Good faith ni nini?

Accacia ndio katuletea matatizo na kuibiwa wote wawili watanzania na barrick. Barrick kumwambia accacia alipe hizo dola milioni 300 ni kumwbia live yaani wewe bwege accacia ulikula hadi kodi za serikali? Lipa halafu mengine tutamalizana mimi na wewe yanayohusu ulichoniibia mimi barrick. Accacia alikuwa akiiba kote anasafirisha kontaine mfano 20 kwetu analaghai kasafirisha nane akifika kwa barrick anawadanganya kuwa kasafirisha kumi yaliyozidi anapeleka nchi nyingine pesa anaweka kibindoni. Ndio maana barrick waliungana na magufuli alipoitisha uhakiki wa kontaina zilizosafirisha na kilichomo Wakasema tuwe pamoja kwenye hili. Akina accacia wakaanza propaganda za kukwepa hilo ndio wakaanza kuhonga wanasiasa Kama Lisu Na chadema na akina Zitto kabwe kama ngome yao ya defence ya kuwalinda vibaka baada ya kuwaona kuwa wananunulika kirahisi kutokana na uchunguzi waliofanya waliogundua. Kila fisadi ni rahisi kununua mwanasiasa yeyote wa chadema Na kuwafanya watetezi wao. Awe fisadi au jambazi la kibiti laweza kuwahonga kesho likipigwa risasi chadema utakuta tayari wanaibuka kulaani jambazi la kibiti kujeruhiwa ukucha lakini polisi hata kumi wakiuawa husikii chadema Kutoa tamko hata pole kisa polisi hawajawapa rushwa Kama majambazi
Yawezekana ulikuwa na hoja, ila ukachanganya na upupu ndani. Kilichotoka ni upumbavu na ujinga.

Usifikirie kwa kutumia makalio
 
Asante kwa kunipigia nakozi hili bichwa buyu lisilo na chembe ya uelewa zaidi ya kuwashambulia watu! Hoja ya msingi tena yenye maana na msaada kwa wale wapiga vigelegele lenyewe linaijadili kipuuzi tu eti kwa kuwa linajua kusoma na kutumia smartphone! Hebu atuondolee mawazo yake ya kifedhuli akagongee ugali mlenda kwa shemejie!
 
Ni pesa inayotolewa mbele kuonyesha nia ya kulipa au kuheshimu na kukubali mapatano. Mara nyingi huwa ni asilimia fulani ya deni linalodaiwa.

Kwenye hotuba ya profesa Kabudi kipengele cha 14 kilisema hivi:

"14. Suala la fidia lilikuwa suala gumu sana na ndilo lililochukua muda mrefu lazima tupitie nyaraka, ila wamekubali kutoa dola milioni 300 wakati mazungumzo ya jambo hilo yanaendela. Watanzania tuna kila sababu ya kumshukuru Rais Magufuli kwa azma ya kusimamia mambo haya kidete na kwa nguvu zote na kututia moyo na kutuamini sisi badala ya kuleta wataalamu kutoka nje."

Kwa maana nyingine mazungumzo kuhusu fidia hayajaisha na yanaendelea. Na Tanzania haijasamehe fidia ambayo haijalipwa. Bado wanaendelea kupitia nyaraka. Barrick wameamua kulipa hizo bilioni 700 kuonyesha nia yao kulipa hiyo fidia makubaliano yatakapokamilika.

Kumekuwa na upotoshaji au kutokuelewa kitu kilichowekwa hadharani. Kuna wanaosema kwa Barrick kutoa good faith money maana yake ni kuwa hawakuwa na kosa lolote.

Wengine wamebeza bilioni 700 ni asilimia ngapi ya trilioni tunazodai?

Kitendo cha wao kukubali kulipa hiyo good faith money maana yake wamekubali tunawadai. Katika hatua hii hawawezi kushinda mahakama yeyote ile ikiwa mapatano yatavunjika kwa wao kugoma kulipa.

Hata kama kuna habari ya kuwa hawana pesa ya kulipa. Kutokuwa na pesa ya kulipa na kukataa kulipa ni vitu tofauti.

