Godbless Lema: Mungu tunakushukuru, Arusha asanteni sana

Watz wa a town wengi wa wanavuta ganja na lema sijui yumo """ nenda mtwara kama una ubavu

Haijalishi kwani ni aina ya kiamsha akili kuelekea kudai haki za msingi. Isingefaa sidhani kama gari za wausalama zingetembea nazo huku wengine wakizigeuza kuwa chumvi na sukari.
 
Nikurekebishe kidogo hapo. Tumeanza na Mungu na tutaendelea na MUNGU. Kumbuka kuwa 2015 siyo mwisho wa safari bali ndyo mwanzo kabisa wakuhitaji hekima na uongozi wa Munngu katika kuhakikisha tunaleta mabadiliko katika maisha ya watz na taifa kwa ujumla. Hekima, maarifa, vision vyote vitahitajika sana baada yakukamata dola na hapo ndipo tutakapomwitaji Mungu zaidi sana kuliko wakati wowote ule. I can say we need GOD always for the best Tanzania we need!


Tumeanza na Mungu tutamaliza na Mungu,CCM na pesa zao sisi na Watanzania wetu hongera Kamanda Lema,hongereni wat wa Arusha kwa kuonyesha njia

"Giza linapokuwa zito sana asubuhi inakaribia" Ahsante kamanda huu ni ukweli mtupu.
 
Hapo kwenye bold ni kweli kabisa Mkuu. Hili linaonyesha jinsi CHADEMA inavyowaheshimu wapiga kura ukilinganisha na CCM ambao wao rushwa ya ubwabwa, kofia, kanga, fulana za rangi yanga, pesa na vyakula kama vile unga na Michele ndio huvitumia ili kuwahonga wapiga kura na kasha kuwatelekeza. Chama kinachowaheshimu wapiga kura kamwe hakiwezi kutumia rushwa na hila mbali mbali za udanganyifu ili kushinda chaguzi.
G.Lema asante hata kwa kukumbuka kutoa neno la shukrani,
siyo kawaida kwa mwanasiasa kurudi na neno la 'ASANTE'

.........Asante zangu zikufikie kwa kujitoa mhanga kwa ajili ya ukombozi wa Tanzania.

Asanteni sana wana Arusha wote kwa moyo wa ujasiri mlio nao, siyo rahisi
kwa mtu wa kawaida kupigwa bomu na bado ukazidi kuwa jasiri kama wana
Arusha.

Nilikuwa namshangaa sana Arushaone aliposema anasimamia wapiga kura
kweli nilimwambia 'take care yourself'. Lakini Mungu aliwapigania na zoezi
likaisha tena kwa mafanikio makubwa.

Natamani kuona Tanzania ikiwa chini ya chama cha CHADEMA, natamani kuiona tena
Tanzania inayoongozwa kwa haki.
 
Mungu Awabariki Sana Wana Arusha Kwa Ujasiri Wenu Hakika Ingekuwa Sehemu Nyingine Ya Tz Kwa Majaribu Na Uonevu Mliofanyiwa Hakika Wasingestahimili!
Asante G Lema Kamanda,
Asante Samson Mwigamba,
Asante Aman Golungwa,
Asante Noel Olevaroya Na Makamanda Wengine Japo Orodha Ni Ndefu Sana!
.....asante sana......
 
Hii tunaiita systemati diagnosis ya CCM by Dr. Slaa wa CDM.......siku ya kura kabla ya saa 10 tayari CCM walishafungasha virago....
 
