Godbless Lema: Mungu tunakushukuru, Arusha asanteni sana

Nashukuru sana Mh. G. Lema!

Tupo pamoja mwanzo mwisho hakika tupo mstari wa mbele katika harakati zote na hakika Mwenyenzi MUNGU akiwa upande wetu hakika hakuna kuogopa chochote!
Mungi tunakushukuru kwa juhudi zako ya kibinafsi tunayoiona Mkubwa!
 
Last edited by a moderator:
Eti jina linalopendwa kuliko majina yote TZ ni chadema nasikia kutapika au umevurugwa wewe mpaka uamini ivyo? Endelea kujidanganya Arusha ndio TZ
Ninatafakari sana na ninaendelea kutafakari wema wa Mungu katika harakati zetu za kutafuta Uhuru wa kweli katika Taifa letu , ushindi katika uchaguzi mdogo wa Madiwani uliofanyika tarehe 14/7/2013 ni ushindi wa maana na muhimu sana katika Siasa za Tanzania na wala sio Arusha peke yake , Nchi nzima kuna furaha kwa watu wote wanaopenda mabadiliko na ndio maana tunasema " MUNGU TUNAKUSHUKURU , ARUSHA ASANTENI SANA "

Ni uchaguzi uliowahi kuwa mchungu sana kwangu na watu wa Arusha na Tanzania nzima na pia ni uchaguzi uliokumbwa na mikasa na uadui mkubwa dhidi ya haki na maisha ya binadamu wa Mungu. Najua tumeshinda uchaguzi huu lakini mioyo yetu ikiwa na majeruhi na mateso makubwa dhidi ya uonevu na mateso tunayoendelea kupewa . Wakati furaha hii ya ushindi ikiwa muhimu sana kwetu na katika Siasa za Nchi yetu ni muhimu pia kuwakumbuka Ndugu , Jamaa na Watu walioumia na kupoteza maisha siku ya tarehe 15/6/2013 pale Viwanja vya Soweto baada ya bomu kupigwa kwenye mkutano wetu wa hadhara ambalo madhara yake ni makubwa zaidi katika mioyo ya Watu wote wenye ni njema na amani ya Taifa hili .

Ushindi huu tumepewa na Mungu na wala sio akili zetu na kutambua hivi ni akili na maarifa makubwa , Wengine tulipaswa kuwa tumekufa leo lakini tuko hai kwa sababu ya Mungu na hata hivyo hatujui wamepanga kutuua lini tena lakini baada ya bomu la tarehe 15/6/2013 nikiwa nyumbani usiku wa manane natafakari Mke wangu aliniambia " Kila mahali Duniani kuna hatari , barabarani kuna ajali lakini hatuachi kuendesha magari , majumbani pia kuna hatari kwani umeme unaotumika majumbani unaweza kuwa balaa pia , kwa hiyo katika hali ya sasa ni muhimu kufikiria kupambana kwenda mbele , sisi kama familia tumeogopa na pengine ushauri wetu wa kwanza ungekuwa kukushauri uache Siasa lakini mimi nakuambia songa mbele kupigani wema na hatari zote Mungu hatawaponya Godbless , nafikiri mimi nimefanywa kuona vizuri zaidi juu ya mnachokipigania . Wanataka kuwaua ? kwanini ? nitamuomba Mungu damu za Watu waliokufa Mungu atalipa " Usiogope Mume wangu , Mungu anakusudi lake juu ya jambo hili subiri utaona " NEEMA LEMA .

Na Mimi nasema Tanzania Msiogope kwani giza nene linapozidi ndipo asubuhi ukaribia , mateso , dhihaka , dharau , kejeli na vipigo na mauaji ni mambo yanayoumiza mioyo yetu na yenu sana tunatembea na uchungu katika mioyo yetu lakini vumilieni bado kitambo kidogo sana Mungu ataanza mwenyewe kulipa kisasi , vumilieni tena vumilieni hakuna dola inayotesa watu wake iatakayosimama mahali popote Duniani " Only time will tell " wengine wanasema tuvumilie kuonewa mpaka lini ? na majibu yangu ni haya " Mpaka Mungu atakapotoa maelekezo Mengine , Tutajuaje ? Msiogope , mtajua wakati ukifika lakini vumilieni tena mabadiliko yako karibu sana kwani Serikali inayotawala sasa ina laana na vilio na damu za watu wengi katika viganja vyake kwa hiyo hawatafika mbali sana , mtaaona na mtakuja kusema niliwaambia .