Vilevile kuna kipengele wamekikubali cha kuwabana waweke pesa katika akaunti za Tanzania. Hapo ndipo asilimia 50 ya Tanzania, kodi na hilo suala la kuwa wana hela ya kulipa au hawana litakapojulikana kirahisi.

Mungu Ibariki Tanzania!

Kwa hiyo hiyo bilioni 700 ni sehemu ya fidia au ni "good faith"? Je, kuna tofauti kati ya "good faith" na "fidia"? Vipi kuhusu malimbikizo ya kodi na mrahaba wanayodaiwa Acacia i.e. US$ 190 bilioni? Je hiyo ndio fidia inayozungumzwa? Fidia = (malimbikizo ya kodi + mrahaba) + interest = good faith? Hiyo good faith ya bilioni 700 ni asilimia ngapi ya fidia? Ukisema fidia, wanafidia nini?
 
Kwa Tanzania kukubali hizo hela zinazoitwa za good faith ni kwamba pande zote zinakubali taratibu zifuatwe kuutafuta ukweli uliokuwa ukidaiwa na kila upande. Msuluhishi asiyeegemea upande wowote atatafutwa, uchunguzi utafanyika, mikataba itapitiwa, sheria itachukua mkondo wake na mwisho wa siku ukweli utabainika. Hizo bilioni 700 zinaweza zikawa hela zetu halali na zikaongezeka au zikageuka na kuwa deni (mkopo) lenye riba kulingana na ripoti itakayotoka. Kwa vyovyote vile suluhisho litapatikana tu Mahakamani.

Kwa kutotaka kushiriki katika haya mazungumko, Acacia wamekuwa wajanja sana kwani makubaliano yoyote yanayofikiwa hayawafungi na ndio maana Barick wakasema subject to approval ya bodi ya Acacia. Kwa sasa ngoja kama kawaida yetu tushangilie, kwa miaka karibu 60 imekuwa kawaida yetu kuwashangilia wapuuzi na kila baada ya miaka mitano tunawarudisha madarakani wezi wale wale. Tukishapiga kura tunarudi katika umasikini wetu ule ule wa siku zote kusubiri uchaguzi mwingine tuwarudishe tena hao hao.
 
Unamdai kwa vielelezo vitakavyothibitishwa mahakamani au kwa ripoti ya profs Ossoro na Mruma?

Hayo malipo ya good faith ni ushahidi wa kukubali kulipa deni. Usipolipa huwezi kwenda mahakama ya nje kushitaki na ukashinda. Isitoshe kuna kipengele cha kuwabana kesi zote ziishie Tanzania.

Yaani hawa jamaa wamezimaindi sana dhahabu za Tanzania mpaka kufikia kukubali masharti ya aina hii.
Walimuangalia Magufuli wakaona sura ya mtu aliyekubali tukose wote
 
Kwa hiyo hiyo bilioni 700 ni sehemu ya fidia au ni "good faith"? Je, kuna tofauti kati ya "good faith" na "fidia"? Vipi kuhusu malimbikizo ya kodi na mrahaba wanayodaiwa Acacia i.e. US$ 190 bilioni? Je hiyo ndio fidia inayozungumzwa? Fidia = (malimbikizo ya kodi + mrahaba) + interest = good faith? Hiyo good faith ya bilioni 700 ni asilimia ngapi ya fidia? Ukisema fidia, wanafidia nini?

Ni hivi, jamaa wamekubali wanadaiwa malimbikizo ya kodi. Lakini hawajakubaliana wanadaiwa ngapi. Mazungumzo yanaendelea na nyaraka zinapitiwa.

Ila kwa kuonyesha kuwa muafaka ukifikiwa wa hilo deni watalipa ndio wakatoa hicho kishika uchumba cha bilioni 700.

