Gonjwa la Corona: Waziri wa Afya mbona unazidi kutuchanganya? Wananchi wanataka elimu sio matamko

lakini jamani mzizi mkuu wa shida ni elimu yetu, tunazalisha watu vilaza sana, hasa zaidi WASIOJIAMINI KABISA unakuta mtu ana Phd lakini ni balaa tupu, au ni umaskini jamani?? kwa sababu me naona ni mtu kaweka ubongo wake pembeni kabisa!

Mpaka hapa kweli anamtegea rais ndo awe msemaji wa mwisho wakati yy ndo anatakiwa kua kinara wa mapambano zidi ya covid 19! Kuna shida sana kwenye elimu yetu! Cha ajabu wizara ya elimu inaongozwa na prof!

Tunahitaji mageuzi kwenye elimu la sivyo tutakula tabu sana
 
Huyu mama muda wake wote anautumia kwa mambo mawili tu:

1) Kugombana na kuwadhalilisha wafamasia.

2) Kuwa mwangwi (echo chamber) wa Jiwe.

Sidhani anafahamu hata wajibu wa Waziri wa Afya ni upi.
 
Nimepigwa na butwaa kusikia Waziri wa Afya akisema kuwa matamko juu ya Covid 19 basi. Maana viongozi wakuu wameshatoa matamko sasa kila mtu achukue wajibu wa kujilinda..
Hawa watu ni kama vile wako Nolywood wanajaribu kuandika scripti ya muvi wasiyoijua! Mheshimiwa wa Mbeya yeye anasema serikali imetumia pesa nyingi sana kujenga hosipitali hivyo zinatakiwa zijae wagonjwa!

Kama ambavyo baa inavyotakiwa kujaa walevi na shamba linavyotakiwa lijae wakulima. Waacheni watu waugue kwa wingi ili wazijaze hosipitali! Hakuna mama yake korona wala shangazi yake korona hapa.
 
Hawa watu ni kama vile wako Nolywood wanajaribu kuandika scipti ya muvi wasiyoijua! Mheshimiwa wa Mbeya yeye anasema serikali imetumia pesa nyingine sana kujenga hosipitali hivyo zinatakiwa zijae wagonjwa!
Huyu Rc hayupo sawa kiakili.
 
Mbona ukimwi watu wanakumbushwa kila siku kujikinga, huyu mama analichukulia hili swala la corona lightly.
Ingekuwa hivyo mahubiri/mawaidha yasingetolewa basi watu si wanajua nn makosa mbele ya mungu mbona wanahubiriwa lila siku????
 
Nimepigwa na butwaa kusikia Waziri wa Afya akisema kuwa matamko juu ya Covid 19 basi. Maana viongozi wakuu wameshatoa matamko sasa kila mtu achukue wajibu wa kujilinda.

Hivi hili gonjwa linahitaji matamko au elimu endelevu na kukumbusha wananchi kuwa makini mara kwa mara?

Wewe kama waziri mwenye dhamana na afya za Watanzania, unalichukulia vipi hili gonjwa?

Kwamba waziri mkuu na rais wakisema watu wavae barako na kunawa mikono ndio inatosha?

Wewe ni mwenye dhamana na afya za Watanzania, kuwa makini na jinsi unavyolichukulia poa hili gonjwa
Ni mgum Sana kumuelewa huyu mama, mfano anakuja na HOJA kwamba Kuna ubadhilifu wa dawa, hivi kwani kabla ya yeye hapakuepo mawazari ,au ndo ile kuona yeye ni mchapa kazi kuliko watangulizi wake, anaivuruga Sana wizara hii,
Tatua tatizo kwanza lililo mbele YAKO ndo uje na lingine,hii formula viongozi wetu huwa hawajui ? Na shule walienda fanya nini?
Mama wizara ilisha mshinda
 
Ni mgum Sana kumuelewa huyu mama, mfano anakuja na HOJA kwamba Kuna ubadhilifu wa dawa, hivi kwani kabla ya yeye hapakuepo mawazari ,au ndo ile kuona yeye ni mchapa kazi kuliko watangulizi wake, anaivuruga Sana wizara hii,
Tatua tatizo kwanza lililo mbele YAKO ndo uje na lingine,hii formula viongozi wetu huwa hawajui ? Na shule walienda fanya nini?
Mama wizara ilisha mshinda
Amna mtu anayeiba dawa za serikali ni hapo mtu amesashu kudocmetn akamapa mgonjwa dawa basi huo ni wizi
 
Amna mtu anayeiba dawa za serikali ni hapo mtu amesashu kudocmetn akamapa mgonjwa dawa basi huo ni wizi
Hawaelewi mkuu ,wapo kutafuta sifa, uteuzi wa wizara nyeti mfano afya sio wakufanya haraka, mtu analeta siasa za ajabu Mara utasikia eti kila kituo kiwe na ilani ya chama,so ilani ndo inatibu wagonjwa, Mambo ya ajabu Sana yanatokea tz,
 
Huyu waziri hana weledi wa kazi hata kdg, ni mkurupukaji na tuendako ataleta hasara sana kwa taifa. Hawa anaowatimua kazi kwa kukurupuka itamtokea puani.
 
Back
Top Bottom