Goli ni Goli; la Mpendazoe nalo Goli!

Mtu B
Wewe ndio bado uko usingizini kabisa naona hujui hata kinachoendelea wake up please kumekucha afadhali u qoute maneno ya Msekwa kuliko unavyosema movie hii ni tofauti na ya enzi za Mrema.

Hii case inafanana na ya Mrema kabisa. Bahati mbaya kwa huyu bwana Mpendazoe ni kwamba hana hata 1% ya umaarufu na nguvu za kisiasa alizokuwa nazo Mrema wakati ule alipotoka CCM. Ndio maana nasema imekula kwake, amefulia, mark my words.

Besides, hiyo CCJ aliyoingia ndiyo itakayompoteza kabisa nje ya ulingo, maana haina hata sifa za kushiriki uchaguzi mkuu mwaka huu, na haitazipata kabla ya uchaguzi huu kwisha. Na hiyo CCJ itakapopata usajili wa kudumu mwaka kesho, Mpendazoe atakuwa ameshasahaulika! Amefulia.
 
Niliona sura ya Msekwa wakati wa mahojiano yake. Sura ilikuwa inasema mengi kuliko kauli yake ya mdomoni. WAKO KATIKA WAKATI MGUMU
 
Mie kumsingi naamini Mpendazoe kachemsha. Ninazo sababu:-

  1. Alitakiwa kuupinga ufisadi akiwa ndani ya CCM. Nje ni kujimaliza kisiasa.
  2. Mtu yeyote anayegombea ubunge huwa ana dhamira mbili. Moja ni kuwa na nafasi ya kupata kipato zaidi (kwa maana ya mshahara zaidi, heshima zaidi kwa kuitwa mheshimiwa na cheo zaidi ikiwa atapewa uwaziri au mamlaka mengine) na mbili ni "kuwatumikia wananchi". Sasa ku sacrifice haki ya kikatiba ya zaidi shilingi 40m/= kwa muda aliotumia kuwatumikia wananchi ni kuchemsha. Labda huko alikoenda amepata zaidi ya hizo (kitu ambacho kitakuwa ni rushwa).
  3. Kama alikuwa na dhamira halisi ya kuhama chama ili baadae aendelee kuwatumikia wanachi kwa kugombea tena ubunge akapata angehamia chama kingine cha kudumu, na sio kwenda kwenye chama ambacho hana uhakika kama kitapata isajili wa kudumu.
  4. Akumbuke mbunge sio kada wa chama. Makada wa chama wana wafuasi ndani ya chama husika. Chama huteua wanachama wake ili wakiwalishe katika uchaguzi fulani kulingana na upepo unavyovuma kwenye jimbo hilo la uchanguzi. Na moja ya sharti la kuteuliwa kugombea ni kuikitumikia, kukishabikia na kukubaliana na maamuzi yote ya chama. Ndio maana kina Wasira waliweza kuhama chama na waliporudi wakpokelewa kwa mikono miwili. Ni upepo tu. Kwa bahati mbaya hana influence ya kuwafanya wana Kishapu kuhamia CCJ. Heri Dan Makanga na UDP vs CCM kule Baridi enzi hizo.
  5. Kajifunga goli. atasononeka. atabaki peke yake.
  6. Kachemsha ile mbaya. Kimsingi huo ndio mwisho wake kisiasa.
Hofu yangu ni moja. Inawezekana Mpendazoe alikuwa anatishwa kimya kimya na dola na vitisho vyenyewe alikuwa anajua vitamdhuru. Akaona akimbie.
 
Mie kumsingi naamini Mpendazoe kachemsha. Ninazo sababu:-

  1. Alitakiwa kuupinga ufisadi akiwa ndani ya CCM. Nje ni kujimaliza kisiasa.
atapingaje ufisadi akiwa CCM ambamo kamati na Halmashauri kuu ambao kimsingi ni mabosi zake ktk chama wanaunga mkono ufisadi, halmashauri kuu ndio kabisaaa , mafisadi papa Ruundo.
 
Hii case inafanana na ya Mrema kabisa. Bahati mbaya kwa huyu bwana Mpendazoe ni kwamba hana hata 1% ya umaarufu na nguvu za kisiasa alizokuwa nazo Mrema wakati ule alipotoka CCM. Ndio maana nasema imekula kwake, amefulia, mark my words.

Besides, hiyo CCJ aliyoingia ndiyo itakayompoteza kabisa nje ya ulingo, maana haina hata sifa za kushiriki uchaguzi mkuu mwaka huu, na haitazipata kabla ya uchaguzi huu kwisha. Na hiyo CCJ itakapopata usajili wa kudumu mwaka kesho, Mpendazoe atakuwa ameshasahaulika! Amefulia.
Wakati Mrema anatoka CCM hakuwa anajua atajiunga chama gani alikuwa anafuatwa na kila chama tofauti na huyu kwanza anaonekana hataki umaarufu kama wa Mrema halafu Mpendazoe inaonekana alijiandaa mapema kwenda CCJ hata baadhi ya watu walibashiri hivyo.
 
Hiyo imetulia, na wengine wamfuate. wawaachie waliokunywa maji ya bendera ya kijani
 
Wakati Mrema anatoka CCM hakuwa anajua atajiunga chama gani alikuwa anafuatwa na kila chama tofauti na huyu kwanza anaonekana hataki umaarufu kama wa Mrema halafu Mpendazoe inaonekana alijiandaa mapema kwenda CCJ hata baadhi ya watu walibashiri hivyo.

Mrema alikuwa na impact kubwa mno kwa CCM, na laiti angetoka wakati Nyerere hayupo angechukuwa nchi.

Kilichoiokoa CCM wakati huo ni Nyerere, maana kila mtanzania alikuwa anamuheshimu Nyerere na kafimbo kake.

Nakumbuka pale nyamagana tulimuzomea Nyerere alipoingia na Mkapa, lakini aliponyosha kafimbo kake kasi, mara kusi ,mara mangaribhi na mashariki, tukatuliza soka kumsikiliza.
Aliyeiokowa CCM kipindi hicho ni Nyerere, ktk kipindi hiki hakuna mwenye madaluga wa kutuliza mizuka kama alivyofanya Nyerere.

Watu potential wamo mle ccm wa kumtikisa JK, Lakini sijui wanaogopa nini kufanya kweli.
Mtu kama una Ph.D naamini hata ukiwa bench hutofulia sana.Mrema amefulia kwa sababu alikuwa na diploma.
 
Wakati Mrema anatoka CCM hakuwa anajua atajiunga chama gani alikuwa anafuatwa na kila chama tofauti na huyu kwanza anaonekana hataki umaarufu kama wa Mrema halafu Mpendazoe inaonekana alijiandaa mapema kwenda CCJ hata baadhi ya watu walibashiri hivyo.

Hataki umaarufu, kwa hiyo anataka nini? Kama hataki umaarufu mbona kaitisha mkutano wa waandishi wa habari kuwajuza kuhusu kuhama kwake? Umaarufu anautaka sana, na anataka agombee tena huko Kishapu. Ingekuwa hataki umaarufu, angesubiri muda wake uishe wa ubunge kipindi hiki, halafu asigombee, aende huko CCJ kimyakimya, habari tungezipata tu bila yeye kuitisha mkutano.

Sasa habari ya ubunge tena ndio asahau, maana hiyo CCJ itapata usajili wa kudumu baada ya uchaguzi mkuu, labda mwaka ujao au hata baadaye.

Amefulia
 
Ndiyo maana nikuambia bado umelala hujui kinachoendelea goli ni goli hata la mkono(maradona) ni goli yanayobaki ni maelezo ya hilo goli kama tunayojaribu ku speculate hapa hatashinda ubunge tena, labda alitaka kufukuzwa, CCJ is a hoax nk
 
......

Wait a minute, kwani Mpendazoe kupoteza ubunge baada kuhamia CCJ na kwamba hatagombea ubunge ndio kufanya awe kafulia?
 
Kwa sasa wapo wanaotaka kujitoa lakini wanapima joto. Mara baada ya kura za maoni itakuwa shughuli kamili.
 
Wait a minute, kwani Mpendazoe kupoteza ubunge baada kuhamia CCJ na kwamba hatagombea ubunge ndio kufanya awe kafulia?