Na sijui makubaliano kamili lakini hizo bilioni 700 zinaweza kutolewa katika deni lao kamili wanalodaiwa siku wakifikia muafaka(makubaliano)
 
Kwa Tanzania kukubali hizo hela zinazoitwa za good faith ni kwamba pande zote zinakubali taratibu zifuatwe kuutafuta ukweli uliokuwa ukidaiwa na kila upande. Msuluhishi asiyeegemea upande wowote atatafutwa, uchunguzi utafanyika, mikataba itapitiwa, sheria itachukua mkondo wake na mwisho wa siku ukweli utabainika. Hizo bilioni 700 zinaweza zikawa hela zetu halali na zikaongezeka au zikageuka na kuwa deni (mkopo) lenye riba kulingana na ripoti itakayotoka. Kwa vyovyote vile suluhisho litapatikana tu Mahakamani.

Kwa kutotaka kushiriki katika haya mazungumko, Acacia wamekuwa wajanja sana kwani makubaliano yoyote yanayofikiwa hayawafungi na ndio maana Barick wakasema subject to approval ya bodi ya Acacia. Kwa sasa ngoja kama kawaida yetu tushangilie, kwa miaka karibu 60 imekuwa kawaida yetu kuwashangilia wapuuzi na kila baada ya miaka mitano tunawarudisha madarakani wezi wale wale. Tukishapiga kura tunarudi katika umasikini wetu ule ule wa siku zote kusubiri uchaguzi mwingine tuwarudishe tena hao hao.

Ongea vya ukweli acha kufikirika. Nani aliyetaja mahakama ya kuchunguza deni katika zile hotuba tatu.
 
In the Indian Penal Code, "good faith" is defined under Section 52 as Nothing is said to be done or believed in “good faith” which is done or believed without due care and attention.
SOURCE :WIKIEPAEDIA
 
Kwahiyo Tz pia imepewa kishika uchumba?
Inavyoonekana tumeahidiwa kishika uchumba, tayari vigodoro vinakesha kushangilia. Ila muoaji ni Barrick au Acacia? au tunaolewa na wanaume wote wawili? Hapo naomba nisaidiwe
 
Usiwadanganye watu. Kasome taarifa ya Barrick. Msipende kujifariji. Hakuna wizi uliothibitika, hakuna udanganyifu uliothibitika wala kodi iliyokwepwa.

Taarifa ya Barrick imesema wazi kuwa tumekubali kuipa Tanzania malipo ya MARA MOJA dola milioni 300 in good faith. Kitu unachopewa in good faith ni pale inapodhihirika huna stahili lakini anayekupa anataka mwendelee kuwa na uhusiano mzuri.

Mazungumzo yatakayoendelea hayahusiani na dola billion 190, yatahusu kufuta kesi na utaratibu wa kutolewa hizo dola milioni 300.

Na Rais aliweka wazi kuwa 'watupatie hizo milioni 300, hawa sasa ni ndugu zetu, tutafanya kazi pamoja, na watu mkishakuwa ndugu mnafanya kazi pamoja. Barrick is here to stay'. Hayo uliyasikia au unajifanya hukuelewa?
 
Bila shaka bhachu atakuwa na jibu kamili
 
Ni pesa inayotolewa mbele kuonyesha nia ya kulipa au kuheshimu na kukubali mapatano. Mara nyingi huwa ni asilimia fulani ya deni linalodaiwa.

Kwenye hotuba ya profesa Kabudi kipengele cha 14 kilisema hivi:

"14. Suala la fidia lilikuwa suala gumu sana na ndilo lililochukua muda mrefu lazima tupitie nyaraka, ila wamekubali kutoa dola milioni 300 wakati mazungumzo ya jambo hilo yanaendela. Watanzania tuna kila sababu ya kumshukuru Rais Magufuli kwa azma ya kusimamia mambo haya kidete na kwa nguvu zote na kututia moyo na kutuamini sisi badala ya kuleta wataalamu kutoka nje."

Kwa maana nyingine mazungumzo kuhusu fidia hayajaisha na yanaendelea. Na Tanzania haijasamehe fidia ambayo haijalipwa. Bado wanaendelea kupitia nyaraka. Barrick wameamua kulipa hizo bilioni 700 kuonyesha nia yao kulipa hiyo fidia makubaliano yatakapokamilika.

