Goldsmith akiri kubadilisha mawazo

Goldsmith akiri kubadilisha mawazo

Herbalist Dr MziziMkavu

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,069
Reaction score
34,836
t.gif
20080315151317lord-goldsmith.jpg

Lord Goldsmith alifikiria sababu ya kujihami haikuwa kigezo tosha kuishambulia Iraq Aliyekuwa mwanasheria mkuu wa Uingereza, Lord Goldsmith, amesema taarifa kutokana na upelelezi hazikuonyesha kwamba Iraq ilikuwa tisho kwa Uingereza, na kwa hiyo nia ya kutaka kujihami haikuwa sababu ya kutosha kuivamia Iraq.
Akitoa ushahidi kwa tume rasmi ya uchungizi, Lord Goldsmith alisema kwamba hisia zako hapo mwanzo ilikuwa kwamba itabidi kupitisha azimio la pili katika Umoja wa Mataifa, ili kuchukua hatua za kijeshi kwa kuzingatia sheria.
Alisema alihisi kwamba ushauri huu haukukaribishwa vyema na aliyekuwa waziri mkuu wakati huo, Tony Blair.
Licha ya hayo alibadilisha mawazo yake, na sababu za kufanya hivyo atajitahidi kuelezea baadaye.



http://www.bbc.co.uk/swahili/news/story/2010/01/100127_goldsmith.shtml
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom