Baada ya kuchemsha kwa Mrisho Gambo, Godbless Lema ahamia kwa Athuman Kihamia (DED Arusha)

Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,894
20,372
Wadau, amani iwe kwenu.

Upo msemo wa kiswahili kuwa ukienda Msituni kuwinda ukakosa mnyama mkubwa uliyemkusudia, hupaswi kurudi mikono mitupu. Unapaswa kuwinda hata ndege ili mradi tu uonekane umerudi na nyama.

Hayo yanatokea kwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema ambaye nadiriki kusema kwa hakika kabisa kuwa maji yamefika shingoni. Hana ujanja tena. Amepelekewa Squad ambayo si size yake. Amepelekewa watu wanaoijua Arusha na uhuni wa Arusha. Arusha sasa imetulia baada ya wenye Arusha kuamua.

Mtakumbuka kuwa mara tu baada ya Mrisho Gambo kuteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Godbless Lema alianza kumshambulia kwa maneno ya dhahiri na kwenye mitandao ya kijamii. Mashambulizi hayo yalijitokeza hata viongozi hao walipokuwa na Kikao na Naibu Waziri TAMISEMI Seleman Jafo. Hata hivyo, umahiri na kujiamini kwa Mrisho Gambo hakika kulimfanya Lema ainamishe kichwa chini asijue nini cha kufanya.

Wakati fukuto likiendelea, Mrisho Gambo akapandishwa Daraja na kuwa Mkuu wa Mkoa. Hakika hii ilikuwa fedheha na aibu kubwa kwa Lema. Aliona sasa njama zake za kumchonganisha na Mamlaka iliyomteua zimeshindikana. Hapo Lema akaamua kunawa mimono. Sasa Gambo amekuwa Mkubwa kwake na hawezi tena kumhusisha na siasa za majitaka.

Amegeukia kwa Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Athuman Kihamia. Baada ya kuteuliwa Kihamia kuwa DED Arusha akitokea Kaliua, Tabora, na baada ya kuona hasomeki, alianza kumsakama DED huyo hasa kwenye mitandao ya kijamii. Kuanzia tarehe 9 Oktoba, 2016, Mashambulizi ya dhahiri dhidi ya Kihamia yamezinduliwa Rasmi na Godbless Lema kwa kuwatumia baadhi ya vijana wa Mkoa wa Kilimanjaro na Arusha wakiwemo Malisa Godlisten, Henry Nkya na Ally Bananga. Nitaweka baadhi ya matukio.

1. Tarehe 9 Oktoba 2016, akiandika kwenye ukurasa wake wa Facebook, Malisa Godlisten alizua tuhuma kuwa Athuman Kihamia amejiidhinishia lita za Mafuta 1,900 kwa ajili ya gari lake. Malisa alisema kuwa Kihamia amejiidhinishia kiasi hicho kikubwa cha mafuta bila ya kufuata taratibu. Hata hivyo, baada ya kupitia nyaraka alizoweka, imethibitika kuwa taratibu zote zilifuatwa na mafuta hayo yaliombwa kwa njia ya dharura. kwenye nyaraka hizo, imebainika kuwa mafuta hayo ni kwa ajili ya matumizi ya Magari yote ya Ofisi Mkurugenzi wa Jiji la Arusha kutokana na shughuli ya dharura iliyojitokeza wakati huo.

Aidha, Malisa pia aliweka nyaraka zinazoonesha kuwa Kihamia ana sifa ya ufisadi na kwamba akiwa Kaliua, Tabora, alikula shilingi 54,966,995 za Ujenzi wa Jengo la Utawala. Kwamba, Bajeti ya Jengo hilo ni shilingi 494,451,516. Zilizotolewa ni shilingi 549,418,511. Kwamba kiasi cha shilingi 54,966,995 hakijafika kwa mkandarasi ingawa fedha ziliidhinishwa na kupewa Kihamia ili ampe Mkandarasi. Hata hivyo, madai hayo yamejibiwa kwenye nyaraka hiyo hiyo kuwa fedha hizo zilikuwa hazijalipwa kwa mkandarasi kwa kuwa ujenzi ulikuwa haujakamilika.

2. Oktoba 12, 2016, kwa mara nyingine Malisa Godlisten alizua madai kuwa Mwalimu Batuli Hamadi ametekwa na kuchomwa sindano ya sumu. Kwamba, waliofanya tukio hilo ni Athuman Kihamia kwa kushirikiana na Catherine Magige ( Mb). Kwamba, Batuli alitekwa na kulishwa sumu kutokana na mwalimu huyo kulalamika kitendo cha kuvuliwa madaraka ya Mratibu wa Elimu Kata. Hili sitalielezea sana kwa vile lipo chini ya uchunguzi wa Jeshi la Polisi.

3. Oktoba 17, 2016, Henry Nkya alisambaza barua ambayo kwa hakika inaonekana ya kughushi ambayo inadaiwa kuandikwa na Afisa Habari wa Jiji la Arusha, Nteghenjwa Hosseah. Barua hiyo inaonekana imeandikwa Oktoba 13, yaani aiku moja tu baada ya madai ya Malisa kuwa Malimu Batuli ametekwa. Kwenye barua hiyo, Inaelezwa kuwa Athuman Kihamia anajigamba kuwa yeye ndiye Mteule wa Rais na kwamba hakuna chombo chochote chenye mamlaka ya kukamata na kumhoji. Hata hivyo, imebainika kuwa Barua hiyo ni ya kughushi na Hosseah amewasilisha malalamiko yake kwa Jeshi la Polisi na TCRA ili wawatafute na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria wale wote waliohusika na uzushi huo.

Ninachokiona kwa Godbless Lema ni kuweweseka. Lema anamuona Catherine Magige kama mshindani wake kwenye ubunge Uchaguzi Mkuu wa 2020. Sina hakika kama Catherine atagombea ama la ila Lema halali usingizi akimhofia.

Ninachokiona pia kwa Kihamia ni kwamba, hapendi mambo ya kipuuzi na kijinga. Madiwani walipojiongezea posho za kufuru Kihamia alisema hapana na akatumia fedha hizo kulipa malimbikizo ya madai ya walimu. Hapo ndipo lilipo chimbuko la Mgogoro wa Lema na Kihamia.

Hata hivyo, nimkumbushe Lema kuwa si kila mtu anaweza kumfitinisha na akafitinika. Wengine ni maji shingo kwake. Aendelee kuchapa kazi ili kuwaletea maendeleo wana Arusha. Majungu na fitina hazitasaidia kitu. Akiendeleza Majungu yake itakuwa ni sawa na kumpiga teke chura. Humuumizk bali unamuongezea mwendo. Sitashangaa kusikia Kihamia anateuliwa kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Arusha
 
Crap..
Lema ahangaiki na Gambo hata siku moja.. Na Lema angekuwa anamwogopa Gambo asingemwalika kwenye function ya leo ya kuweka jiwe la msingi la hospital kubwa inayoanza ujenzi Arusha.. Badala yake Gambo kanywea kwenda kwenye hii function sababu ya kuona aibu ya maendeleo yanayoletwa na Lema jijini Arusha.
Shame on you Gambo and your puppets!!!
 
Pamoja na yote, tuweke fitina mbali, wakurugenzi wengi wa halmashauri akiwemo na huyo wana under performance..!!! Nadhani weledi wao wengi bado ni mdogo, maana wanahangaika na vitu vingine ambavyo kimsingi wameshindwa wao wenyewe
Usigeneralize Mkuu
 
Mrisho Gamba ni dhaifu kama alivyo Makonda na wamewezwa mpaka vimbelembele vyao chini mbona mrisho gambo kaufyata si amuweke lema ndani tena mbona anamkoromea kila siku na hajathubutu kuinua kinywa, muulize mrisho gambo anazunga na ving,ora tena pale Arusha, muulize Mrisho kwa nini hajafanya mkutano Arusha mjini, sawa na Makonda hawezi kuitisha mkutano zaidi yakuwatumia Home shopping centre aka GSM kwenye mish mishe zake
 
Mrisho Gamba ni dhaifu kama alivyo Makonda na wamewezwa mpaka vimbelembele vyao chini mbona mrisho gambo kaufyata si amuweke lema ndani tena mbona anamkoromea kila siku na hajathubutu kuinua kinywa, muulize mrisho gambo anazunga na ving,ora tena pale Arusha, muulize Mrisho kwa nini hajafanya mkutano Arusha mjini, sawa na Makonda hawezi kuitisha mkutano zaidi yakuwatumia Home shopping centre aka GSM kwenye mish mishe zake
Duh! Kama Makonda na Mrisho Gambo unawaona ni dhaifu basi wewe utakuwa ni mmoja kati ya wale wanne
 
Dah!!! Lizaboni, bro we umejuaje Lema halali ucngizi akimwazia cathetine?? unalala nae? au kuna tucchokijua... hahahah natania tu broo,, ila sitakagi ujinga mimi.
 
bandiko lako limekaa kimama mama tu, arusha ina raisi wake na raisi ni lema, juma mwenyee hatumtambui sembuse gumbo.
 
Back
Top Bottom