Kumekuwa na upotoshaji au kutokuelewa kitu kilichowekwa hadharani. Kuna wanaosema kwa Barrick kutoa good faith money maana yake ni kuwa hawakuwa na kosa lolote.

Wengine wamebeza bilioni 700 ni asilimia ngapi ya trilioni tunazodai?

Kitendo cha wao kukubali kulipa hiyo good faith money maana yake wamekubali tunawadai. Katika hatua hii hawawezi kushinda mahakama yeyote ile ikiwa mapatano yatavunjika kwa wao kugoma kulipa.

Hata kama kuna habari ya kuwa hawana pesa ya kulipa. Kutokuwa na pesa ya kulipa na kukataa kulipa ni vitu tofauti.

Vilevile kuna kipengele wamekikubali cha kuwabana waweke pesa katika akaunti za Tanzania. Hapo ndipo asilimia 50 ya Tanzania, kodi na hilo suala la kuwa wana hela ya kulipa au hawana litakapojulikana kirahisi.

Mungu Ibariki Tanzania!
Tulishaambiwa hao ni wezi. Huu utamaduni wa kujadiliana na mwizi umeanza lini? Hiyo ni sifa ya mtu mwoga na asiyejiamini.
 
Usiwadanganye watu. Kasome taarifa ya Barrick. Msipende kujifariji. Hakuna wizi uliothibitika, hakuna udanganyifu uliothibitika wala kodi iliyokwepwa.

Taarifa ya Barrick imesema wazi kuwa tumekubali kuipa Tanzania malipo ya MARA MOJA dola milioni 300 in good faith. Kitu unachopewa in good faith ni pale inapodhihirika huna stahili lakini anayekupa anataka mwendelee kuwa na uhusiano mzuri.

Mazungumzo yatakayoendelea hayahusiani na dola billion 190, yatahusu kufuta kesi na utaratibu wa kutolewa hizo dola milioni 300.

Na Rais aliweka wazi kuwa 'watupatie hizo milioni 300, hawa sasa ni ndugu zetu, tutafanya kazi pamoja, na watu mkishakuwa ndugu mnafanya kazi pamoja. Barrick is here to stay'. Hayo uliyasikia au unajifanya hukuelewa?

Kumbe ile mitihani ya open book watu wanafeli kweli!

Na wewe kajifunze kingereza. Profesa Thornton kalihutubia taifa kwamba suala la deni la kodi ni gumu na bado hawajafikia muafaka. Hivyo basi wameaumua kutengeneza timu/tume ya pande zote mbili kufuatilia suala hilo.
Kuonyesha nia njema ya kuendelea na mazungumzo ndio wameamua kutoa hizo bilioni saba.
 
Accacia ndio katuletea matatizo na kuibiwa wote wawili watanzania na barrick. Barrick kumwambia accacia alipe hizo dola milioni 300 ni kumwbia live yaani wewe bwege accacia ulikula hadi kodi za serikali? Lipa halafu mengine tutamalizana mimi na wewe yanayohusu ulichoniibia mimi barrick. Accacia alikuwa akiiba kote anasafirisha kontaine mfano 20 kwetu analaghai kasafirisha nane akifika kwa barrick anawadanganya kuwa kasafirisha kumi yaliyozidi anapeleka nchi nyingine pesa anaweka kibindoni. Ndio maana barrick waliungana na magufuli alipoitisha uhakiki wa kontaina zilizosafirisha na kilichomo Wakasema tuwe pamoja kwenye hili. Akina accacia wakaanza propaganda za kukwepa hilo ndio wakaanza kuhonga wanasiasa Kama Lisu Na chadema na akina Zitto kabwe kama ngome yao ya defence ya kuwalinda vibaka baada ya kuwaona kuwa wananunulika kirahisi kutokana na uchunguzi waliofanya waliogundua. Kila fisadi ni rahisi kununua mwanasiasa yeyote wa chadema Na kuwafanya watetezi wao. Awe fisadi au jambazi la kibiti laweza kuwahonga kesho likipigwa risasi chadema utakuta tayari wanaibuka kulaani jambazi la kibiti kujeruhiwa ukucha lakini polisi hata kumi wakiuawa husikii chadema Kutoa tamko hata pole kisa polisi hawajawapa rushwa Kama majambazi
Tatizo lako inaonekana huna kumbukumbu nzuri. ni hivi, Barrick Gold ndiyo walioanzisha "African Barrick Gold" ambayo baadaye ilikuja kubadili jina kuwa "Acacia Mining". kimsingi hii ni mali ya Barrick Gold. unaweza kujiuliza iweje Acacia hawana nafasi kwenye majadiliano, lakini linapokuja suala la kulipa inabidi Acacia ndio waidhinishe? Kwa nini Acacia wasishiriki majadiliano ili wakikubaliana waende kwenye utekelezaji moja kwa moja? na kwa nini basi huo uidhinishaji haukukamilishwa kwanza kabla ya kujitokeza na hiyo "good faith" gesture?