Uchaguzi huu haukuwa wa Huru na Haki hata kidogo baada ya mabomu kampeni zilizuiwa kwa Chadema takribani wiki tano lakini CCM na viongozi wake waliendelea na Kampeni za Nyumba kwa Nyumba , tulizuiwa hata kuwatangazia watu tarehe ya kupiga kura kwa kutumia magari na vipaza sauti na tume ya uchaguzi pia haikufanya hivyo kwa makini hili CCM watumie mtandao wao wa Mabalozi wa Nyumba kumi kumi kuhamasisha wanachama wao kwenda kupiga kura na Polisi pia waliendelea kutoa vitisho kwa wapiga kura hata sheria za msingi za uchaguzi zilibezwa na hakutakiwa Mtu kuonekana kituo cha kupigia kura baada ya kupiga kura vitisho hivi viliongeza hofu kwa wapiga kura na kuogopa kujitokeza huku CCM wakiamini mtandao wao wa Mabalozi ungetosha kuwapa ushindi na badala yake Mabalozi wa CCM walibeba na kukumbusha Watu kwenda kupiga kulikuwa na hila nyingi na mipango michafu mingi katika vituo vya kupigia kura , Watu walipigwa na Green Guard na polisi bila kuchukua hatua yeyote . Ndio maana tunasema " TUNAKUSHUKURU MUNGU , ARUSHA ASANTENI SANA "

Sasa tumerudisha Viti vya Madiwani tuliowafukuza ni fundisho kwa yeyote ndani ya Chama chenu hatakayefikiri anaweza kucheza na masilahi ya UMMA na Chama chenu na Wananchi wa Arusha wamepeleka salamu nzuri sana Tanzania kwamba jina linalopendwa kuliko majina yote Tanzania ni CHADEMA na MALENGO YAKE , sio sura ya Mtu wala umaarufu wake ni MALENGO ya CHADEMA .
Arusha Mungu awabariki sana na tutaendelea kupigania haki , uhuru wa kweli , bila kuogopa matusi , kejeli , vipigo , na jela , watawatukana sana na kuwaumiza kwa njia mbali mbali kama ambavyo wengine wako magereza kwa tuhuma za uongo lakini MSIOGOPE

Tunakushukuru sana Mwenyezi Mungu na Watu wote Arusha nawapongeza kwa ujasiri wenu na uvumilivu wenu hakika kila mmoja wetu amechangia ushindi huu wale ambao hawakuweza kuwa nasi mbele zaidi walikuwa nasi kwa maombi , dua na wengine walitupa maji ya kunywa , Wazee wetu walioko majumbani pia walituombea kwa Mungu.
Timu zote za Kampeni katika kata zote wamefanya kazi ngumu bila malipo yeyote na vijana wetu wa ulinzi wameendelea kujitolea kulinda Chama na Wanchama kwa risk kubwa bila malipo yeyote kwa kweli kila mmoja wetu amekuwa muhimu kwetu hata Wapinzani wetu na Maadui zetu pia wamekuwa msaada kwani walifanya tufikirie zaidi ambayo imekuwa afya katika kupanga mikakati bora na imara zaidi .

Mwenyekiti wetu na Katibu Mkuu wetu wamefurahi sana lakini Mh Joseph Mbilinyi (Sugu ) yeye amelaumu sana kwanini CCM wamepata kura Arusha na kwa niaba yenu nimefikiria na nimeamua kumuomba Mh Joseph Mbilinyi ( Sugu ) msamaha na kuhaidi kuwa wakati unaokuja tutajirekebisha juu ya jambo hili la kuhuzunisha kwa hizo kura walizopata CCM .
Nawapenda sana Arusha , Asanteni sana .

