwa tayari nimeshazipata

Njia ya kupata PIN nilitumia Anuani ya P.O Box amalo unalotumia na kama hauna basi unaweza kufungua la mtu Binafsi kwa kipindi nilichofungua mimi ilikuwa 27,000/= ila kwa sasa sijui.

Kwanini huwa wanakutumia PIN?
Google wanataka kuakikisha sehemu uliopo kwa sababu kuna mataifa hawana maelewano mzuri kibiashara na ndiomaana ufanya ivyo.
 
Bloga wengi wa bongo ni hao wa type namba mbili. Na huwez kupewa technique mpaka uwe unajuana nao. Mwaka 2019 nilimfata bloga mmoja mpaka mbeya lakn nikaishia kuchoma pesa yangu kama laki 6 hv.

Sent from my TECNO LC6a using JamiiForums mobile app
Ulichoma pesa kwa sababu ulikua unataka shortcut!

Kwenye content creation hakuna shortcut kama unataka mafanikio ya muda mrefu.
 
Nachojua kuna aina mbili za piblishers.

Publishers wasafi - kwa upande wa bloggers wengi bado wapo google adsense lakini wengi wao wanacheza wanapokea laki 2 jadi laki 8 kwa mwezi, hali hii imefanya wengi kuhamia youtube kwenye nafuu, kuna kipindi youtube ilimpa millard ayo mkwaja mrefu miaka ya 2013 hadi 2015 alikuwa anapiga views kijiji ila saizi ushindani ni mkubwa na pia mabando yamepanda bei ni changamoto kiasi, pia kuna adsense ya kwenye apps nayo imetulia maana ushindani ni mdogo ukilenga penye uhitaji unaogelea pesa.

Pubishers watukutu - hawa wanatengeneza blog hata haina mpangilio inakuwa na kitufe ambacho mtu akiminya pesa imeingia, wanashare lnk za blog zao kwa kutegesha picha zinazoshawishi kuminya kwenye makundi ya facebook ili wapate watembeleaji, hawa wanapiga hadi milioni 20 kwa mwezi, adsense walipowastukia mchezo wao wakahamia propeller ads, huko nako wakazinguliwa wakahamia adsterra, kwa sasa wapo huko kunaitwa gg agency, mtu analaza dola 300 kila siku utadhani mchezo.

miaka hiyo wakiwa google adsense ikifika tarehe 22 ndio ilikuwa siku ya malipo, unakuta dogo ana miaka 19 amaenda kuchukua dola milioni 4 na upuuzi kwenye lile dirisha la kupokea hela kwa western union, hapo walikuwa wanapiga milioni 4.x kwa maksudi maana ilikuwa ukizidisha hapo basi western union inakua ngumu kutoa hela, sasa hao bloggers wakaja kufanya uchunguzi wa kuruka hicho kiunzi ndio wakajua kuna njia ya bank transfer inayorusu kutoa pesa zaidi na pesa zinaingia moja kwa moja benki, hii watu walikuwa wanapiga dola milioni 20 kila mwezi, benki pendwa ilikuwa ni Equity Bank ambayo waliweza kuungansha hio njia ya bank transfer, watu wa bank walikuwa wanashangaa sana. Mpaka sasa watu wanaendelea kupiga dollar ila wamehamia gg agency huko naskia wanalipa kwa bitcoins then unaziuza na kuzibadili ziwe tshs.

Huku mtu akikusikia anaweza kuona ni rahisi ila asikwambie mtu huku mambo yanabadilka sana, njia ikianz kutumika leo kupiga dollar unakuta inakaa miezi sita tu baada ya hapo ishachuja, hizi njia wanaziita "triki", ili kupata hizo triki inabidi uwe karibu na wenye nazo na muhimu zaidi uwe na pesa ya kulipia, triki zinauzwa mpaka milioni huko, kwa mfano kupewa orodha ya groups za kuposti link yako watu walikuwa wanauziawa laki 5, kusetiwa matangazo laki 3, n.k. na ninarudia tena, hapa inabidi uwe unajuana nao au umeshikwa mkono, unaweza kwenda na pesa wakakutolea nje.

