Goodluck Ole Medeye aikimbia CHADEMA. Atimkia UDP

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,599
6,669
image.jpeg

image.jpeg
Kada wa CHADEMA na mbunge wa zamani wa Arumeru Magharibi, Goodluck Ole Medeye leo ametangaza kuhamia UDP.

Amesema inasimamia haki na demokrasia. Anasema anataka demokrasia ya kweli na jukwaa la haki ktk kuleta haki na maendeleo kwa Watanzania.

Ameyasema haya akiongea na waandishi wa habari muda mfupi uliopita.

Medeye amezungumza kwa kujipambanua kuwa yeye anasimamia haki na demokrasia, na kwamba amekerwa sana na tabia ya vyama vya Upinzani kutomheshimu Naibu Spika.

DISCLAIMER: Bango linaloonekana nyuma yake halina uhusiano na habari, lipo ofisi za UDP
 
Umekosea hapo juu tu uliposema KADA wa cdm hayo mengine mwache aende kutafuta panapo mfaa
 
Tunaheshimu maamuzi yake. Ila hajahama kwa sababu kukosa demokrasia ya kweli ndani ya CHADEMA, labda sababu nyingine tu!

By the way? Hivi Makamu mwenyekiti wa UDP ni nani? Katibu je? Mara ya mwisho UDP walifanya mkutano wao mkuu mwaka gani?
 
Ni haki Yake kikatiba kuchagua chama cha siasa kila la heri katika chama chake kipya
 
Angeenda zanzibar maana kule ndiyo kuna njia za mkato kujipatia uwaziri kama Hamadi Rashid
 
Mbona hilo bango linaonesha Mkutano Mkuu wa tarehe 26/3/2011? Toa ufafanuzi wa hiyo picha
 
Back
Top Bottom