Ni mimi Rafiki yenu .
Godbless J Lema ( MB)
 
Eti jina linalopendwa kuliko majina yote TZ ni chadema nasikia kutapika au umevurugwa wewe mpaka uamini ivyo? Endelea kujidanganya Arusha ndio TZ

Mkuu uko sahihi; ila ujue ni uhalisia wa kupenda kilicho dhaifu kinapokabiliana na changamoto za ukweli
 
thannnx mh lema mungu akiwa upande wetu nani alie juu yetu????? Hakuna asnteni arusha asante mungu
 
Amen, Mungu baba wa mbinguni uhimidiwe.
 
Asante Kamanda Lema. You're as impressive as you've always been.
Hongera sana na ubarikiwe kwa kazi na kujitoa kwako....kwani wewe ni zaidi ya mwanasiasa/mbunge
 
Mungu akupe Maisha marefu Godbless Lema.Kazi uliyofanya Arusha haitasahaulika kamwe.
 
Nimependa sana huu waraka Wa Mh. Lema na nampongeza kwa yote aliyoyafanya na kuyasimamia.

Natamani tungeweza kutenge nakala nyingi ili wapenda nchi na wale wanaosubiri kuongoka wausome!
 
Watz wa a town wengi wa wanavuta ganja na lema sijui yumo """ nenda mtwara kama una ubavu

umetokea wapi tena huku, mbona hapa sio mahali pako, wewe jukwaa linalokufaa ni lile la mambo ya udaku na mipasho hukooooooo facebook. Huku tuachie wenyewe PIMBI weye.

NB: HONGERENI SANA WANA WA ARUSHA KWA MOYO WA UVUMILIVU NA UKAKAMAVU. KILA LA HERI KATIKA KUENDELEZA JIJI LETU BAADA YA MUDA MREFU WA KUKALIWA NA HAYA MAHAYAWANI.

MZIKI WA CHADEMA CCM MTAUWEZA WAPIIIII!!!???
 
Tumekusoma Kamanda....sasa yatupasa kumuondosha meya wa kichina...uwepo wake ni ishara ya dhuluma

Ninatafakari sana na ninaendelea kutafakari wema wa Mungu katika harakati zetu za kutafuta Uhuru wa kweli katika Taifa letu , ushindi katika uchaguzi mdogo wa Madiwani uliofanyika tarehe 14/7/2013 ni ushindi wa maana na muhimu sana katika Siasa za Tanzania na wala sio Arusha peke yake , Nchi nzima kuna furaha kwa watu wote wanaopenda mabadiliko na ndio maana tunasema “ MUNGU TUNAKUSHUKURU , ARUSHA ASANTENI SANA “

Ni uchaguzi uliowahi kuwa mchungu sana kwangu na watu wa Arusha na Tanzania nzima na pia ni uchaguzi uliokumbwa na mikasa na uadui mkubwa dhidi ya haki na maisha ya binadamu wa Mungu. Najua tumeshinda uchaguzi huu lakini mioyo yetu ikiwa na majeruhi na mateso makubwa dhidi ya uonevu na mateso tunayoendelea kupewa . Wakati furaha hii ya ushindi ikiwa muhimu sana kwetu na katika Siasa za Nchi yetu ni muhimu pia kuwakumbuka Ndugu , Jamaa na Watu walioumia na kupoteza maisha siku ya tarehe 15/6/2013 pale Viwanja vya Soweto baada ya bomu kupigwa kwenye mkutano wetu wa hadhara ambalo madhara yake ni makubwa zaidi katika mioyo ya Watu wote wenye ni njema na amani ya Taifa hili .

Ushindi huu tumepewa na Mungu na wala sio akili zetu na kutambua hivi ni akili na maarifa makubwa , Wengine tulipaswa kuwa tumekufa leo lakini tuko hai kwa sababu ya Mungu na hata hivyo hatujui wamepanga kutuua lini tena lakini baada ya bomu la tarehe 15/6/2013 nikiwa nyumbani usiku wa manane natafakari Mke wangu aliniambia “ Kila mahali Duniani kuna hatari , barabarani kuna ajali lakini hatuachi kuendesha magari , majumbani pia kuna hatari kwani umeme unaotumika majumbani unaweza kuwa balaa pia , kwa hiyo katika hali ya sasa ni muhimu kufikiria kupambana kwenda mbele , sisi kama familia tumeogopa na pengine ushauri wetu wa kwanza ungekuwa kukushauri uache Siasa lakini mimi nakuambia songa mbele kupigani wema na hatari zote Mungu hatawaponya Godbless , nafikiri mimi nimefanywa kuona vizuri zaidi juu ya mnachokipigania . Wanataka kuwaua ? kwanini ? nitamuomba Mungu damu za Watu waliokufa Mungu atalipa “ Usiogope Mume wangu , Mungu anakusudi lake juu ya jambo hili subiri utaona “ NEEMA LEMA .