ninatafakari sana na ninaendelea kutafakari wema wa mungu katika harakati zetu za kutafuta uhuru wa kweli katika taifa letu , ushindi katika uchaguzi mdogo wa madiwani uliofanyika tarehe 14/7/2013 ni ushindi wa maana na muhimu sana katika siasa za tanzania na wala sio arusha peke yake , nchi nzima kuna furaha kwa watu wote wanaopenda mabadiliko na ndio maana tunasema “ mungu tunakushukuru , arusha asanteni sana “

ni uchaguzi uliowahi kuwa mchungu sana kwangu na watu wa arusha na tanzania nzima na pia ni uchaguzi uliokumbwa na mikasa na uadui mkubwa dhidi ya haki na maisha ya binadamu wa mungu. Najua tumeshinda uchaguzi huu lakini mioyo yetu ikiwa na majeruhi na mateso makubwa dhidi ya uonevu na mateso tunayoendelea kupewa . Wakati furaha hii ya ushindi ikiwa muhimu sana kwetu na katika siasa za nchi yetu ni muhimu pia kuwakumbuka ndugu , jamaa na watu walioumia na kupoteza maisha siku ya tarehe 15/6/2013 pale viwanja vya soweto baada ya bomu kupigwa kwenye mkutano wetu wa hadhara ambalo madhara yake ni makubwa zaidi katika mioyo ya watu wote wenye ni njema na amani ya taifa hili .

Ushindi huu tumepewa na mungu na wala sio akili zetu na kutambua hivi ni akili na maarifa makubwa , wengine tulipaswa kuwa tumekufa leo lakini tuko hai kwa sababu ya mungu na hata hivyo hatujui wamepanga kutuua lini tena lakini baada ya bomu la tarehe 15/6/2013 nikiwa nyumbani usiku wa manane natafakari mke wangu aliniambia “ kila mahali duniani kuna hatari , barabarani kuna ajali lakini hatuachi kuendesha magari , majumbani pia kuna hatari kwani umeme unaotumika majumbani unaweza kuwa balaa pia , kwa hiyo katika hali ya sasa ni muhimu kufikiria kupambana kwenda mbele , sisi kama familia tumeogopa na pengine ushauri wetu wa kwanza ungekuwa kukushauri uache siasa lakini mimi nakuambia songa mbele kupigani wema na hatari zote mungu hatawaponya godbless , nafikiri mimi nimefanywa kuona vizuri zaidi juu ya mnachokipigania . Wanataka kuwaua ? Kwanini ? Nitamuomba mungu damu za watu waliokufa mungu atalipa “ usiogope mume wangu , mungu anakusudi lake juu ya jambo hili subiri utaona “ neema lema .

na mimi nasema tanzania msiogope kwani giza nene linapozidi ndipo asubuhi ukaribia , mateso , dhihaka , dharau , kejeli na vipigo na mauaji ni mambo yanayoumiza mioyo yetu na yenu sana tunatembea na uchungu katika mioyo yetu lakini vumilieni bado kitambo kidogo sana mungu ataanza mwenyewe kulipa kisasi , vumilieni tena vumilieni hakuna dola inayotesa watu wake iatakayosimama mahali popote duniani “ only time will tell “ wengine wanasema tuvumilie kuonewa mpaka lini ? Na majibu yangu ni haya “ mpaka mungu atakapotoa maelekezo mengine , tutajuaje ? Msiogope , mtajua wakati ukifika lakini vumilieni tena mabadiliko yako karibu sana kwani serikali inayotawala sasa ina laana na vilio na damu za watu wengi katika viganja vyake kwa hiyo hawatafika mbali sana , mtaaona na mtakuja kusema niliwaambia .

Uchaguzi huu haukuwa wa huru na haki hata kidogo baada ya mabomu kampeni zilizuiwa kwa chadema takribani wiki tano lakini ccm na viongozi wake waliendelea na kampeni za nyumba kwa nyumba , tulizuiwa hata kuwatangazia watu tarehe ya kupiga kura kwa kutumia magari na vipaza sauti na tume ya uchaguzi pia haikufanya hivyo kwa makini hili ccm watumie mtandao wao wa mabalozi wa nyumba kumi kumi kuhamasisha wanachama wao kwenda kupiga kura na polisi pia waliendelea kutoa vitisho kwa wapiga kura hata sheria za msingi za uchaguzi zilibezwa na hakutakiwa mtu kuonekana kituo cha kupigia kura baada ya kupiga kura vitisho hivi viliongeza hofu kwa wapiga kura na kuogopa kujitokeza huku ccm wakiamini mtandao wao wa mabalozi ungetosha kuwapa ushindi na badala yake mabalozi wa ccm walibeba na kukumbusha watu kwenda kupiga kulikuwa na hila nyingi na mipango michafu mingi katika vituo vya kupigia kura , watu walipigwa na green guard na polisi bila kuchukua hatua yeyote . Ndio maana tunasema “ tunakushukuru mungu , arusha asanteni sana “

sasa tumerudisha viti vya madiwani tuliowafukuza ni fundisho kwa yeyote ndani ya chama chenu hatakayefikiri anaweza kucheza na masilahi ya umma na chama chenu na wananchi wa arusha wamepeleka salamu nzuri sana tanzania kwamba jina linalopendwa kuliko majina yote tanzania ni chadema na malengo yake , sio sura ya mtu wala umaarufu wake ni malengo ya chadema .
arusha mungu awabariki sana na tutaendelea kupigania haki , uhuru wa kweli , bila kuogopa matusi , kejeli , vipigo , na jela , watawatukana sana na kuwaumiza kwa njia mbali mbali kama ambavyo wengine wako magereza kwa tuhuma za uongo lakini msiogope

tunakushukuru sana mwenyezi mungu na watu wote arusha nawapongeza kwa ujasiri wenu na uvumilivu wenu hakika kila mmoja wetu amechangia ushindi huu wale ambao hawakuweza kuwa nasi mbele zaidi walikuwa nasi kwa maombi , dua na wengine walitupa maji ya kunywa , wazee wetu walioko majumbani pia walituombea kwa mungu.
Timu zote za kampeni katika kata zote wamefanya kazi ngumu bila malipo yeyote na vijana wetu wa ulinzi wameendelea kujitolea kulinda chama na wanchama kwa risk kubwa bila malipo yeyote kwa kweli kila mmoja wetu amekuwa muhimu kwetu hata wapinzani wetu na maadui zetu pia wamekuwa msaada kwani walifanya tufikirie zaidi ambayo imekuwa afya katika kupanga mikakati bora na imara zaidi .

Mwenyekiti wetu na katibu mkuu wetu wamefurahi sana lakini mh joseph mbilinyi (sugu ) yeye amelaumu sana kwanini ccm wamepata kura arusha na kwa niaba yenu nimefikiria na nimeamua kumuomba mh joseph mbilinyi ( sugu ) msamaha na kuhaidi kuwa wakati unaokuja tutajirekebisha juu ya jambo hili la kuhuzunisha kwa hizo kura walizopata ccm .
Nawapenda sana arusha , asanteni sana .

Ni mimi rafiki yenu .
godbless j lema ( mb)

mh. Godbless mungu akubariki sana,ujumbe wako karibu unitoe machozi japo umenitia moyo.hakika giza likisonga mapambazuko yamekaribia.mungu awalinde nyote na ninawapongeza sana watu wa arusha kwa umoja na uvumilivu wenu bila kujali kabila, dini au nasaba.god will reward your efforts na atalipa kisasi juu ya damu zilizomwagika na zitakazomwagika. Kusudi la mungu halibatilishwi na mwanadamu
 
Ninatafakari sana na ninaendelea kutafakari wema wa Mungu katika harakati zetu za kutafuta Uhuru wa kweli katika Taifa letu , ushindi katika uchaguzi mdogo wa Madiwani uliofanyika tarehe 14/7/2013 ni ushindi wa maana na muhimu sana katika Siasa za Tanzania na wala sio Arusha peke yake , Nchi nzima kuna furaha kwa watu wote wanaopenda mabadiliko na ndio maana tunasema “ MUNGU TUNAKUSHUKURU , ARUSHA ASANTENI SANA “