Amefulia kwa sababu hicho anachodai anapigania hatafanikiwa katika hiyo CCJ. Na kwa style aliyotoka nayo, kajinyima kabisa ukumbi wa kuendeleza mapambano. Kwa hiyo amefulia
 
Ndiyo maana nikuambia bado umelala hujui kinachoendelea goli ni goli hata la mkono(maradona) ni goli yanayobaki ni maelezo ya hilo goli kama tunayojaribu ku speculate hapa hatashinda ubunge tena, labda alitaka kufukuzwa, CCJ is a hoax nk

Kinachoendelea nakielewa. Kajitoa CCM kwa kuwa chama kina mafisadi, anataka kupambana nao. Huko alikoenda amekwenda kujifukia, kujinyima kabisa uwezo na hata ulingo wa mapambano, ataishia kuwa mtazamaji tu na mlalamishi asiyekuwa na impact yoyote. Amefulia.
 
Amefulia kwa sababu hicho anachodai anapigania hatafanikiwa katika hiyo CCJ. Na kwa style aliyotoka nayo, kajinyima kabisa ukumbi wa kuendeleza mapambano. Kwa hiyo amefulia

Nadhani Mpendazoe ameonyesha kuwa ni mpambanaji wa ukweli. Kupigania watanzania sio lazima uwe mbunge.

Mpendazoe, ameanzisha njia kutuonyesha wapiganaji wa kweli, walio tayari kuachia viti vya ubunge, mafao ya ubunge na vingine vyote ili kupigania haki na maendeleo ya Mtanzania.

Mpiganaji au mpambanaji wa kweli, hanyamazi, hapoonzwi kwa cheo wala mali.

Hongera sana ndugu Mpendazoe, Mungu akuongoze katika kufanikisha yale uliyoyadhamiria.
 
Hataki umaarufu, kwa hiyo anataka nini? Kama hataki umaarufu mbona kaitisha mkutano wa waandishi wa habari kuwajuza kuhusu kuhama kwake? Umaarufu anautaka sana, na anataka agombee tena huko Kishapu. Ingekuwa hataki umaarufu, angesubiri muda wake uishe wa ubunge kipindi hiki, halafu asigombee, aende huko CCJ kimyakimya, habari tungezipata tu bila yeye kuitisha mkutano.

Sasa habari ya ubunge tena ndio asahau, maana hiyo CCJ itapata usajili wa kudumu baada ya uchaguzi mkuu, labda mwaka ujao au hata baadaye.

Amefulia

nani alikwambia kuita waandishi wa habari ni kutafuta umaarufu?!! we nawe... usiandike ili kuongeza idadi za thread zako hapa. wewe unafikiri wakati anachukua uamuz wa kahama chama cha wezi na kwenda ccj alikuwa hajui kuwa hicho chama hakina usajili wa kudumu??!
kama amediliki kuacha ubunge na alikuwa mbenge halali unadhani mchezo ee! mara ohh huyu kama mrema.... wa wapi wewe bado una mawazo ya 1994? mrema na huyu ni tofauti kwa kila kitu.
Usitulilie badae!!
 
Harakati za Makamba na UVCCM kusafishana na kutishiana zinatakiwa zioneshwe na majasiri wengine kama Mpendazoe, watoke na kujiunga upinzani bila woga wa kifilisiwa na chama tawala, upinzani upate nguvu na CCM iwe chama cha Upinzani
 
Wameshasema eti hakuwahi kuongoza hata shina. Shem on them.

Hi sanaa jamani .kwani jimbo sie sehemu aliyoiongoza huyu mh.?na nimesoma kwenye gazeti moja Msekwa kasema anashangaa kuitwa kigogo,kigogo alikuwa mrema si Mpendazoe.
 
Hii case inafanana na ya Mrema kabisa. Bahati mbaya kwa huyu bwana Mpendazoe ni kwamba hana hata 1% ya umaarufu na nguvu za kisiasa alizokuwa nazo Mrema wakati ule alipotoka CCM. Ndio maana nasema imekula kwake, amefulia, mark my words.

Besides, hiyo CCJ aliyoingia ndiyo itakayompoteza kabisa nje ya ulingo, maana haina hata sifa za kushiriki uchaguzi mkuu mwaka huu, na haitazipata kabla ya uchaguzi huu kwisha. Na hiyo CCJ itakapopata usajili wa kudumu mwaka kesho, Mpendazoe atakuwa ameshasahaulika! Amefulia.

ref_cornerkick_shadowgram.gif
 
Back
Top Bottom