Na Mimi nasema Tanzania Msiogope kwani giza nene linapozidi ndipo asubuhi ukaribia , mateso , dhihaka , dharau , kejeli na vipigo na mauaji ni mambo yanayoumiza mioyo yetu na yenu sana tunatembea na uchungu katika mioyo yetu lakini vumilieni bado kitambo kidogo sana Mungu ataanza mwenyewe kulipa kisasi , vumilieni tena vumilieni hakuna dola inayotesa watu wake iatakayosimama mahali popote Duniani “ Only time will tell “ wengine wanasema tuvumilie kuonewa mpaka lini ? na majibu yangu ni haya “ Mpaka Mungu atakapotoa maelekezo Mengine , Tutajuaje ? Msiogope , mtajua wakati ukifika lakini vumilieni tena mabadiliko yako karibu sana kwani Serikali inayotawala sasa ina laana na vilio na damu za watu wengi katika viganja vyake kwa hiyo hawatafika mbali sana , mtaaona na mtakuja kusema niliwaambia .

Uchaguzi huu haukuwa wa Huru na Haki hata kidogo baada ya mabomu kampeni zilizuiwa kwa Chadema takribani wiki tano lakini CCM na viongozi wake waliendelea na Kampeni za Nyumba kwa Nyumba , tulizuiwa hata kuwatangazia watu tarehe ya kupiga kura kwa kutumia magari na vipaza sauti na tume ya uchaguzi pia haikufanya hivyo kwa makini hili CCM watumie mtandao wao wa Mabalozi wa Nyumba kumi kumi kuhamasisha wanachama wao kwenda kupiga kura na Polisi pia waliendelea kutoa vitisho kwa wapiga kura hata sheria za msingi za uchaguzi zilibezwa na hakutakiwa Mtu kuonekana kituo cha kupigia kura baada ya kupiga kura vitisho hivi viliongeza hofu kwa wapiga kura na kuogopa kujitokeza huku CCM wakiamini mtandao wao wa Mabalozi ungetosha kuwapa ushindi na badala yake Mabalozi wa CCM walibeba na kukumbusha Watu kwenda kupiga kulikuwa na hila nyingi na mipango michafu mingi katika vituo vya kupigia kura , Watu walipigwa na Green Guard na polisi bila kuchukua hatua yeyote . Ndio maana tunasema “ TUNAKUSHUKURU MUNGU , ARUSHA ASANTENI SANA “

Sasa tumerudisha Viti vya Madiwani tuliowafukuza ni fundisho kwa yeyote ndani ya Chama chenu hatakayefikiri anaweza kucheza na masilahi ya UMMA na Chama chenu na Wananchi wa Arusha wamepeleka salamu nzuri sana Tanzania kwamba jina linalopendwa kuliko majina yote Tanzania ni CHADEMA na MALENGO YAKE , sio sura ya Mtu wala umaarufu wake ni MALENGO ya CHADEMA .
Arusha Mungu awabariki sana na tutaendelea kupigania haki , uhuru wa kweli , bila kuogopa matusi , kejeli , vipigo , na jela , watawatukana sana na kuwaumiza kwa njia mbali mbali kama ambavyo wengine wako magereza kwa tuhuma za uongo lakini MSIOGOPE

Tunakushukuru sana Mwenyezi Mungu na Watu wote Arusha nawapongeza kwa ujasiri wenu na uvumilivu wenu hakika kila mmoja wetu amechangia ushindi huu wale ambao hawakuweza kuwa nasi mbele zaidi walikuwa nasi kwa maombi , dua na wengine walitupa maji ya kunywa , Wazee wetu walioko majumbani pia walituombea kwa Mungu.
Timu zote za Kampeni katika kata zote wamefanya kazi ngumu bila malipo yeyote na vijana wetu wa ulinzi wameendelea kujitolea kulinda Chama na Wanchama kwa risk kubwa bila malipo yeyote kwa kweli kila mmoja wetu amekuwa muhimu kwetu hata Wapinzani wetu na Maadui zetu pia wamekuwa msaada kwani walifanya tufikirie zaidi ambayo imekuwa afya katika kupanga mikakati bora na imara zaidi .

