Godbless Lema: Nimemaliza Arusha sasa nashuka Mtwara

Wana wa Arusha wamesema mwakilishi wao halali wa kuwawakilisha ni Mh Lema na madiwani waliowachagua,
Ewe MUNGU endelea kuwapa watu wako baraka ya ukombozi wa kifikra,
 
Heshima kwenu makamanda popote mlipo, na hongereni sana kwa ushindi wa sunami hapo jana.

Watanzania ambao tupo mbali na Arusha tunakiu ya kusikia japo neno moja tu kutoka kwa viongozi wetu hasa kamanda Lema a.k.a muarobaini wa magamba kuhusu uchaguzi wa Arusha ulivyofanikiwa na mtawafanyia nini wana Arusha ndani ya siku 100 baada ya madiwani kuapishwa.

Pia msisahau kuhusu meya wa Kichina!
 
Hatima ya uwepo wa CCM na CUF huku kusini ipo mikononi mwa CDM,Hakuna uchaguzi walioshinda ccm kwa kura ktk siku za hv karibuni huku.Kifupi wananchi tumeshawashitukia CCM na CUF ni dili moja,Kitu ambacho kimetufanya kutafuta ufumbuzi mbadala kwani wengi wetu tuliichagua CUF kutokana na kuikataa CCM kumbe mwisho wa siku m/kiti wa cuf taifa kakiunganisha na magamba kimyakimya.Amesahau kuwa sisi hatukukipenda CUF kutokana na uzuri wa sura wa viongozi wake badala yake tulikipenda kwa kuamini kina sera mbadala zitakazotutoa hapa tulipokwamishwa na ccm!.Kusini sasa sio kwamba wanakisikia tu CDM ila wanakiona kupitia vyombo ya habari makini hususani tv na mitandao ya kijamii pia,Ikumbukwe huku tuliwekwa ndani ya box kwa kurushiwa matangazo ya TBC taifa pekee! Bilashaka hakuna asiyejua utendaji wa sasa wa kituo hiki.Lkn sasa watu wametoka ndani ya box na kujua kuna vyanzo vingi vya habari na taarifa muhimu na vyenye kuaminika duniani kote tofauti na walivyokituaminisha hawa ccm zamani eti habari mzuri na yakuamini ni ile inayotolewa na vyombo vyao au vishirika na wao!,Tunawahitaji CDM kusini kwa sasa kuliko wakati wowote uliowahi kutokea! Ninarudia kusema tena kuwa unapoizungumzia kusini MOYO wake ni NACHINGWEA! CDM ikija kuisambaratisha rasmi ccm Nachingwea basi kazi imekwisha,Na kazi iliyobaki ni kidogo mnoo.Naamini CDM kikimpeleka Lema na Lisu wakawapa muda wa hata dk 45 tu kila mmoja! Kwa ninavyowafahamu hawa makamanda huu muda unawatosha kuizika ccm na mshirika wao Cuf kusini.Musiofu ikiwezekana waagizeni viongozi wenu wa kanda ya kusini watutangazie wananchi tuchangie hiyo ziara na mutashangazwa kwa jinsi gani watu watakavyojitolea kwa moyo mmoja kwa hari ma mali,Kusini hatuamini propaganda za kitoto zinazoenezwa wa baadhi ya wasioitakia mema nchi hii na chama hiki pendwa kuwa ni cha kikanda,kidini,Kikabila n.k. Kwani hatudanganyiki ng'o.Njooni CDM kusini mutuongoze kondoo wenu! Kwani imefika wakati hadi waliokaamia cuf wanafikiri kurudi ccm baada ya kuwagundua viongozi wa cuf niwasaliti. Mwisho kabisa niwakumbushe tu viongozi wa chama ninachikipenda CDM kuwa; Kufuru ya ccm kupitia mbunge woa Chikawe ya kuwagawia wananchi waliompigia kura zawadi za SANDA kila nyumba ndo inayowatafuna,Kile kitendo wananchi wamelia sana ndo maana hadi leo hii mh. Anaogopa kufanya mikutano ya hadhara na wananchi wa Nachingwea hususani maeneo ya tarafa za mjini.KARIBUNI CDM KUSINI ccm na washirka wao cuf hawana mpya na wenyewe wanalijua hilo ndo maana akili zao wanaelekeza kwenye kuiba kura tu.

Aaaa Lema kumbe una I'd nyingi,huu uandishi wako haufanani na wamachinga

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Heshima kwenu makamanda popote mlipo, na hongereni sana kwa ushindi wa sunami hapo jana.

Watanzania ambao tupo mbali na Arusha tunakiu ya kusikia japo neno moja tu kutoka kwa viongozi wetu hasa kamanda Lema a.k.a muarobaini wa magamba kuhusu uchaguzi wa Arusha ulivyofanikiwa na mtawafanyia nini wana Arusha ndani ya siku 100 baada ya madiwani kuapishwa.

Pia msisahau kuhusu meya wa Kichina!

....Kamanda anaelekea Mtwara....

Jukumu la kuijenga Arusha Mpinga na wenzake wanatosha tutawapa ushirikiano wakutosha G LEMA tumempa jukumu la kwenda KUKOMBOA Mtwara ..........

Arusha madiwani na sisi wapiga kura YATOSHA!!!!
 
Wapi shonza?jana aliweka bandiko lake hapa jf eti magamba yatashinda arusha anzisha tena u-ko a town tunaijua wenyewe
 
Kweli Kabisa yaan huyo jamaa anachokifanya ni kulipa fadhila maana wachina walikuwa hawana cha kusubiri ispokuwa ni kunyonga tuuu yule mwehu...!na babake akaona chakufanya ni kuuza nyumbani kwao(Bagamoyo na sasa anamalizia kwa wakwe zake..!
 
Kijana mwenye mikakati madhubuti ya ushndi Godbless Lema, ametamka kuwa amemaliza Arusha kurudisha kata zote 4 kama zawad ya wananchi kwa Lema kurudisha Ubunge wake, sasa atamka kuwa anadondoka rasmi kuikomboa Mtwara.

Amesema Mtwara imekosa mpambanaji wa kweli mwenye kujiamini na hvyo anashuka rasmi mtwara. CHADEMA leo imetwaa kata zote 4 licha ya nguvu kubwa ya CCM na jesh la Polisi hadi kupelekea naibu katbu mkuu Mwigulu kupga kambi Arusha mwezi mzima. LEMA amethbitisha umwamba wake katka siasa za Arusha. Lema ni kpenz cha wanaArusha bila shaka.

Amesema CCM wajiandae Mtwara kwa kuwa anaenda na kuipatia uhuru mtwara. Kumbuka A GRAIN OF WHEAT.

Kuna koti moja pale magogoni likimsikia huyu jamaa linatamani kuhama nchi...
 
the great god almighty can not side with a CRIMINAL....
huyu mungu wenu sijui ni yupi, after all inaelekea wewe ni mbumbumbu wa jiografia na historia ya tanzania.
kuifananisha ARUSHA NA MTWARA ni uendawazimu.
huku hakuna WACHAGA. na hata arusha siku wenye mji wao watakapowakataa walowezi, mtarudi kujibana kwenuuuuuuuuu uchagani
Mods wanawafurahia member kama nyie muliojizira umetoka kwenu kupalula migebuka upo Dar kwa raha zako wazaramo hawajakutimua ila unataka wachaga watimuliwe wakati wamasai wametapakaa Tanzania nzima kuliko kabila lolote lile duh
 
Mungu endelea kuibariki cdm na utuokoe na jinamizi ccm pamoja na hawala yake cuf
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom