Golden opportunity for central & local government in Dar!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Golden opportunity for central & local government in Dar!!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kasheshe, Dec 24, 2011.

 1. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #1
  Dec 24, 2011
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Kama kuliwahi kutokea, wakati muafaka wa kuwaondoa watu waliojenga mabondeni ni huu!!! Serikali ya mitaa na kuu wanatakiwa kuhakikisha mabaki yote ya nyumba yasafishwa mara moja kuhakikisha ndugu zetu hawapati sababu za kurudi huko mabondeni, Waziri wa Ardhi (Tibaijuka, this is your time to accomplish your long due plan for better urban settlement, itakuwa kama unasukuma mlevi), TAMISEMI, mambo ya ndani, Ustawi wa Jamii, Ofisi ya Waziri Mkuu mafaa; Please act!Kumbuka kitachokuwa kinavunjwa sio nyumba tena, bali mabaki ya nyumba... nasubiria mawe lakini habari ndio hiyo... time for change to rescue ever loosing of Tanzanians lives....
   
 2. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #2
  Dec 24, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  sio rahisi ki hivyo maana itabidi uestablish a strong base ya kuhalalisha hiyo 'exodus' maaana hata wanaoishi maeneo ambayo awali yalikuwa hayapo kwenye list ya maeneo ya bondeni ktk mafuriko haya yameonekana kama ni maeneo ya bondeni.
   
 3. Bantugbro

  Bantugbro JF-Expert Member

  #3
  Dec 24, 2011
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 2,684
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Tatizo ni wabunge wa Dar haswa wa Ilala yule anaejiita Zungu...yeye aliapa kuwa hatatoa ushirikiano kwa waziri katika hili suala la kuhamisha wanaoishi mabondeni, ndo maana katika msiba huu yuko kimyaaaa ka kata mtungini.:tongue:
   
 4. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #4
  Dec 24, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,758
  Likes Received: 6,062
  Trophy Points: 280
  Ha ha ha ha ha ha! Mkuu hapo kwenye red umenikumbusha mbali sana. Yaani ile "great trek" ya wana Israel kutoka utumwani kwa Farao kuelekea nchi ya ahadi - Kanaani - safari nzima ikiratibiwa na kuongozwa na Mungu mwenyewe kama Mkuu wa msafara pamoja na viongozi wengine wadogo wadogo Nabii Musa & Co. Walikula Mana na kunywa Jangwani na hata wakati mwingine wakipatiwa Nyama safi kutoka Mbinguni.

  Mchana wakiongozwa na Wingu na usiku Nguzo ya Moto wasife kwa joto na baridi hatari ya Jangwani. Wakaingia Sinai pale wakapewa Maagizo (Amri) za Mwenyezi Mungu hatimaye Mtu wa Mungu akafia huko. Hatimaye Joshua akachukua usukani kuliongoza kundi kwa mafanikio ya kutisha mwishowe wakaingia Kanaani wakiizunguka Ngome ya Yeriko hatimaye wakachukua nchi sawa sawa na agizo la Mungu.

  Sasa kwenye hii exodus yetu ya mabondeni sijui nani mkuu wa msafara, sijui viongozi ni akina nani, sijui wanaelekea eneo lipi, watalishwa nini, na nani na kwa wakati gani zaidi ya dhuluma, uonevu, masimango, matusi, kejeli, dharau, na kila aina ubaya. Maana hata Nape tayari keshatoa pongezi kwa vijana wake wa CCM.

  Wale ni ndugu zetu iwe waliishi pale kwa halali au isivyo halali, hali iliyowakuta isiwe sababu ya dharau kwao; watendewe kibinadamu ikiwepo kuwezeshwa namna ya kuanza maisha mapya endapo itabidi kuhama. Sioni ni kwa nini serikali ishindwe kuwajengea nyumba kwenye maeneo mapya - in fact kwa serikali makini na inayojali hili ni jukumu lake la msingi.

  LAKINI pia sitashangaa kuona maeneo watakayoondoka yakauzwa kwa mafisadi na "wawekezaji" mara moja. Kama tungekuwa na Bunge makini sheria ingetungwa haraka kuhifadhi maeneo husika dhidi ya UFISADI uliotamalaki nchi hii. Nawasilisha.
   
 5. majata

  majata JF-Expert Member

  #5
  Dec 24, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 385
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 45
  Imetulia.
   
 6. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #6
  Dec 24, 2011
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,020
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
  huu sio ushauri wa kitaalamu bali ni uhuni uliozidi vipimo.leo hii shirika la nyumba linajenga apartments za mabilioni ya shilingi nyumba ambazo hata mfanyakazi wa serikali hawezi kuzinunua.je ni kwa nini shirika hili lisipewe maelekezo ya mara moja kuwajengea wakazi wa mabondeni nyumba za bei nafuu??ni upuuzi kusema watu wahame huku ukiwa hujawataarishia sehemu za kuhamia.tusifanye mambo kiujanja ujanja,tusidhani kwamba watu hawajui kuwa tunachoma masoko ili kuwaondoa wafanyabiashara wadogo na kuwajengea wafanyabiashara vigogo.sioni mantiki ya kumvizia mwananchi kama una nia ya dhati ya kumsaidia.
   
 7. Mupirocin

  Mupirocin JF-Expert Member

  #7
  Dec 24, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,596
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  nimeipenda hii, tuombe huruma ya Mungu iwatawle hawa viongozi angalau wawe na huruma hata kidogo tu kama chembe ya haradari.
   
 8. Mbugi

  Mbugi JF-Expert Member

  #8
  Dec 24, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,488
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 160
  sijui kama wanapata wasaa wa kutembelea jf maana hapa umetoa angalizo bila chenga wala ada; asante sana
   
Loading...