Mwenyekiti wetu na Katibu Mkuu wetu wamefurahi sana lakini Mh Joseph Mbilinyi (Sugu ) yeye amelaumu sana kwanini CCM wamepata kura Arusha na kwa niaba yenu nimefikiria na nimeamua kumuomba Mh Joseph Mbilinyi ( Sugu ) msamaha na kuhaidi kuwa wakati unaokuja tutajirekebisha juu ya jambo hili la kuhuzunisha kwa hizo kura walizopata CCM .
Nawapenda sana Arusha , Asanteni sana .

Ni mimi Rafiki yenu .
Godbless J Lema ( MB)
 
Ninatafakari sana na ninaendelea kutafakari wema wa Mungu katika harakati zetu za kutafuta Uhuru wa kweli katika Taifa letu , ushindi katika uchaguzi mdogo wa Madiwani uliofanyika tarehe 14/7/2013 ni ushindi wa maana na muhimu sana katika Siasa za Tanzania na wala sio Arusha peke yake , Nchi nzima kuna furaha kwa watu wote wanaopenda mabadiliko na ndio maana tunasema “ MUNGU TUNAKUSHUKURU , ARUSHA ASANTENI SANA “

Ni uchaguzi uliowahi kuwa mchungu sana kwangu na watu wa Arusha na Tanzania nzima na pia ni uchaguzi uliokumbwa na mikasa na uadui mkubwa dhidi ya haki na maisha ya binadamu wa Mungu. Najua tumeshinda uchaguzi huu lakini mioyo yetu ikiwa na majeruhi na mateso makubwa dhidi ya uonevu na mateso tunayoendelea kupewa . Wakati furaha hii ya ushindi ikiwa muhimu sana kwetu na katika Siasa za Nchi yetu ni muhimu pia kuwakumbuka Ndugu , Jamaa na Watu walioumia na kupoteza maisha siku ya tarehe 15/6/2013 pale Viwanja vya Soweto baada ya bomu kupigwa kwenye mkutano wetu wa hadhara ambalo madhara yake ni makubwa zaidi katika mioyo ya Watu wote wenye ni njema na amani ya Taifa hili .

Ushindi huu tumepewa na Mungu na wala sio akili zetu na kutambua hivi ni akili na maarifa makubwa , Wengine tulipaswa kuwa tumekufa leo lakini tuko hai kwa sababu ya Mungu na hata hivyo hatujui wamepanga kutuua lini tena lakini baada ya bomu la tarehe 15/6/2013 nikiwa nyumbani usiku wa manane natafakari Mke wangu aliniambia “ Kila mahali Duniani kuna hatari , barabarani kuna ajali lakini hatuachi kuendesha magari , majumbani pia kuna hatari kwani umeme unaotumika majumbani unaweza kuwa balaa pia , kwa hiyo katika hali ya sasa ni muhimu kufikiria kupambana kwenda mbele , sisi kama familia tumeogopa na pengine ushauri wetu wa kwanza ungekuwa kukushauri uache Siasa lakini mimi nakuambia songa mbele kupigani wema na hatari zote Mungu hatawaponya Godbless , nafikiri mimi nimefanywa kuona vizuri zaidi juu ya mnachokipigania . Wanataka kuwaua ? kwanini ? nitamuomba Mungu damu za Watu waliokufa Mungu atalipa “ Usiogope Mume wangu , Mungu anakusudi lake juu ya jambo hili subiri utaona “ NEEMA LEMA .

