Hatima ya uwepo wa CCM na CUF huku kusini ipo mikononi mwa CDM,Hakuna uchaguzi walioshinda ccm kwa kura ktk siku za hv karibuni huku.Kifupi wananchi tumeshawashitukia CCM na CUF ni dili moja,Kitu ambacho kimetufanya kutafuta ufumbuzi mbadala kwani wengi wetu tuliichagua CUF kutokana na kuikataa CCM kumbe mwisho wa siku m/kiti wa cuf taifa kakiunganisha na magamba kimyakimya.Amesahau kuwa sisi hatukukipenda CUF kutokana na uzuri wa sura wa viongozi wake badala yake tulikipenda kwa kuamini kina sera mbadala zitakazotutoa hapa tulipokwamishwa na ccm!.Kusini sasa sio kwamba wanakisikia tu CDM ila wanakiona kupitia vyombo ya habari makini hususani tv na mitandao ya kijamii pia,Ikumbukwe huku tuliwekwa ndani ya box kwa kurushiwa matangazo ya TBC taifa pekee! Bilashaka hakuna asiyejua utendaji wa sasa wa kituo hiki.Lkn sasa watu wametoka ndani ya box na kujua kuna vyanzo vingi vya habari na taarifa muhimu na vyenye kuaminika duniani kote tofauti na walivyokituaminisha hawa ccm zamani eti habari mzuri na yakuamini ni ile inayotolewa na vyombo vyao au vishirika na wao!,Tunawahitaji CDM kusini kwa sasa kuliko wakati wowote uliowahi kutokea! Ninarudia kusema tena kuwa unapoizungumzia kusini MOYO wake ni NACHINGWEA! CDM ikija kuisambaratisha rasmi ccm Nachingwea basi kazi imekwisha,Na kazi iliyobaki ni kidogo mnoo.Naamini CDM kikimpeleka Lema na Lisu wakawapa muda wa hata dk 45 tu kila mmoja! Kwa ninavyowafahamu hawa makamanda huu muda unawatosha kuizika ccm na mshirika wao Cuf kusini.Musiofu ikiwezekana waagizeni viongozi wenu wa kanda ya kusini watutangazie wananchi tuchangie hiyo ziara na mutashangazwa kwa jinsi gani watu watakavyojitolea kwa moyo mmoja kwa hari ma mali,Kusini hatuamini propaganda za kitoto zinazoenezwa wa baadhi ya wasioitakia mema nchi hii na chama hiki pendwa kuwa ni cha kikanda,kidini,Kikabila n.k. Kwani hatudanganyiki ng'o.Njooni CDM kusini mutuongoze kondoo wenu! Kwani imefika wakati hadi waliokaamia cuf wanafikiri kurudi ccm baada ya kuwagundua viongozi wa cuf niwasaliti. Mwisho kabisa niwakumbushe tu viongozi wa chama ninachikipenda CDM kuwa; Kufuru ya ccm kupitia mbunge woa Chikawe ya kuwagawia wananchi waliompigia kura zawadi za SANDA kila nyumba ndo inayowatafuna,Kile kitendo wananchi wamelia sana ndo maana hadi leo hii mh. Anaogopa kufanya mikutano ya hadhara na wananchi wa Nachingwea hususani maeneo ya tarafa za mjini.KARIBUNI CDM KUSINI ccm na washirka wao cuf hawana mpya na wenyewe wanalijua hilo ndo maana akili zao wanaelekeza kwenye kuiba kura tu.