Ni uchaguzi uliowahi kuwa mchungu sana kwangu na watu wa Arusha na Tanzania nzima na pia ni uchaguzi uliokumbwa na mikasa na uadui mkubwa dhidi ya haki na maisha ya binadamu wa Mungu. Najua tumeshinda uchaguzi huu lakini mioyo yetu ikiwa na majeruhi na mateso makubwa dhidi ya uonevu na mateso tunayoendelea kupewa . Wakati furaha hii ya ushindi ikiwa muhimu sana kwetu na katika Siasa za Nchi yetu ni muhimu pia kuwakumbuka Ndugu , Jamaa na Watu walioumia na kupoteza maisha siku ya tarehe 15/6/2013 pale Viwanja vya Soweto baada ya bomu kupigwa kwenye mkutano wetu wa hadhara ambalo madhara yake ni makubwa zaidi katika mioyo ya Watu wote wenye ni njema na amani ya Taifa hili .

Ushindi huu tumepewa na Mungu na wala sio akili zetu na kutambua hivi ni akili na maarifa makubwa , Wengine tulipaswa kuwa tumekufa leo lakini tuko hai kwa sababu ya Mungu na hata hivyo hatujui wamepanga kutuua lini tena lakini baada ya bomu la tarehe 15/6/2013 nikiwa nyumbani usiku wa manane natafakari Mke wangu aliniambia “ Kila mahali Duniani kuna hatari , barabarani kuna ajali lakini hatuachi kuendesha magari , majumbani pia kuna hatari kwani umeme unaotumika majumbani unaweza kuwa balaa pia , kwa hiyo katika hali ya sasa ni muhimu kufikiria kupambana kwenda mbele , sisi kama familia tumeogopa na pengine ushauri wetu wa kwanza ungekuwa kukushauri uache Siasa lakini mimi nakuambia songa mbele kupigani wema na hatari zote Mungu hatawaponya Godbless , nafikiri mimi nimefanywa kuona vizuri zaidi juu ya mnachokipigania . Wanataka kuwaua ? kwanini ? nitamuomba Mungu damu za Watu waliokufa Mungu atalipa “ Usiogope Mume wangu , Mungu anakusudi lake juu ya jambo hili subiri utaona “ NEEMA LEMA .

Na Mimi nasema Tanzania Msiogope kwani giza nene linapozidi ndipo asubuhi ukaribia , mateso , dhihaka , dharau , kejeli na vipigo na mauaji ni mambo yanayoumiza mioyo yetu na yenu sana tunatembea na uchungu katika mioyo yetu lakini vumilieni bado kitambo kidogo sana Mungu ataanza mwenyewe kulipa kisasi , vumilieni tena vumilieni hakuna dola inayotesa watu wake iatakayosimama mahali popote Duniani “ Only time will tell “ wengine wanasema tuvumilie kuonewa mpaka lini ? na majibu yangu ni haya “ Mpaka Mungu atakapotoa maelekezo Mengine , Tutajuaje ? Msiogope , mtajua wakati ukifika lakini vumilieni tena mabadiliko yako karibu sana kwani Serikali inayotawala sasa ina laana na vilio na damu za watu wengi katika viganja vyake kwa hiyo hawatafika mbali sana , mtaaona na mtakuja kusema niliwaambia .

Uchaguzi huu haukuwa wa Huru na Haki hata kidogo baada ya mabomu kampeni zilizuiwa kwa Chadema takribani wiki tano lakini CCM na viongozi wake waliendelea na Kampeni za Nyumba kwa Nyumba , tulizuiwa hata kuwatangazia watu tarehe ya kupiga kura kwa kutumia magari na vipaza sauti na tume ya uchaguzi pia haikufanya hivyo kwa makini hili CCM watumie mtandao wao wa Mabalozi wa Nyumba kumi kumi kuhamasisha wanachama wao kwenda kupiga kura na Polisi pia waliendelea kutoa vitisho kwa wapiga kura hata sheria za msingi za uchaguzi zilibezwa na hakutakiwa Mtu kuonekana kituo cha kupigia kura baada ya kupiga kura vitisho hivi viliongeza hofu kwa wapiga kura na kuogopa kujitokeza huku CCM wakiamini mtandao wao wa Mabalozi ungetosha kuwapa ushindi na badala yake Mabalozi wa CCM walibeba na kukumbusha Watu kwenda kupiga kulikuwa na hila nyingi na mipango michafu mingi katika vituo vya kupigia kura , Watu walipigwa na Green Guard na polisi bila kuchukua hatua yeyote . Ndio maana tunasema “ TUNAKUSHUKURU MUNGU , ARUSHA ASANTENI SANA “