Na Mimi nasema Tanzania Msiogope kwani giza nene linapozidi ndipo asubuhi ukaribia , mateso , dhihaka , dharau , kejeli na vipigo na mauaji ni mambo yanayoumiza mioyo yetu na yenu sana tunatembea na uchungu katika mioyo yetu lakini vumilieni bado kitambo kidogo sana Mungu ataanza mwenyewe kulipa kisasi , vumilieni tena vumilieni hakuna dola inayotesa watu wake iatakayosimama mahali popote Duniani “ Only time will tell “ wengine wanasema tuvumilie kuonewa mpaka lini ? na majibu yangu ni haya “ Mpaka Mungu atakapotoa maelekezo Mengine , Tutajuaje ? Msiogope , mtajua wakati ukifika lakini vumilieni tena mabadiliko yako karibu sana kwani Serikali inayotawala sasa ina laana na vilio na damu za watu wengi katika viganja vyake kwa hiyo hawatafika mbali sana , mtaaona na mtakuja kusema niliwaambia .

Uchaguzi huu haukuwa wa Huru na Haki hata kidogo baada ya mabomu kampeni zilizuiwa kwa Chadema takribani wiki tano lakini CCM na viongozi wake waliendelea na Kampeni za Nyumba kwa Nyumba , tulizuiwa hata kuwatangazia watu tarehe ya kupiga kura kwa kutumia magari na vipaza sauti na tume ya uchaguzi pia haikufanya hivyo kwa makini hili CCM watumie mtandao wao wa Mabalozi wa Nyumba kumi kumi kuhamasisha wanachama wao kwenda kupiga kura na Polisi pia waliendelea kutoa vitisho kwa wapiga kura hata sheria za msingi za uchaguzi zilibezwa na hakutakiwa Mtu kuonekana kituo cha kupigia kura baada ya kupiga kura vitisho hivi viliongeza hofu kwa wapiga kura na kuogopa kujitokeza huku CCM wakiamini mtandao wao wa Mabalozi ungetosha kuwapa ushindi na badala yake Mabalozi wa CCM walibeba na kukumbusha Watu kwenda kupiga kulikuwa na hila nyingi na mipango michafu mingi katika vituo vya kupigia kura , Watu walipigwa na Green Guard na polisi bila kuchukua hatua yeyote . Ndio maana tunasema “ TUNAKUSHUKURU MUNGU , ARUSHA ASANTENI SANA “

Sasa tumerudisha Viti vya Madiwani tuliowafukuza ni fundisho kwa yeyote ndani ya Chama chenu hatakayefikiri anaweza kucheza na masilahi ya UMMA na Chama chenu na Wananchi wa Arusha wamepeleka salamu nzuri sana Tanzania kwamba jina linalopendwa kuliko majina yote Tanzania ni CHADEMA na MALENGO YAKE , sio sura ya Mtu wala umaarufu wake ni MALENGO ya CHADEMA .
Arusha Mungu awabariki sana na tutaendelea kupigania haki , uhuru wa kweli , bila kuogopa matusi , kejeli , vipigo , na jela , watawatukana sana na kuwaumiza kwa njia mbali mbali kama ambavyo wengine wako magereza kwa tuhuma za uongo lakini MSIOGOPE

Tunakushukuru sana Mwenyezi Mungu na Watu wote Arusha nawapongeza kwa ujasiri wenu na uvumilivu wenu hakika kila mmoja wetu amechangia ushindi huu wale ambao hawakuweza kuwa nasi mbele zaidi walikuwa nasi kwa maombi , dua na wengine walitupa maji ya kunywa , Wazee wetu walioko majumbani pia walituombea kwa Mungu.
Timu zote za Kampeni katika kata zote wamefanya kazi ngumu bila malipo yeyote na vijana wetu wa ulinzi wameendelea kujitolea kulinda Chama na Wanchama kwa risk kubwa bila malipo yeyote kwa kweli kila mmoja wetu amekuwa muhimu kwetu hata Wapinzani wetu na Maadui zetu pia wamekuwa msaada kwani walifanya tufikirie zaidi ambayo imekuwa afya katika kupanga mikakati bora na imara zaidi .

