Goli ni Goli; la Mpendazoe nalo Goli!

yani mzee mwanakijiji hoya yako ulivyoiwakilisha yani mbavu sina mana umeieleza jinsi ilivyo kisahihi kabisa ata mjinga lazima aelewe. lingine ni majibu ya katibu mkuu wa ccm wakati anahojiwa na wapo radio hakika ni pigo kwao kwa jinsi mzee anavyopenda kuropoka lakini jana alivyokuwa anajibu ungecheka ila jibu kubwa alisema aliingia ccm kwa hiari yake mwenyewe na ameondoka kwa hiari yake mwenyewe na ushindi ni lazima ccm
 
unajua ni pigo sana kwa ccm hata waseme vipi.

kwanza huyu jamaa alikuwa mbunge, lakini kachoshwa na mambo ya ccm,

lazima kaona kuna tatizo mahali ndo maana kaamua kuchukua maamuz mazito kama haya. safi sana mpendazoe. na nilipenda kauli yako uliposma ccm sio mama yako Helena.
 
halafu jamaa alikuwa underground sana, sikuwahi kumsikia kama hao waengine wanafiki wakubwa kila siku gazetinina kwenye Matv, huyu kafanya maamuzi sahii kabisa, kuacha marupurupu si mchezo na mwezi wa ngapai pale wanalipwa mamilioni ya tsh kama wabunge,

namsubiri shibuda maana nasikia wanampiga vita sana.
 
Hili Goli halijawakera CCM peke yao linakera hata kwa baadhi ya vyama vya upinzani.Hili gaoli limekuja kwa wakati mbaya sana na linatishia usalama wa wachezaji wa timu nyingine.
 
Wenye ujasiri huo sio wengi. Nimemshangaa sana Selelii remarks yake kwamba Mpendazoe angemtaka ushauri angemwambia asiondoke na kwamba yeye hatatoka CCM. Wengi ni aina hiyo ya kuganga njaa na hawajui wanatetea nini.

Big up Mpendazoe.
Seleli kusema hataondoka CCM ni siasa tu hata Mpendazoe majuzi alikana hivyo hivyo kwa hiyo Mchili dont take them seriously
 
Currently Active Users Viewing This Thread: 106 (39 members and 67 guests)
Edson, MIGNON, Luteni, Kungurumweupe, Einstein, Prodigal Son, mzeewadriver, afande samwel, CarthbertL, jethro, Kenge (Eng), sosoliso, Pilato2006, Madikizela, Tangawizi, Don Cicci, Nandoa, Mpita Njia, Kibuja, Milindi, Mubii, MWANALUGALI, Democrasia, Mtu66, consigliori, nkosikazi, Mfuatiliaji, M-bongo, Rugas, Kiraka, Saharavoice, Mzee Mwanakijiji, Bobby, iramusm, Lusyonja, Bramo, MC, nyakyegi, Kufakunoga
 
Awe na ajenda ya siri moyoni kwake, au ametumwa kweli na dhamira yake..silihuhukumu kwa sasa. Ninapenda kuangalia impact ya kitendo chake..Ameweza kuonyesha njia..Ningependa kama watanzania wote watakichukulia kitendo hiki in a positive way..na iwe chachu kama ni kweli tunataka kuleta mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi katika taifa letu..Mpendazoe ameonyesha njia..sisi nasi tunatakiwa tumuunge mkono kwa vitendo..Nadhani vijana tuna sehemu kubwa sana ya ku-play..Nafasi ndio hii....Big up Mpendazoe!!:D
 
Hilo goli la Mpendazoe kajifunga mwenyewe. Yaani imekula kwake.
Mtu B
Wewe ndio bado uko usingizini kabisa naona hujui hata kinachoendelea wake up please kumekucha afadhali u qoute maneno ya Msekwa kuliko unavyosema movie hii ni tofauti na ya enzi za Mrema.
 
In real life sometimes its possible to be caught off-guard as it appears to CCM...!
 