kwa kifupi ni kwamba something is very wrong here, na ufumbuzi siyo kushangilia, bali kujipanga. lakini tunajipangaje kama tunalaumiana tu badala ya kukaa pamoja kama watanzania? Approach ya Magu ni divisive. hatambui mchango wa wapinzani miaka yote, ambao walimpinga Mkapa alipoanza hii mikataba feki. hatambui hata mchango wa JK katika kurekebisha mikataba hii. umoja ni muhimu, lakini unahitaji kufanyiwa kazi, siyo tu kubeza wengine na kuwaita wasaliti
 
Mzungu kasema hivi:

"All these arrangements need to be approved by the independent shareholders and independent directors of our 64% owned London listed subsidiary Acacia".

Hapo hata yule mkalimani alichapia kidogo akasema hao wakurugenzi na wenye hisa ndio wanaomiliki asilimia 64.

Usahihi ni kuwa Barrick wanamiliki asilimia 64. Na Acacia ni tawi la Barrick.

Mkumbuke mchanga ulipokamatwa muhusika mkuu mwenye mali alikuja mwenyewe Dar kuuliza kulikoni?
Hivyo ni sawa makubaliano haya kufanywa kati ya Tanzania na Barrick.

Kama Acacia hawana hela ya kulipa hilo litakuwa deni ni tofauti na kusema hawataki kulipa.

Hivi daladala likifutiwa leseni anayeenda polisi ni mwenye daladala au dereva?
 
Ni hivi, jamaa wamekubali wanadaiwa malimbikizo ya kodi. Lakini hawajakubaliana wanadaiwa ngapi. Mazungumzo yanaendelea na nyaraka zinapitiwa.

Ila kwa kuonyesha kuwa muafaka ukifikiwa wa hilo deni watalipa ndio wakatoa hicho kishika uchumba cha bilioni 700.

Na sijui makubaliano kamili lakini hizo bilioni 700 zinaweza kutolewa katika deni lao kamili wanalodaiwa siku wakifikia muafaka(makubaliano)

Nafikiri wewe ulikuwa unasikiliza ulichotaka kusikia. Ni nani amesema na ni wapi umesikia kwamba wamekubali wanadaiwa malimbikizo ya kodi? Hata Kabudi na Magufuli hawakusema hivyo. Wamefurahi tu kwamba Barick wamekubali kufuata sheria yetu mpya ya madini na kugawana 'economic benefits' 50/50. Na fidia ni nini? Kwa hiyo Tsh. 700 billion si "good faith" tena bali ni sehemu ya malipo ya malimbikizo ya kodi/mrahaba?
 
14. Suala la fidia lilikuwa suala gumu sana na ndilo lililochukua muda mrefu lazima tupitie nyaraka, ila wamekubali kutoa dola milioni 300 wakati mazungumzo ya jambo hilo YANAENDELEA.......
- Profesa Kabudi

Na kwenye kingereza profesa Thornton kasema wazi suala la kodi lilikuwa na kutokukubaliana na wameanzisha tume ya pande zote mbili kutafuta ufumbuzi.
Ila wametoa hizo milioni mia tatu in good faith. Tafuta kwa lugha yeyote good faith payment ni sehemu ya deni anayodaiwa mdeni au mnunuzi.
 
Back
Top Bottom