Pia kuna visasi na umafia wa hali ya juu sana, unakuta kuna wale waliokuwa wananyimwa triki, wamepambana wakapata triki zao wakaanza kupiga dollar, hizo triki huwa hawawapi waliowanyima enzi hizo, kazi inakuwa ni kuposti tu dollar wanazopiga ila hawakupi mbinu, kuna bloggers walikuwa wanalaza dolla za kutosha miaka ya 2015 lakini baada ya triki zao kuchujaleo hii wanatia huruma uchumi umeyumba, so huku hkunaga uhakika wa kesho.

Binafsi nilikuwa natamani huko sehemu ya pili ila ilishindikana maana kuna umafia wa hali ya juu sana, nilikosai laki 3 ya kusetiwa blog, wakati naitafuta nikatonywa kwamba bado watahitaji laki 3 ya groups, sikuja tena kufikiria kurudi huko, nikaona ntamezwa tu.

Kundi la kwanza uhakika na usalama ila linahitaji uvumilivu sana maana unaweza kuanza kupiga hela ya maana kidogo baada ya msoto wa miaka mitatu. kundi la pili hilo halina uhakika na ni hatari lakini pesa ipo ukijua kucheza na game, ila ndio hivyo tena, wapo watu waliotikisa miaka ya juzi tu hapo 2018 ila leo hii wameanguka vibaya mno.
Asante sana kwa kushea Stori hiyo. Binafsi nilitaka nijikite kwenye maswala ya blogu, ila content nyingi nikitaka kulenga audience wa Kiswahili na hasa wabongo. Ila kikwazo ni AdSense Kwa blog zinazo tumia Kiswahili ikawa kisanga.

Ila Kwa sasa nimeamua kujikita kwenye YouTube hapo nitavumiliana nao hata miaka kadhaa mpaka tobo litakapo onekana.
 
Kama utafikisha vigezo vya kulipwa na Google adsense kuna njia 3 za kupokea pesa zako uliofanikiwa kutengeneza.

Njia ya kwanza kupitia western union

Njia ya pili ni bank wire transfer ambayo mimi huwa na itumia kwa sababu inanipa taharifa kupitia simu yangu ya mkononi kwamba kuna pesa imeingia kwenye account yangu ya bank, njia hii unachotakiwa kufanya unaenda kwenye bank yako usika au utawapigia simu ila uzuri uwende ukaombe SWIFT codes Ambazo utazijaza kwenye Google adsense yako na account number ya Bank.

Njia ya tatu ni PayPal account njia hii kwetu ni ngumu kupokea pesa kwa sababu serikali yetu hajakubaliana kupokea pesa kupitia mfumo huu.

Kupata PIN kutoka Google adsense inachukua siku 14 tu ila kwangu ilichukua siku 7 nilikuwa tayari nimeshazipata

Njia ya kupata PIN nilitumia Anuani ya P.O Box amalo unalotumia na kama hauna basi unaweza kufungua la mtu Binafsi kwa kipindi nilichofungua mimi ilikuwa 27,000/= ila kwa sasa sijui.

Kwanini huwa wanakutumia PIN?
Google wanataka kuakikisha sehemu uliopo kwa sababu kuna mataifa hawana maelewano mzuri kibiashara na ndiomaana ufanya ivyo.
Walikutimia hiyo barua yenye PIN je ilichukua muda gani kukufikia?
 
Kimasiara nimefungua kiblog nimeunaga na adsterra hii ni siku ya 3 ngoja nione maendeleo

Hongera maana hii ni moja ya hatua nzuri huenda karibuni mkwanja unaweza kuvuna.
 
Asante sana kwa kushea Stori hiyo. Binafsi nilitaka nijikite kwenye maswala ya blogu, ila content nyingi nikitaka kulenga audience wa Kiswahili na hasa wabongo. Ila kikwazo ni AdSense Kwa blog zinazo tumia Kiswahili ikawa kisanga.

Ila Kwa sasa nimeamua kujikita kwenye YouTube hapo nitavumiliana nao hata miaka kadhaa mpaka tobo litakapo onekana.
Ukitegemea audience wa bongo utaishia kupata lower cpm
 
Hongera maana hii ni moja ya hatua nzuri huenda karibuni mkwanja unaweza kuvuna.
shida kubwa ni pesa haziongezeki zilikuja kwa speed zika ganda ghafla

gc.PNG
 
Back
Top Bottom