Godbless Lema Taifa linaongozwa na sauti yako tuliyoikataa

Sidhani mleta mada ukiwa Mwanamke kumsifia mume wa Mtu Godbless Lema hujamtendea haki mkewe hizo sifa ulizomumwagia mumewe angekuwa nchini mkewe angkuzaba vibao

Beatrice kasifie wako hata kama haenei

Chako ni chako hata kama ni chongo
Mumeo anaenea? Kilangila.
 
Mara baada ya waziri mkuu msitaafu Edward Lowasa kujiunga na kuinunua Chadema ili awe mgombea urais mwaka 2015 , kitu cha kwanza kabisa alipokabidhiwa tu chama alipiga marufuku siasa za kiharakati na kushauri siasa hizo hazina tija kwa sasa. Edward Lowasa alionya kuwa Chadema lazima igraduate kutoka chama cha kiharakati hadi kuwa chama cha siasa sasa.

Edward Lowasa alifafanua madhara ya chama kubaki cha kiharakati muda wote kuwa ni pamoja na kupinga maendeleo yote ya nchi ,kuombea mabaya nchi ,kushirikiana na mabeberu ili kuiibia nchi ,pamoja na kushangilia kila lililobaya kwa taifa ili kumfurahisha tu anayefadhili hizo harakati zako. Matokeo ya harakati hizi ni chama kuchukiwa na wazalendo na kupoteza ushawishi kwa wananchi.
Hakika Lowasa aliona mbali. Leo brand ya chadema imeharibiwa vibaya, chama kilichojizolea umarufu kwa kutetea wanyonge leo kinataka machinga na mama ntilie wafukuzwe mitaani!!! Leo ni furaha kubwa kwa Chadema ndege kukamatwa na wazungu!!!

Pia tangu tarehe 17 mwezi march Tanzania imekumbwa na simanzi isiyo na kifani mara baada ya kutangazwa kwa kifo cha rais Magufuli.
Mamilioni ya watanzania wameangua kilio kila kona kwamba sasa mwokozi wao ameondoka, cha kushitusha ni kwamba wananchi wa hali ya chini kabisa ndiyo wanaoongoza kwa kilio kinyume na tulivyokuwa tumeaminishwa kwamba Magufuli alikuwa ananyonga wanyonge!
Kitendo cha hayati rais Magufuli kuagwa na mamilioni ya watanzania huku wakiangua vilio njia nzima na kutandika kanga zao chini ili mwili upite imeenda kinyume kabisa na wasaliti wa nchi hii akina Tundu Lisu na genge lake.

Kwa jinsi msiba huu unavyoenda naamini utakuwa darasa tosha kwa wasaliti wa nchi hii akina Tundu Lisu ,Godbless Lema, Chahali, Ngurumo, Mange Kimambi na wengine wengi, sasa wataelewa kumbe watanzania siyo vilaza.
Wataelewa kumbe watanzania wanajua yupi anapigania haki zao kwa vitendo na ni yupi ni mpiga makelele nyuma ya keyboard.

Kwa mapenzi haya yanayoonyeshwa na Watanzania kwenye msiba huu ni lofa tu atakayeendelea kuamini kwamba eti Tundu Lisu aliibiwa kura kwenye uchaguzi mkuu uliopita.

Wito wangu kwa wasaliti wa nchi hii wanaoshangilia msiba kwamba sasa Magufuli ameondoka watarudi Tanzania na kuanza tena kutumika kuiba rasilimali za nchi hii kama walivyokuwa wanafanya huko nyuma wajue tu kwamba wanapoteza muda.
Watanzania siyo vilaza ,wanajua fika Tundu Lisu aliwatisha kwamba watashitakiwa MIGA ikiwa watabadili sheria za madini.
Tundu Lisu aelewe kuwa hawezi kuwa rais wa Tanzania kwa kushinda Twitter akikejeli kila lililojema kuhusu nchi yetu,
Tundu Lisu kupitia msiba huu atakuwa ameelewa na kupata darasa kwamba ukitaka kupendwa na Watanzania tumikia watanzania na siyo kutumikia Acacia
mkuu magu kashakufa hamuamini tu.
 
Huyu mtu unajiuliza anakosekanaje Bungeni? Anakosekanaje kwenye uongozi wa nchi hii? Kweli huyu niwakwenda kuishi ukimbizini? Kutuambia ukweli ndo kigezo chakutisha atoroke nchi? Na tunaamini kweli kwamba alikuwa adui wa Taifa Leo au alikuwa adui wa watu wasiowaadilifu?