Attachments

  • off guard.jpg
    off guard.jpg
    25.1 KB · Views: 28
Mpendazoe hajaifungaCCM goli bali amejifunga mwenyewe kwenye mechi isiyokuwa na referee.Huo umaarufu wa mpendazoe unaodaiwa na watu si chochote kwani wanaoona kama ni maarufu ni watu wa aina yake na wale wengine wanaojiita mashujaa wa kupambana na ufusadi.Lakini kama ni mkweli mbona hawajaeleza hao wanatuhumiwa na ufisadi wamefanya nini na kuthibitisha tuhuma hizo.kilichosikika ni kelele za mbwa mwoga tuu.tena kwa mtuu yeyote makini hakuna mchango wowote wa maendeleo walioufanya aidha katika majimbo yao na hata katika chama chao katika ngazi ya wilaya.Hasara walioifanya katika majimbo yao ni kujenga makundi tuu.Let them go na hao wengine.
Nani kakwambia Mpendazoe anatafuta umaarufu yeye katoka kimya kimya alichofanya ni kusimama kuhesabiwa tu CCM ndio wanaohaha na maneno kibao na wewe pia umejinga nao sizitaki mbichi hizi
 
Utasiki benchi la ufundi likiongozwa na Msekwa,makamba,chiligati,tambwe na wengineo watakavyotoa mneno ya kukata tamaa

Walioko CCM kama ni wapambanaji kweli watoke na wasitegemee kusifiwa na CCM yenyewe
 
Mpendazoe amefanya kile anachokiaona kwake inamfaa. tukumbuke kuwa hadi sasa jamaa anaongoza kwa goli, ccm sifuri. Labda waje na janja nyingine.
 
Namfagilia Mpendazoe, ila kwa maoni yangu, angejiunga CHADEMA. CHADEMA ipo imara sana ukilinganisha na vyama vingine.
 
CCM ni kama JF unaingia mwenyewe kwa hiyari yako na ukiona umechoka unatoka na kuwaachia wengine waendeze libeneke. Mimi binafsi ninamtakia kila la heri huko alipokwenda ana haki ya kutumia uhuru wake wa kujihusisha na chama au jamii yeyote bila ya kuvunja sheria za nchi.
Kidumu Chama Cha Mapinduzi
 
Ni Jambo la kawaida kuhama kutoka chama kimoja hadi nyingine...Kwani Mpendazoe ni nani kiasi cha kushabikia? Tatizo letu Watanzania tunaongea sana kuliko vitendo! CCM mnaijua, vyama vya upinzani mnaijua....wangapi wamekihama CCM? Tusubiri tuone mwisho wa huyo Mpendazoe na wengine watakao kihama CCM. Ofcoz watakosa mwelekeo mwisho wataishia mitaani! Mimi siyo mwanaccm lakini mkubali msikubali CCM chama KUBWA SANA!
 
Kazi ipo. Kuna kitu MMKJ umekisema lazima watu tuwe makini.....kule CCM kuna watu walisomea kozi za propaganda.Tutaanza kuona matumizi yake kipindi hiki
 
Maneno mazito, makini na kweli tupu. Sio yangu ila ni ya Mpendazoe

"Nasononeka CCM imegeuka gulio la kila mtafuta cheo na utajiri haramu. CCM imegeuka kimbilio la kila mwenye dhamira ya ulanguzi. CCM imepoteza maadili ya uongozi na imekuwa ngome ya mafisadi wanaotafuna utajiri wa nchi yetu. Natoka CCM na sijutii uamuzi wangu," aliongeza.
 
Hapa kwa kweli Mzee Mwanakijiji umesema, sijui hawa CM watatueleza nina propaganda zao, ni wakati wa Vitendo na wala si swala la kusubiria.

Hongera sana Mpendazoe kwa kuonyesha njia, wengi watakufuata.


Watakwambia hana impact! huo Msekwa anashangaa waandishi kusema kigogo wa CCM amehama chama?
 
Back
Top Bottom