Goodluck Ole Medeye aikimbia CHADEMA. Atimkia UDP

Goodluck Ole Medeye aikimbia CHADEMA. Atimkia UDP

Spika wa UKAWA huyo.

Watu walifuata asali wakakuta nyuki. Asione soni kurudi nyumbani, maana ameona hata Lowassa mwenyewe anaongea huko kwa vile tu amenunua chama.

mwakani tutaona wengi.
 
Tunaheshimu maamuzi yake. Ila hajahama kwa sababu kukosa demokrasia ya kweli ndani ya CHADEMA, labda sababu nyingine tu!

By the way? Hivi Makamu mwenyekiti wa UDP ni nani? Katibu je? Mara ya mwisho UDP walifanya mkutano wao mkuu mwaka gani?
Mkuu vipi tena? Unahoji demokrasia ndani ya UDP ilhali kwenye chama chenu hakuna demokrasia! Inashangaza
 
Yaani watu wengine sijui Mungu awape nini. Chukulia mfano Lawrence Masha, mtu aliyepata bahati ya kuwa waziri akiwa chini ya miaka 35. Lakini badala ya kujitahidi kumaintain position yake, anajikuta anafanya ujingaujinga na kupotea kabisa hewani. Sijui tatizo huwaga nini?
Huyu naye ndiyo mwingine anapotea.
 
Njaa hii jamani inaleta aibu, hata kama ni haki yake ya kidemokrasia sasa UDP ndiyo chama gani?, si bora angeenda cuf mweeee au nccr mageuzi
 
Duuuh...huyu si ndio yule aliyekuwa anamsindikiza lowassa katika kila tukio kipindi kileee!!!wanasiasa buana.kwahiyo chadema hakuna hayo anayoyasema!na tungempa uspika je?haaminiki.
 
Mkuu vipi tena? Unahoji demokrasia ndani ya UDP ilhali kwenye chama chenu hakuna demokrasia! Inashangaza
Jibu maswali hapo juu, acha Porojo, CHADEMA ni taasisi huwezi kuifananisha na UDP au TLP. Nakubali CHADEMA kama taasisi ina changamoto zake ambazo hazikwepeki na chama kinazifanyia kazi ili kuondokana nazo.
MEDEYE ameenda huko UDP kwa kuwa anafahamu atapata cheo cha bwerere na ushindani sio mkali, lakini unapaswa kujua UDP sio chama bora ni bora chama!
 
Cheyo atamtoa out....hivi cheyo yupo kweli? Ataukubali u DC?
 
Back
Top Bottom