Sasa tumerudisha Viti vya Madiwani tuliowafukuza ni fundisho kwa yeyote ndani ya Chama chenu hatakayefikiri anaweza kucheza na masilahi ya UMMA na Chama chenu na Wananchi wa Arusha wamepeleka salamu nzuri sana Tanzania kwamba jina linalopendwa kuliko majina yote Tanzania ni CHADEMA na MALENGO YAKE , sio sura ya Mtu wala umaarufu wake ni MALENGO ya CHADEMA .
Arusha Mungu awabariki sana na tutaendelea kupigania haki , uhuru wa kweli , bila kuogopa matusi , kejeli , vipigo , na jela , watawatukana sana na kuwaumiza kwa njia mbali mbali kama ambavyo wengine wako magereza kwa tuhuma za uongo lakini MSIOGOPE

Tunakushukuru sana Mwenyezi Mungu na Watu wote Arusha nawapongeza kwa ujasiri wenu na uvumilivu wenu hakika kila mmoja wetu amechangia ushindi huu wale ambao hawakuweza kuwa nasi mbele zaidi walikuwa nasi kwa maombi , dua na wengine walitupa maji ya kunywa , Wazee wetu walioko majumbani pia walituombea kwa Mungu.
Timu zote za Kampeni katika kata zote wamefanya kazi ngumu bila malipo yeyote na vijana wetu wa ulinzi wameendelea kujitolea kulinda Chama na Wanchama kwa risk kubwa bila malipo yeyote kwa kweli kila mmoja wetu amekuwa muhimu kwetu hata Wapinzani wetu na Maadui zetu pia wamekuwa msaada kwani walifanya tufikirie zaidi ambayo imekuwa afya katika kupanga mikakati bora na imara zaidi .

Mwenyekiti wetu na Katibu Mkuu wetu wamefurahi sana lakini Mh Joseph Mbilinyi (Sugu ) yeye amelaumu sana kwanini CCM wamepata kura Arusha na kwa niaba yenu nimefikiria na nimeamua kumuomba Mh Joseph Mbilinyi ( Sugu ) msamaha na kuhaidi kuwa wakati unaokuja tutajirekebisha juu ya jambo hili la kuhuzunisha kwa hizo kura walizopata CCM .
Nawapenda sana Arusha , Asanteni sana .

Ni mimi Rafiki yenu .
Godbless J Lema ( MB)

Mungu akubariki Lema we na familia yako, na ninakuhakikishia watatupiga na kutuua lakini damu na machozi yetu yatakuwa laana kwao hao mafedhuli na kwetu yatakuwa baraka kwa wapenda ukombozi wa kweli.
MUNGU IBARIKI ARUSHA, MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
Hongereni wana Arusha, Hongera kamanda Lema.
UPENDO WA MUNGU BABA, NA USHIRIKA WA ROHO MTAKATIFU, UKAE NANYI WOTE, SASA NA HATA MILELE, AMEN!
 
waraka murua kabisa!

Umenigusa. The content and context altogether is emotional leave alone the factual side of it.

Kwa ufupi G. Lema yupo juu na sote tunakushukuru. You are becoming an icon of change kwa kuongoza mabadiliko ya kuleta ukombozi halisi katika nchi yetu.

God bless us all
 
Watz wa a town wengi wa wanavuta ganja na lema sijui yumo """ nenda mtwara kama una ubavu

Hana haja ya kwenda Mtwara kwani huko kuna Lema wengine wa kutosha. La msingi ni wananchi kutambua haki yao wataipata wapi kwani CCM imeshindwa kuwaonyesha njia!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom