Goli ni Goli; la Mpendazoe nalo Goli!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,476
39,995
GOLI NI GOLI HATA LA MPENDAZOE NALO GOLI!

Na. M. M. Mwanakijiji


Kwenye kandakanda kuna magoli yanaudhi sana na yanakera. Kuna magoli ambayo mtu unakubali tu kuwa goli hilo "halina utata" na mnajitahidi kurudisha majibu.

Lakini, wakati mwingine magoli mengine yanamfanya mtu usikie donge kooni, presha ipande na kushuka na hata kuna mengine yanaweza kufanya timu nzima muende kumzonga mwamuzi kwani goli lililokubaliwa linaonekana kama limependelewa.

Bahati mbaya goli ni goli liwe la kuudhi au kukera lakini alimradi limekubaliwa basi wakati wengine wanasikia machungu wajue kabisa ipo timu nyingine inashangilia hata kama na wao wanaona kwa kweli lile goli lilikuwa baya.

Mbunge wa Kishapu Mhe. Fred Mpendazoe kawafunga bao CCM tena bao la kuudhi, kukera, kupandisha hasira na kwa kila kipimo bao ambalo CCM ile ya zamani isingeweza kufungwa kijinga hivi. Bao alilowafunga naweza kulilinganisha na bao la "tobo" au linakaribiana na bao la kipa "kupigwa kanzu"! Mwingine anaweza kusema "kapigwa kanzu halafu akapigwa tobo".

Kujiondoa kwa Mpendazoe kutoka Chama cha Mapinduzi kwa sababu yeyote ile kwa namna aliyotoka kunatufanya tusubiri kwa hamu maelezo ya CCM ya kutufafanulia kwanini goli hili siyo goli.Chama cha Mapinduzi bila ya shaka ambacho kina wasomi na watu waliobobea katika propaganda ya uzugaji kwa maneno kinakaribiwa na wakati mgumu wa kuelezea kujiondoa kwa Mpendazoe na bila ya shaka wanachama wengine huko mbeleni.

ref_cornerkick_shadowgram.gif

 

Attachments

  • GOLI NI GOLI HATA LA MPENDAZOE NALO GOLI.doc
    40 KB · Views: 321
Hapa kwa kweli Mzee Mwanakijiji umesema, sijui hawa CM watatueleza nina propaganda zao, ni wakati wa Vitendo na wala si swala la kusubiria.

Hongera sana Mpendazoe kwa kuonyesha njia, wengi watakufuata.
 
ndiyo inaitwa sanaa ya uzugaji.. sitoshangaa vijana wa CCM watakuwa wa kwanza kuandamana kumpinga.. halafu kabla hawajameza mate.. mwingine naye anachomoka..
 
Mhhhhh ila sina hakika sana wangapi watamfuata !!! watu wengi walioko CCM ni wezi, mafisadi nk, nk. wanajuwa wakienda vyama vingine hawatapata nafasi za kuibaaaaaaaaaa kwa hiyo wanaona ni bora wakae huko huko CCM waendelee kutuibiaaaaaa mpaka mwisho wa dunia. Wakihama CCM watoto wao hawatasoma nje, na mambo mengi ya maisha ya kifahari hayatakuwepo, wako CCM siyo kwasasababu wanaipenda ni kwa ajili ya masilahi yao tuu, na wala siyo masilahi ya watanzania upo hapo!
 
Eti alikuwa mzigo..... Lol

Lazima maumivu wanayasikilizia. ukiachana na hilo huyu Mh. kawamaliza sana manake ni kama timu mnaongoza mpaka dakika ya 90 then kwenye majeruhi jamaa wanarudisha na kuongeza bao. Natumaini CCM watakuja na hoja za msingi. Subiri siku moja ambapo vijana wa kitanzania watakapoamua kukipa talaka chama hiki hilo litakuwa sio tena bao bali gharika.
 
Ningeweza kuzaliwa zama za kina Hitler na leo hii nisingekuwa hai. Namshukuru mwenyezi Mungu kwa kuwa hai leo hii kushuhudia Game za kuvutia na za nguvu katika mwaka huu 2010.

Kombe la dunia limeshaanza tayari, pop corn zangu mkononi, big screen mbele, Brazil hawajaingia bado, CCJ nawaona wako uwanjani ni timu mpya haijaota meno bado lakini tayari wameshakata kipande cha nyama ya nyati kwa ufizi.

Nina hamu ya kushuhudia mengi. Hili jamvi mwaka huu litapendeza mno. Yaani ni raha tupu, kesho nasikia nanihii naye anapiga bao, nanihii, yule mzee wa 'siogopi'

Mwaka huu unachagua unataka raha au utamu?
 
Tambwe Hiza nae anadiriki kusema kutoka kwa Mpendazoe ni faraja kwa CCM! Watu kama Mpendazoe wakiondoka kutakisaidia Chama kufanya kazi zake bila matatizo! Hii ni sawa na kusema wanakerwa sana na wanachama wanaowabana kuwa wasafi wakati wao hawataki. Hata hivyo huyu ni Tambwe Hizza, si la kushangaza sana
 
Mpendazoe kaonyesha njia, tunasubiri na wengine wenye ujasiri wachomoke kutoka sisisem!
 
wana propaganda wao wanahaha, kwanza walisema kuwa hakuna mwanaCCM atakae jiunga na CCJ, mara wakadai CCJ si tishio kwao, na jana wamekaririwa wakidai kuvuja kwa pakacha nafuu ya mchukuzi, wakati hayo yakiendelea Tabwe Hiza anadai ni heri kuondoka kwake maana alikua hajui taratibu za chama, haeshimu vikao wala viongozi wake....kwakweli kunamtatiziko ndani ya cHAMA, Macho yote yanamwangalia Sitta na wapiganaji wengine.
Hongera Mpendazoe, haina maana kupigana na Mafisadi papa wakati ukiwa chama kimoja na Lowasa,RA,Manji,Makamba na wengine wa kariba hiyo.
Goli ni goli, bora refa kanyosha mkono kati.
 
nyie subirini tu mwisho watabakia wenyewe humo ndani wote wachafu huku wakiendelea kuimbiana "wewe msafi, mimi msafi, sote wasafi ye ye ye"!!
 
nyie subirini tu mwisho watabakia wenyewe humo ndani wote wachafu huku wakiendelea kuimbiana "wewe msafi, mimi msafi, sote wasafi ye ye ye"!!

Hapa sina cha kuongeza, nimei'quote ili niisome tena na tena. Yaani verse utafikiri msaafu......duh! Nagonga thanks kama bilioni sita hivi za kampeni ya urais kwako MM.
 
nyie subirini tu mwisho watabakia wenyewe humo ndani wote wachafu huku wakiendelea kuimbiana "wewe msafi, mimi msafi, sote wasafi ye ye ye"!!
Makamba, Karamagi, Lowassa,Manji, Rostam Aziz, Peter Serukamba, wataungana na Mkapa, Yona.....orodha yao ni ndeefu saana....ni ulaji na ulaji tu.,kwao taifa si kitu ila mkate wao wa kila siku.
 
Back
Top Bottom