Mjumbe wa Kamati Kuu Chadema na Mbunge wa Jimbo la Arusha Godbless Lema leo ameanza rasmi kazi ya kusambaratisha CCM Arusha.
Lema ambaye ameamua kutembelea kata zote za Jimbo la Arusha kabla ya kurudi bungeni wiki ijayo leo alikuwa katika kata ya Kimandolu na Kaloleni.
Katika kata hiyo aliyoanza kutembelea tangu asubuhi amefanikiwa kuzindua mashina 12 ya CHADEMA.Akizungumza na wanachama katika maeneo hayo Lema alielezea kwa kina uonevu uliofanywa na mkuu wa mkoa Magessa Mulongo dhidi yake na CHADEMA kwa ujumla.
Wachambuzi wa siasa za Arusha wanasema mpaka kumaliza ziara hii katika kata zote Lema atakuwa ameijeruhi vibaya CCM.