Taifa letu tutazidi kukwama Hadi pale tutakapoanza kuwakumbatia wazalendo na watu wenye uelewa mpana Kama Lema. Leo kelele za Kodi alizompigia Makamu wa Rais Bungeni ndo tunazinduka kuzifanyia kazi, kwanini Mzee Mpango ukumsikiliza kipindi kile kabla Taifa alijapata hasara?.

Lema uishi maisha marefu uione Tanzania ya Ndoto yako. Kukosekana kwako Bungeni tunaona pengo, praising team haina hoja kinzani.
Bado lile la Ndugai
 
Hayo Hayo Hayo maswala ya kodi lema sio mtu wa kwanza kuyasema bungeni. Hapo uwazungumzie akina zitto kabwe, akina Mbowe, msigwa na Mnyika.

Lema huwa anarudia hoja zile zile za nyuma ila kwa sauti tu. Hajawahi kuja na hoja binafsi ambayo ina mashiko.

Wewe utakuwa umeanza kufuatilia bunge kipindi cha awamu ya magufuri. Ungekuwa unafuatilia tokea kipindi spika ni mzee Pius Msekwa ungeelewa hizi hoja za kodi zimetokea wapi.
 
Sidhani mleta mada ukiwa Mwanamke kumsifia mume wa Mtu Godbless Lema hujamtendea haki mkewe hizo sifa ulizomumwagia mumewe angekuwa nchini mkewe angkuzaba vibao

Beatrice kasifie wako hata kama haenei

Chako ni chako hata kama ni chongo
Kama ana hoja jibu hoja yake hii biashara ya mipasho ya singeli achana nayo ndugu.
 
Lema huyu anayedaiwa alikuaga mwizi wa magari tena sio mtaalam wa chochote ndio unatutisha eti taifa linamkosa? Hebu muachage mzaha wajameni.
Yaezekana ukawa na hoja ili twende sawa ni vyema ungeweka ushahid angalau magari matatu aliyoiba, alimuibia nan na kama kuyauza aliyauza kwa nan. Ahsnt jibu tafadhali
 
Ni kweli walikua na hoja mbadala bungeni, ila ndani ya chama walikua wapigaji pamoja na mwenyekiti. Haiwezekan milioni 300 kila mwezi ya ruzuku kwa muda wa miaka 5 washindwe kujenga hata ofisi. Uliwaambia ukweli huu wanatukana... Sujui demokrasia gani wanaitaka hawa wachaga

Sent from my Android using JamiiForums mobile app
Kwanza kbs acha ukabila!! Pili.. ni vyema ungeleta na draft ya matumizi yao ya ruzuku ili tujiridhishe pesa yetu ya kodi ni wap wameipiga. Ni vyema pia uka attach mikoani kote shughuli zao za kiofisi kila cku hua wanazifanyia wap ili tujiridhishe kua hata ofis tu hawana, ahsnt majibu tafadhali. Kama hua wanafanyia kaz zao za kiofis bar tutajua tu
 
kodi ilipigiwa kelele na Nape, msigwa, magufuli, n.k

una mahaba kwa Lema, tatizo kaoa na yuko canada
Mkuu yeye ame mention mmoja ambae ni Lema, hivyo kumlazimisha afanye representation kwa wote humtendei haki. Kikubwa anzisha naww uzi u represents waliobaki.
 
Uhuru wa mitandao usikufanye uwaseme watu wezi wamagari wakati ukiambiwa thibitisha huwezi
Issue ni hapo kweny evidence 🤣🤣🤣! Mimi kuna mmoja humu nimeomba atoe ushahid angalau wa magari matatu aliyoiba ili tujiridhishe. Lkn hakuna majibu
 
Mara baada ya waziri mkuu msitaafu Edward Lowasa kujiunga na kuinunua Chadema ili awe mgombea urais mwaka 2015 , kitu cha kwanza kabisa alipokabidhiwa tu chama alipiga marufuku siasa za kiharakati na kushauri siasa hizo hazina tija kwa sasa. Edward Lowasa alionya kuwa Chadema lazima igraduate kutoka chama cha kiharakati hadi kuwa chama cha siasa sasa.

Edward Lowasa alifafanua madhara ya chama kubaki cha kiharakati muda wote kuwa ni pamoja na kupinga maendeleo yote ya nchi ,kuombea mabaya nchi ,kushirikiana na mabeberu ili kuiibia nchi ,pamoja na kushangilia kila lililobaya kwa taifa ili kumfurahisha tu anayefadhili hizo harakati zako. Matokeo ya harakati hizi ni chama kuchukiwa na wazalendo na kupoteza ushawishi kwa wananchi.
Hakika Lowasa aliona mbali. Leo brand ya chadema imeharibiwa vibaya, chama kilichojizolea umarufu kwa kutetea wanyonge leo kinataka machinga na mama ntilie wafukuzwe mitaani!!! Leo ni furaha kubwa kwa Chadema ndege kukamatwa na wazungu!!!

