Elias Msuya
Senior Member
- Dec 23, 2011
- 175
- 681
Mwenyekiti wa Taasisi ya Taifa ya Taaluma ya Madereva Tanzania (TATAMATA), Godlove Materu ameachiliwa na Jeshi la Polisi baada ya kukamatwa tangu Februari 5, 2026.
Taarifa iliyotolewa na Wakili wake, Aloyce Komba kutoka Haki Kwanza Advocates leo Februari 12 imesema Materu ameachiwa huru baada ya kudhaminiwa na mke wake Februari 9, 2026.
“Tunautaarifu umma wa watanzania na vyombo vya habari kwamba, mteja wetu, Godlove Materu aliyekamatwa na Jeshi la Polisi mkoa wa Songwe mnamo tarehe 05. 02. 2026 na kushikiliwa kwa siku tano (5) bila kujulikana alipo, ameachiwa huru baada ya kudhaminiwa na mke wake Februari 9, 2026,” imesema taarifa hiyo.
Wakili Komba amesema, Materu, ametakiwa na Kamanda wa Upelelezi wa Mkoa wa Songwe, ACP John Maro, aende kituo cha polisi cha Tunduma mnamo Februari 13, 2026 (Ijumaa) saa 5 asubuhi.
“Hadi tunapotoa taarifa hii, mteja wetu hajaambiwa ametenda kosa au makosa gani ya kijinai kwa muda wote aliposhikiliwa katika vituo mbali mbali vya Jeshi la Polisi katika mkoa wa Songwe na mkoa wa Mbeya.
“Aidha, polisi inashikilia komppyuta mpakato (laptop), simu mbili za mkononi na funguo za makufuli ya sehemu yake ya biashara mjini Tunduma, mtaa wa Chapwa,” amesema.
Awali Materu alikamatwa na watu wasiojulikana Februari 5, lakini taarifa ya Jeshi la Polisi iliyotolewa Februari 9 ilisema kuwa wanamshikilia kiongozi huyo na kuwataka wananchi kupuuza taarifa kuwa alichukuliwa na watu wasiojulikana.
Hata hivyo, taarifa ya polisi haikufafanua kuwa wanamshikilia Materu kwa makossa gani.
Soma pia: Madereva wa malori waipa Serikali skku 2 mwenzao apatikane
Taarifa ya polisi ilikuja baada ya tamko la viongozi wa TATAMATA waliolitoa kwa vyombo vya habari mnamo Februari08, 2026 wakisema hawakujua kiongozi mwenzao alipo na kupanga kuwataarifu waajiri wao kwamba kama asingepatikana ifikapoFebruari 10, 2025 wangesimamisha shughuli zao nchi nzima na nchi za jirani ili wamtafute.
Soma pia: Wakili wa Godlove Materu awauliza polisi maswali matano