Godoro gani ni zuri?

Nalalia Tanfoam ni miaka zaidi ya kumi liko vile vile..... Km kuna godoro bora zaidi ya hili mtu aje ani prove wrong sasa hv
 
Bora uongezee tu hela ununue lenye spring kwa size hiyo hiyo lakini lenye spring. Kwanza litadumu miaka mingi. Pili linasaidia kunyoosha mgongo. Hutasikia habari za kiuono,mgongo au shingo. Wengi hawajui,matatizo ya migongo na viuno yanaanzia kwenye hayo magodoro yasiyo na spring ksbb lisilo na spring likitumika kwa muda wa miezi kadhaa linakosa level, linabonyea,linaanza kwa bila wewe kuliiona,baadae linaonekana mfano mkilalia wawili linawakusanya katikati. Linaweza kuwa ni kubwa vile vile,lakini linawakusanya katikati. Lakini la spring hata liwe la muda mrefu kwa kiasi gani halibonyei upande
 
Nenda opposite na maktaba pale posta kuna showroom ya vita uchague godoro upendalo na bei ni nafuu sana, mtaani wanaongeza kama laki nzima mkuu
 
Ukiachana na Majina makubwa ya Tanfoam na QFL dodoma.

Nimekuja kugundua Vitafoam ndio kampuni best ya magodoro Tanzania,magodoro yao yana madaraja ambayo utachagua wewe kuendana na hela yako.

Binafsi nilinunua godoro la VitaSupreme godoro ni quality sana na bei ni nafuu sana ila nashauri nunua katika maduka yao..
Tanfoam is best but it's overprice
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom