Uamuzi wa kuvifungua vyuo anastahili kongole zake, lakini uharaka wa kutaka kuvifungua hapo hapajatulia kabisa. Mimi ningeshauri angevuta tu subira mpaka tarehe 1 Julai, ili aweze kuupima upepo na kuusoma vizuri mchezo, ili apate nafasi nzuri ya kuangalia nini hasa ambacho kinafaa kufanyika hasa kupitia kujifunza kwa mataifa mengine. Tukikosea tu "timing" Watanzania tutageuka kuwa "laughing stock" mbele ya mataifa mengine ulimwenguni hasa jirani zetu.