Pia tangu tarehe 17 mwezi march Tanzania imekumbwa na simanzi isiyo na kifani mara baada ya kutangazwa kwa kifo cha rais Magufuli.
Mamilioni ya watanzania wameangua kilio kila kona kwamba sasa mwokozi wao ameondoka, cha kushitusha ni kwamba wananchi wa hali ya chini kabisa ndiyo wanaoongoza kwa kilio kinyume na tulivyokuwa tumeaminishwa kwamba Magufuli alikuwa ananyonga wanyonge!
Kitendo cha hayati rais Magufuli kuagwa na mamilioni ya watanzania huku wakiangua vilio njia nzima na kutandika kanga zao chini ili mwili upite imeenda kinyume kabisa na wasaliti wa nchi hii akina Tundu Lisu na genge lake.

Kwa jinsi msiba huu unavyoenda naamini utakuwa darasa tosha kwa wasaliti wa nchi hii akina Tundu Lisu ,Godbless Lema, Chahali, Ngurumo, Mange Kimambi na wengine wengi, sasa wataelewa kumbe watanzania siyo vilaza.
Wataelewa kumbe watanzania wanajua yupi anapigania haki zao kwa vitendo na ni yupi ni mpiga makelele nyuma ya keyboard.

Kwa mapenzi haya yanayoonyeshwa na Watanzania kwenye msiba huu ni lofa tu atakayeendelea kuamini kwamba eti Tundu Lisu aliibiwa kura kwenye uchaguzi mkuu uliopita.

Wito wangu kwa wasaliti wa nchi hii wanaoshangilia msiba kwamba sasa Magufuli ameondoka watarudi Tanzania na kuanza tena kutumika kuiba rasilimali za nchi hii kama walivyokuwa wanafanya huko nyuma wajue tu kwamba wanapoteza muda.
Watanzania siyo vilaza ,wanajua fika Tundu Lisu aliwatisha kwamba watashitakiwa MIGA ikiwa watabadili sheria za madini.
Tundu Lisu aelewe kuwa hawezi kuwa rais wa Tanzania kwa kushinda Twitter akikejeli kila lililojema kuhusu nchi yetu,
Tundu Lisu kupitia msiba huu atakuwa ameelewa na kupata darasa kwamba ukitaka kupendwa na Watanzania tumikia watanzania na siyo kutumikia Acacia
"WASALITI WA NCHI" Ni mwananchi mshe**zi tu anaeweza kuwaita wananchi wenzake majina kama hayo na yanayo fanana na hayo,kisa tu mnatofautiana misimamo au mitizamo ama imani.
Kujiona nyinyi wazalendo huku nyuma tuhuma za ukabaji,dhuruma na ukatili zikiwaandama,Wasiojulikana,kubambikia watu kesi matendo ya watu kama bashite,sabaya's. MTU ANAYE SHIRIKI AU KUUNGA MKONO MAZINGIRA NA UCHAFU HUO HAWEZI KUWAITA WATANZANIA WENGINE WASALITI! NEVER NAKATAA HADI KABURINI.
Kaeni chini ondoeni vibanzi machoni mwenu,safisheni nyumba yenu ndio mrudi mtuite wachafu.
 
Kwanza kbs acha ukabila!! Pili.. ni vyema ungeleta na draft ya matumizi yao ya ruzuku ili tujiridhishe pesa yetu ya kodi ni wap wameipiga. Ni vyema pia uka attach mikoani kote shughuli zao za kiofisi kila cku hua wanazifanyia wap ili tujiridhishe kua hata ofis tu hawana, ahsnt majibu tafadhali. Kama hua wanafanyia kaz zao za kiofis bar tutajua tu
Mkuu hawana ofisi wanayomiliki, nyingi wamepewa msaada na kupanga. Ikiwa makao makuu ni kama 'kibanda umiza' itakuaje huko mikoani?

Kuhusu ripoti za matumizi ya ruzuku mie sina. Ila report ya CAG mwaka huu imeonesha matumizi yasiyo na ushahidi wa mamilioni ya shilingi. Hii nenda hata Google utaipata ushahidi wa ripoti ya CAG kwa vyama vya siasa. Ushahidi mwingine, rejea maneno ya lijua likali.

Kuhusu ukabila, nisamehe kama nimeelewa vibaya. Mie si makabila ila pale CDM walizidi kuwekana wachaga au wakaskazini.

Sent from my Android using JamiiForums mobile app
 
Saa ingine mnchekesha SANA!
tapatalk_1537986306530.jpg
 
Back
Top Bottom