Mwenyekiti wetu na Katibu Mkuu wetu wamefurahi sana lakini Mh Joseph Mbilinyi (Sugu ) yeye amelaumu sana kwanini CCM wamepata kura Arusha na kwa niaba yenu nimefikiria na nimeamua kumuomba Mh Joseph Mbilinyi ( Sugu ) msamaha na kuhaidi kuwa wakati unaokuja tutajirekebisha juu ya jambo hili la kuhuzunisha kwa hizo kura walizopata CCM .
Nawapenda sana Arusha , Asanteni sana .

Ni mimi Rafiki yenu .
Godbless J Lema ( MB)

kakangu na mbunge wangu mpendwa Lema pole kwa kazi nzito. Tunakupenda sana Lema wewe ni msema kweli na ukweli wako mpaka leo umesimama. Mungu atakulinda na nakuhakikishia tuko tayari kufa wote kupigania haki, cc watutaki ufalme wa duniani tunapenda ufalme wa kweli mbinguni, tuko pamoja katika mapambano na kumwomba mungu atupe nguvu na imani zaidi. CHADEMA tunawapenda wote mungu awabariki kwani ni katika kipindi chenu tumejua nchi hii inaliwa na wachache kutoka CCM, Mungu awabariki na awalinde daima
 
Kamanda hongereni. Tunamshukuru mungu kwakoa ametimiza ahadi yake kwa watu wake. Binafsi nilijua tutashinda ila nilishtushwa sana na namna ya ujasiri wa kijangili na dhuluma zidi ya haki ya watu kuishi na haki ya watu kushiriki katika kuhamua hatma yao ya kisiasa. Kujichagulia viongozi watakao waongoza wao. Tunautoa ushindi huu kwa makamanda wetu waliopoteza maisha na waliojeruhiwa vibaya katika kuhakikisha ushindi huu. Mungu akiwa upande wetu ni nani alie juu yetu?
Imenuchukua muda kidogo kuutafakari ushindi huu na mwenendo mzima wa uchaguzi huu nikajifunza mambo makubwa matatu
1. Hakuna nguvu yoyote duniani inayoweza kushinda nguvu ya umma. Umma ukitaka, hakuna mamlaka itakayoweza kuwalazimisha.
2.Dhuluma na udhalimu hujenga ushupavu na ujasiri wa kutetea haki. Tumejengeka zaidi kutokana na njama za kidhalimu na unyanyasaji unaoendelea kufanyika zidi ya wazalendo na makamanda wenzetu
3.Ukombozi ni sasa na watanzania wako tayari kwa ukombozi wa kweli na uhuru wa kweli. Iwe kwa mateso na hujuma iwayo yote... Nakumbuka maneno ya comrade sugu... Huwezi zuia mvua..kama yanyesha yanesha tu... Ni msimu wa mvua lazma inyeshe. Maccm hawawezi zuia wimbi hili la mabadiliko maana kwa wingi au uchache wetu mabadiliko yatakuja.

Walitupiga, tukajipa nguvu na moyo tukasonga mbele, wakapunguza idadi ya kura zetu kwa vitisho na kupunguza majina, wakapata ujumbe kwamba hata wale wachache walio amini wako upande wao wako upande wa ukweli ka haki tukashinda, wakatupiga mabomu.
Jan 5 mashujaa tunawakumbuka, wakawapa majina na kuwatesa makamanda wetu wakazaliwa na kuishi makamanda wapya. Arusha wameweka standards, wametuma ujumbe na wametoa taswira ya Tanzania. Makamanda na watz wote tupeane shime.. Makamanda wote tuwe na sehemu ya kazi ya Mnyika.. Kwa nafasi na fursa zetu tueneze ujumbe wa ukombozi... Tuwaandae watanzania kuhama kwenye dhiki na dhuluma kwenda kwenye haki na neema, tuwaandae kutoka kwenye zama za wananchi kuitumikia serikali kwenda kwenye zama za serikali kuwajibika kwa wananchi kutoka kiangazi kwenda kwa masika

Tuutumie ushindi huu na fursa hii kuwaandaa watz kwa ushindi mkuu ujao.

Asanteni
 
G.lema ni kichwa...huyu jamaa ana busara sana ni vile tu ccm wanapenda ufisadi ndio maana wanamuona ni adui yao mkubwa.Mungu akubariki sana mh.Lema
 
27926_300536303400033_1520956517_n.jpg
 
Back
Top Bottom